Hadithi

Hakika wewe utaiendea jamii ya watu wa kitabu (Mayahudi na Wakristo), utakapowajia basi waite kushuhudia kuwa hapana Mola apasaye kuabudiwa kwa haki isipokuwa Mwenyezi Mungu, nakuwa Muhammadi ni Mjumbe wa Mwenyezi Mungu

Chanzo: HadeethEnc.com, Kiswahili v1.18.0

SahihiWamekubaliana Bukhari na Muslim juu ya usahihi wake

Matini ya Kiarabu

عَنِ ابْنِ عَبَّاسٍ رَضِيَ اللَّهُ عَنْهُمَا قَالَ: قَالَ رَسُولُ اللهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ لِمُعَاذِ بْنِ جَبَلٍ، حِينَ بَعَثَهُ إِلَى الْيَمَنِ: «إِنَّكَ سَتَأْتِي قَوْمًا أَهْلَ كِتَابٍ، فَإِذَا جِئْتَهُمْ فَادْعُهُمْ إِلَى أَنْ يَشْهَدُوا أَنْ لَا إِلَهَ إِلَّا اللهُ، وَأَنَّ مُحَمَّدًا رَسُولُ اللهِ، فَإِنْ هُمْ أَطَاعُوا لَكَ بِذَلِكَ، فَأَخْبِرْهُمْ أَنَّ اللهَ قَدْ فَرَضَ عَلَيْهِمْ خَمْسَ صَلَوَاتٍ فِي كُلِّ يَوْمٍ وَلَيْلَةٍ، فَإِنْ هُمْ أَطَاعُوا لَكَ بِذَلِكَ، فَأَخْبِرْهُمْ أَنَّ اللهَ قَدْ فَرَضَ عَلَيْهِمْ صَدَقَةً تُؤْخَذُ مِنْ أَغْنِيَائِهِمْ فَتُرَدُّ عَلَى فُقَرَائِهِمْ، فَإِنْ هُمْ أَطَاعُوا لَكَ بِذَلِكَ، فَإِيَّاكَ وَكَرَائِمَ أَمْوَالِهِمْ، وَاتَّقِ دَعْوَةَ الْمَظْلُومِ، فَإِنَّهُ لَيْسَ بَيْنَهُ وَبَيْنَ اللهِ حِجَابٌ».

Tafsiri

Imepokelewa Kutoka kwa bin Abbasi -Radhi za Allah ziwe juu yao- Amesema: Alisema Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- kumwambia Muadhi Ibn Jabal, alipomtuma kwenda Yemen: "Hakika wewe utaiendea jamii ya watu wa kitabu (Mayahudi na Wakristo), utakapowajia basi waite kushuhudia kuwa hapana Mola apasaye kuabudiwa kwa haki isipokuwa Mwenyezi Mungu, nakuwa Muhammadi ni Mjumbe wa Mwenyezi Mungu Ikiwa watakutii kwa hilo, basi waeleze kuwa Mwenyezi Mungu amewalazimisha juu yao swala tano katika kila usiku na mchana, ikiwa watakutii kwa hilo, basi waeleze kuwa Mwenyezi Mungu amewalazimisha juu yao zaka, huchukuliwa kutoka kwa matajiri wao na kurudishwa kwa mafukara wao, ikiwa watakutii kwa hilo, basi jiepushe na mali zao za thamani, na ogopa maombi ya mwenye kudhulumiwa, kwani maombi hayo hayana baina yake na Mwenyezi Mungu kizuizi".

