Chanzo: HadeethEnc.com, Kiswahili v1.18.0
Matini ya Kiarabu
عن سَعِيدِ بْنِ الْمُسَيَّبِ، عَنْ أَبِيهِ قَالَ: لَمَّا حَضَرَتْ أَبَا طَالِبٍ الْوَفَاةُ، جَاءَهُ رَسُولُ اللهِ صلى الله عليه وسلم فَوَجَدَ عِنْدَهُ أَبَا جَهْلٍ وَعَبْدَ اللهِ بْنَ أَبِي أُمَيَّةَ بْنِ الْمُغِيرَةِ، فَقَالَ: «أَيْ عَمِّ، قُلْ: لَا إِلَهَ إِلَّا اللهُ، كَلِمَةً أُحَاجُّ لَكَ بِهَا عِنْدَ اللهِ»، فَقَالَ أَبُو جَهْلٍ وَعَبْدُ اللهِ بْنُ أَبِي أُمَيَّةَ: أَتَرْغَبُ عَنْ مِلَّةِ عَبْدِ الْمُطَّلِبِ، فَلَمْ يَزَلْ رَسُولُ اللهِ صلى الله عليه وسلم يَعْرِضُهَا عَلَيْهِ، وَيُعِيدَانِهِ بِتِلْكَ الْمَقَالَةِ، حَتَّى قَالَ أَبُو طَالِبٍ آخِرَ مَا كَلَّمَهُمْ: عَلَى مِلَّةِ عَبْدِ الْمُطَّلِبِ، وَأَبَى أَنْ يَقُولَ: لَا إِلَهَ إِلَّا اللهُ، قَالَ: قَالَ رَسُولُ اللهِ صلى الله عليه وسلم: «وَاللهِ لَأَسْتَغْفِرَنَّ لَكَ مَا لَمْ أُنْهَ عَنْكَ»، فَأَنْزَلَ اللهُ: {مَا كَانَ لِلنَّبِيِّ وَالَّذِينَ آمَنُوا أَنْ يَسْتَغْفِرُوا لِلْمُشْرِكِينَ} [التوبة: 113]، وَأَنْزَلَ اللهُ فِي أَبِي طَالِبٍ، فَقَالَ لِرَسُولِ اللهِ صلى الله عليه وسلم: {إِنَّكَ لا تَهْدِي مَنْ أَحْبَبْتَ وَلَكِنَّ اللهَ يَهْدِي مَنْ يَشَاءُ} [القصص: 56].
Tafsiri
Kutoka kwa Saidi Bin Musayyab, kutoka kwa baba yake amesema: Yalipomfika mauti Abuu Twalib, Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- alimjia akamkuta yuko pamoja na Abuu Jahali na Abdallah Bin Umaiyya bin Mughiira, akasema: "Ewe baba yangu mdogo, sema: Laa ilaaha illa llaahu (Hapana Mola apasaye kuabudiwa kwa haki isipokuwa Mwenyezi Mungu) neno ambalo nitakutetea kwalo mbele ya Mwenyezi Mungu", Abuu Jahali akasema: Hivi unataka kuichukia mila ya Abdul Muttwalib (Yaani baba yake) Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- akaendelea kumrejelea neno hilo, nao pia wakirudia kumwambia maneno yao, mpaka Abuu Twalib akasema kwa neno lake la mwisho alilowasemesha: Niko katika mila ya Abdul Muttwalib, na akakataa kusema: Laa ilaaha illa llaah, mpokezi anasema: Akasema Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake-: "Wallahi (Namuapia Allah) nitakuombea msamaha kwa muda wote madam sijakatazwa, Allah akateremsha: "Haifai wala haitakiwi kwa Nabii na wale walioamini kuwaombea msamaha washirikina" [Attauba: 113], Na akateremsha kuhusu Abuu Twalib, akasema kumwambia Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake-: "Hakika wewe humuongoi umpendaye, lakini Allah anamuongoa amtakaye" [Al-Qasas:56]
Ufafanuzi
Aliingia Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- kwa Ami yake Abuu Twalib akiwa katika hali ya kukaribia kufa, akasema kumwambia: Ewe Ami yangu sema "Laa ilaaha illa llaah", neno ambalo nitakutolea ushahidi kwalo mbele ya Allah, Abuu Jahali na Abdallah Bin Abiiy Umaiyya wakasema: "Wewe Abuu Twalib!, unaacha mila ya baba yako Abdul Muttwalib?! ambayo ni kuabudu masanamu, wakaendelea kumwambia hivyo mpaka akasema neno lake la mwisho alilowaambia kuwa: Niko katika mila ya Abdul Muttwalib, mila ya ushirikina na kuabudu masanamu, Akasema Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake-: Nitakuombea msamaha madam sijakatazwa na Mola wangu kuhusu hilo, ikateremka kauli ya Mwenyezi Mungu Mtukufu: "Haipasi kwa Nabii na wale walioamini kuwatakia msamaha washirikina, hata kama watakuwa ni jamaa zao, baada ya kwisha bainika kuwa hao ni watu wa Motoni" [Attauba: 113], Na ikateremka kumuhusu Abuu Twalib kauli ya Mwenyezi Mungu Mtukufu: "Hakika wewe, humuongoi, unayependa aongoke. Lakini Mwenyezi Mungu, Anamuongoa Anayemtaka. Na Yeye Ndiye Anayemjua zaidi anayefaa kuongoka". Kwani hakika wewe humuongoi umpendaye kumuongoa, bali jukumu lako ni kufikisha, na Allah anamuongoa amtakaye.
