Hadithi

Likiwekwa Jeneza, na wanaume wakalibeba katika shingo zao, likiwa ni la mtu mwema basi husema: Niwahisheni,

Chanzo: HadeethEnc.com, Kiswahili v1.18.0

SahihiImepokelewa na Al-Bukhaariy

Matini ya Kiarabu

عَن أَبِي سَعِيدٍ الخُدْرِيَّ رَضِيَ اللَّهُ عَنْهُ أَنَّ رَسُولَ اللَّهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ قَالَ: «إِذَا وُضِعَتِ الجِنَازَةُ وَاحْتَمَلَهَا الرِّجَالُ عَلَى أَعْنَاقِهِمْ فَإِنْ كَانَتْ صَالِحَةً قَالَتْ: قَدِّمُونِي، وَإِنْ كَانَتْ غَيْرَ صَالِحَةٍ قَالَتْ: يَا وَيْلَهَا أَيْنَ يَذْهَبُونَ بِهَا؟ يَسْمَعُ صَوْتَهَا كُلُّ شَيْءٍ إِلَّا الإِنْسَانَ، وَلَوْ سَمِعَهُ صَعِقَ».

Tafsiri

Kutoka kwa Abuu Saidi Al-Khudry -radhi za Allah ziwe juu yake- yakwamba Mtume rehema na amani ziwe juu yake: "Likiwekwa Jeneza, na wanaume wakalibeba katika shingo zao, likiwa ni la mtu mwema basi husema: Niwahisheni, na likiwa si la mtu mwema basi husema: Ubaya ulioje, mnalipeleka wapi? Huisikia sauti yake kila kitu isipokuwa mwanadamu, na lau angelisikia basi angezimia".

Ufafanuzi

Ameeleza Mtume rehema na amani ziwe juu yake kwamba Jeneza likiwekwa kitandani, na wanaume wakalibeba katika shingo zao, likiwa ni la mtu mwema basi husema: Niwahisheni, kwa yale linayoyaona mbele yake katika neema, na likiwa si la mtu mwema, hupiga yowe kwa sauti mbaya ya kukera, na kusema: Nasikitika kwa maangamivu yake, mnalipeleka wapi?! kwa yale linayoyaona mbele yake miongoni mwa adhabu, inasikika sauti yake kwa kila kitu isipokuwa mwanadamu, na lau angeliisikia basi angezimia kutokana na ukubwa wa kile alichosikia.

Mafunzo

  • Maiti mwema huanza kuona habari njema kabla ya kuzikwa kwake, na kafiri hufadhaika, na kuona mambo kinyume na hivyo.
  • Baadhi ya suti husikiwa na viumbe vingine tofauti na mwanadamu, na wala mwanadamu hawezi kuzisikia.
  • Sunna ni kulibeba Jeneza juu ya mabeba ya wanaume na si wanawake; kwa katazo la Mtume rehema na amani ziwe juu yake kuwakataza wanawake kusindikiza Jeneza.
Ufafanuzi: العربية

أخبر النبيُّ صلى الله عليه وسلم أنه إذا وضعت الجنازة على السرير، واحتملها الرجال على أعناقهم، فإن كانت صالحة قالت: قدموني لما تراه أمامها من النعيم، وإن كانت غير صالحة صاحت بصوت منكر: يا هلاكها أين يذهبون بها؟! لما تراه أمامها من العذاب، يسمع صوتها كل شيء إلا الإنسان، ولو سمعه لغشي عليه من شدة ما يسمعه.

  • الميت الصالح يرى المُبَشِّرات قبل دفنه، ويجزع الكافر، ويرى عكس ذلك.
  • بعض الأصوات يسمعها غير الإنسان، ولا يستطيع الإنسان سماعها.
  • السنة حمل الجنازة على أعناق الرجال دون النساء؛ لنهي النبي صلى الله عليه وسلم النساء عن اتباعها.

Mada

Ripoti kosa

Zaidi