Ufafanuzi

Alipomtuma Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- Muadhi Ibn Jabal -Radhi za Allah ziwe juu yake- kwenda katika miji ya Yemen kama mlinganizi wa kuwaita watu kwa Mwenyezi Mungu na kama mwalimu, alimuweka wazi kuwa atakumbana na jamii ya Wakristo; ili awe na maandalizi, kisha aanze katika kuwaita kwake na mambo muhimu zaidi kisha yanayofuatia, Atawaita kurekebisha itikadi kwanza; washuhudie kuwa hapana Mola apasaye kuabudiwa kwa haki isipokuwa Mwenyezi Mungu, nakuwa Muhammad ni Mjumbe wa Mwenyezi Mungu; Kwa sababu wao kwa itikadi hiyo yakuwa hapana mola apasae kuabudiwa kwa haki isipokuwa Mwenyezi Mungu peke yake; wataingia katika Uislamu, ikiwa watatii hilo basi awaamrishe wasimamishe swala; kwani huo ndio wajibu mkubwa baada ya tauhidi, Watakapoisimamisha awaamrishe matajiri wao kutoa zaka ya mali zao kuwapa mafukara wao, kisha akamtahadharisha na kuchukua mali bora; kwa sababu ya wajibu ni mali ya kati na kati, Kisha akamuusia aiepuke dhulma; asijekumuombewa dua mbaya aliyemdhulumu, kwani dua yake hupokelewa.

Mafunzo

  • Maana ya kushuhudia kuwa hapana Mola apasaye kuabudiwa kwa haki isipokuwa Allah, ni kumfanya Allah kuwa wa pekee kwa ibada, na kuacha kuabudu visivyokuwa Yeye.
  • Maana ya kushuhudia kuwa Muhammad ni Mjumbe wa Mwenyezi Mungu; Ni kumuamini yeye na yale aliyokuja nayo na kumsadikisha, nakuwa yeye ni wa mwisho katika Wajumbe wa Mwenyezi Mungu kuja kwa wanadamu.
  • Nikuwa kujadiliana na msomi mwenye hoja tata si sawa na kujadiliana na mjinga; Ndio maana alimtanabahisha Muadhi kwa kumwambia: "Hakika wewe unakwenda katika jamii ya watu wa kitabu".
  • Kuna umuhimu wa muislamu kuwa na uelewa katika dini yake; ili asalimike na upotovu wa wenye kumtia utata, na hii inakuwa kwa kutafuta elimu.
  • Ubatili wa dini ya Mayahudi na Wakristo baada ya kutumwa Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake-, nakuwa wao si miongoni mwa watakao okoka siku ya Kiyama mpaka waingie katika dini Uislamu, na wamuamini Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake-.
Ufafanuzi: العربية

لما أَرسلَ النبيُّ صلى الله عليه وسلم معاذَ بن جبل رضي الله عنه إلى بلاد اليمن داعيًا إلى الله ومُعلِّمًا، بَيَّنَ له أنه سيواجه قومًا من النصارى؛ ليكون على استعداد لهم، ثم ليبدأ في دعوتهم بالأهم فالأهم، فيدعوهم إلى إصلاح العقيدة أولًا؛ بأن يشهدوا أن لا إله إلا الله، وأن محمدا رسول الله؛ لأنهم بها يدخلون الإسلام، فإذا انقادوا لذلك أمرهم بإقام الصلاة؛ لأنها أعظم الواجبات بعد التوحيد، فإذا أقاموها أمر أغنياءهم بدفع زكاة أموالهم إلى فقرائهم. ثم حذّره من أخذ أفضل المال؛ لأن الواجب الوسط. ثم أوصاه باجتناب الظلم؛ لئلا يدعو عليه المظلوم، فإن دعوته مستجابة.

  • معنى شهادة أن لا إله إلا الله هو إفراد الله بالعبادة، وترك عبادة ما سواه.
  • معنى شهادة أن محمدًا رسول الله هو الإيمان به وبما جاء به وتصديقه وأنه آخر رسل الله إلى البشرية.
  • مخاطبة العالِم ومَن لديه شُبهات ليست كمخاطبة الجاهل؛ لذا نَبَّه معاذًا بقوله: "إنك تأتي قومًا أهل كتاب".
  • أهمية أن يكون المسلم على بصيرة من دينه؛ ليَتَخلَّص من شُبهات المشبِّهين، وذلك بطلب العلم.
  • بطلان دين اليهود والنصارى بعد بعثة الرسول صلى الله عليه وسلم، وأنهم ليسوا من أهل النجاة يوم القيامة حتى يدخلوا في دين الإسلام، ويؤمنوا بالنبي صلى الله عليه وسلم.

Mada

Ripoti kosa

Zaidi