Mafunzo
- Uharamu wa kuwaombea msamaha washirikina vyovyote vile utakavyokuwa ukaribu wao na matendo yao na wema wao.
- Kuwaiga mababa na wazee katika batili ni katika vitendo vya watu wa zama za ujinga.
- Ukamilifu wa huruma yake Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- na pupa yake katika kuwalingania watu na kuwaongoza.
- Hili ni jibu kwa watu wanaodai kuwa Abuu Twalib alisilimu.
- Matendo huzingatiwa mwisho.
- Kubatilika kujifungamanisha na kushikamana na Mtume au mwingine asiyekuwa yeye kwa lengo la kupata kheri na kuzuia madhara.
- Atakayesema "Laa ilaaha illa llaah" kwa kuwa na elimu na yakini na kuitakidi kwa dhati juu yake basi atakuwa kaingia ndani ya Uislamu.
- Madhara ya watu waovu na marafiki wabaya kwa mwanadam.
- Maana ya "Laa ilaaha illa llaah": Ni kuacha ibada za masanamu na wachamungu na watu wema na kumpwekeshea ibada Mwenyezi Mungu peke yake, nakwamba washirikina wanaju maana yake.
- Inafaa kumtembelea mgonjwa mshirikina ikiwa anatarajiwa huenda akasilimu.
- Uongofu wa kumuafikisha mja afungue moyo wake uko mkononi mwa Allah peke yake hana mshirika, bali jukumu la Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- ni kuongoza kwa kuelekeza, muongozo, na kufikisha ujumbe.
Ufafanuzi: العربية
دَخَلَ النبيُّ صلى الله عليه وسلم على عَمِّه أبي طالب وهو يَحْتَضِرُ، فقال له: يا عم، قل "لا إله إلا الله"، كلمة أشهد لك بها عند الله، فقال أبو جهل وعبد الله بن أبي أمية: يا أبا طالب، تترك ملة أبيك عبد المطلب؟! وهي عبادة الأصنام، فلم يزالا يُكلِّمانه حتى قال آخر شيء كلَّمهم به: على مِلَّةِ عبد المطلب، ملة الشرك وعبادة الأصنام، فقال النبي صلى الله عليه وسلم: سأدعوا لك بالمغفرة ما لم ينهني ربي عن ذلك، فنزل قول الله تعالى: {مَا كَانَ لِلنَّبِيِّ وَالَّذِينَ آمَنُوا أَنْ يَسْتَغْفِرُوا لِلْمُشْرِكِينَ وَلَوْ كَانُوا أُولِي قُرْبَى مِنْ بَعْدِ مَا تَبَيَّنَ لَهُمْ أَنَّهُمْ أَصْحَابُ الْجَحِيمِ} [التوبة: 113]، ونزل في أبي طالب قول الله تعالى: {إِنَّكَ لا تَهْدِي مَنْ أَحْبَبْتَ وَلَكِنَّ اللَّهَ يَهْدِي مَنْ يَشَاءُ وَهُوَ أَعْلَمُ بِالْمُهْتَدِينَ} [القصص: 56]، فإنك لا تهدي مَن أحببتَ هدايتَه، إنما عليك البلاغ، والله يهدي من يشاء.
- تحريم الاستغفار للمشركين مهما كانت قرابتهم وعملهم وإحسانهم.
- تقليدُ الآباء والأكابر بالباطل مِن فِعْل أهل الجاهلية.
- كمالُ شفقة النبيِّ صلى الله عليه وسلم وحرصِه على دعوة الناس وهدايتهم.
- الرد على مَن زعم إسلام أبي طالب.
- الأعمال بالخواتيم.
- بطلان التعلُّق بالنبيِّ عليه الصلاة والسلام وغيره لِجَلْب النفع أو دفع الضرر.
- من قال "لا إله إلا الله" عن علمٍ ويقين واعتقادٍ دخل في الإسلام.
- مضرة أصحاب السوء وقرناء الشر على الإنسان.
- معنى "لا إله إلا الله": تركُ عبادة الأصنام والأولياء والصالحين وإفراد الله بالعبادة، وأنّ المشركين يعرفون معناها.
- جواز عيادة المريض المشرك إذا رُجي إسلامُه.
- هداية التوفيق بيد الله وحده لا شريك له، وإنما على الرسول صلى الله عليه وسلم هداية الدلالة والإرشاد والبلاغ.