Hadithi

Hassan na Hussein ni mabosi wa vijana wa peponi

Chanzo: HadeethEnc.com, Kiswahili v1.18.0

SahihiImepokelewa na Tirmidhiy na Ahmad

Matini ya Kiarabu

عن أبي سعيد الخدري رضي الله عنه قال: قال رسول الله صلى الله عليه وسلم: «الحَسَن والحُسَيْن سَيِّدا شَباب أهْل الجنة».

Tafsiri

Imepokelewa kutoka kwa Saidi Al-Khuduriy -radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake- amesema: Amesema Mtume -rehema na amani ziwe juu yake-: "Hassan na Hussein ni mabosi wa vijana wa peponi".

Ufafanuzi

Alieleza Mtume -rehema na amani ziwe juu yake kuwa wajukuu zake Hassan na Hussein watoto wa Ally bin Abii Twalib na Fatma binti wa Mtume -rehema na amani ziwe juu yake na Allah amridhie, wao ni mabosi katika fadhila wa kila aliyekufa akiwa kijana na akaingia peponi, au wao ni mabosi wa vijana wa watu wa peponi, kasoro Manabii na Mahalifa (viongozi) waongofu.

Mafunzo

  • Hapa kuna fadhila za wazi za Hassan na Hussein radhi za Allah ziwe juu yao.
  • Imesemekana katika maana ya hadithi kuwa: Wao wakati wa kuzungumzwa hadithi hii walikuwa ndio mabosi wa vijana wa wale miongoni mwao watakaokuwa katika watu wa peponi katika vijana wa zama hizi, au wao ni bora kuliko yule ambaye fadhila zake hazijathibiti kwa ujumla kama Manabii na Mahalifa (viongozi), au wao ni mabosi wa kila mwenye kusifika na sifa ya ujana, kama murua (heshima) na ukarimu na ushujaa, na haukutajwa umri maalumu wa ujana; kwa sababu Hassan na Hussein walikufa wakiwa watu wazima.
Ufafanuzi: العربية

أَخْبَرَ النبيُّ صلى الله عليه وسلم أنَّ حَفيدَيه الحسن والحسين ابنا علي بن أبي طالب وفاطمة بنت النبي صلى الله عليه وسلم ورضي عنهم، هما سيدا كلِّ مَن مات وهو شاب ودخل الجنة في الفضل، أو أنهما سيدا شباب أهل الجنة باستثناء الأنبياء والخلفاء الراشدين.

  • فيه فضيلة ظاهرة للحسن والحسين رضي الله عنهما.
  • قيل في معنى الحديث: أنهما في وقت الحديث هما سيدا شباب مَن هم من أهل الجنة من شُبّان هذا الزمان، أو أنهما أفضل ممن لم يثبت فيه تفضيلٌ عامٌّ كالأنبياء والخلفاء، أو أنهما سيدا من اتصف بصفات الشباب والفُتُوَّة كالمروءة والكرم والشجاعة، ولم يَرِدْ بذلك سِنَّ الشباب؛ لأن الحسن والحسين ماتا كَهْلَين.

Mada

Ripoti kosa

Zaidi