Chanzo: HadeethEnc.com, Kiswahili v1.18.0
Matini ya Kiarabu
عَنْ عَبْدِ اللَّهِ بْنِ عُمَرَ رَضِيَ اللَّهُ عَنْهُمَا: أَنَّ رَسُولَ اللَّهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ قَالَ: «إِنَّ أَحَدَكُمْ إِذَا مَاتَ عُرِضَ عَلَيْهِ مَقْعَدُهُ بِالْغَدَاةِ وَالعَشِيِّ، إِنْ كَانَ مِنْ أَهْلِ الجَنَّةِ فَمِنْ أَهْلِ الجَنَّةِ، وَإِنْ كَانَ مِنْ أَهْلِ النَّارِ فَمِنْ أَهْلِ النَّارِ، فَيُقَالُ: هَذَا مَقْعَدُكَ حَتَّى يَبْعَثَكَ اللَّهُ يَوْمَ القِيَامَةِ».
Tafsiri
Kutoka kwa Abdillah bin Omari radhi za Allah ziwe juu yao: Yakwamba Mtume rehema na amani za Allah ziwe juu yake amesema: "Hakika mmoja wenu anapokufa huonyeshwa makao yake asubuhi na jioni, akiwa katika watu wa peponi basi huonyeshwa katika watu wa peponi, na akiwa katika watu wa motoni basi huonyeshwa katika watu wa motoni, basi husemwa: Haya ndiyo makao yako mpaka atakapokufufua Mwenyezi Mungu siku ya Kiyama".
Ufafanuzi
Ameeleza Mtume rehema na amani ziwe juu yake ya kwamba mja anapokufa huonyeshwa mbele yake makao yake na sehemu yake maalumu peponi au motoni, mwanzo wa mchana na mwisho wake; mahali pake peponi, na sehemu yake motoni akiwa ni miongoni mwa watu wa motoni, na huambiwa: Haya ndiyo makao yako utakayofufuliwa kwayo siku ya Kiyama; na katika hilo kuna kuneemeka kwa muumini, na kuadhibiwa kwa kafiri.
Mafunzo
- Adhabu za kaburi na neema zake ni kweli.
- Amesema bin Hajari: Hakika kuonyeshwa huku kwa muumini na kafiri kuko wazi, na ama muumini aliyechanganya mema na maovu inategemea anaweza kuonyeshwa makao yake katika pepo atakayofikia.
Ufafanuzi: العربية
أخبر النبي صلى الله عليه وسلم أن العبد إذا مات عُرِضَ عليه نُزُلُه ومكانه الخاص من الجنة أو النار، أول النهار وآخره؛ مكانه في الجنة إن كان من أهل الجنة، ومكانه في النار إن كان من أهل النار، ويُقال له: هذا مقعدك الذي تبعث إليه يوم القيامة؛ وفي ذلك تنعيم للمؤمن، وتعذيب للكافر.
- عذاب القبر ونعيمه حقٌّ.
- قال ابن حجر: إن هذا العرض للمؤمن المتقي والكافر ظاهر، وأما المؤمن المُخلّط فيحتمل أيضًا أن يعرض عليه مقعده من الجنة التي سيصير إليها.