Hadithi

Atakayependa Mwenyezi Mungu amuokoe na Matatizo ya siku ya Kiyama, basi amtatulie shida mwenye hali ngumu au ampunguzie

Chanzo: HadeethEnc.com, Kiswahili v1.18.0

SahihiImepokelewa Imamu Muslim

Matini ya Kiarabu

عَنْ أَبَي قَتَادَةَ رضي الله عنه أنَّهُ طَلَبَ غَرِيمًا لَهُ، فَتَوَارَى عَنْهُ ثُمَّ وَجَدَهُ، فَقَالَ: إِنِّي مُعْسِرٌ، فَقَالَ: آللَّهِ؟ قَالَ: آللَّهِ؟ قَالَ: فَإِنِّي سَمِعْتُ رَسُولَ اللهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ يَقُولُ: «مَنْ سَرَّهُ أَنْ يُنْجِيَهُ اللهُ مِنْ كُرَبِ يَوْمِ الْقِيَامَةِ فَلْيُنَفِّسْ عَنْ مُعْسِرٍ أَوْ يَضَعْ عَنْهُ».

Tafsiri

Kutoka kwa Abuu Qatada radhi za Allah ziwe juu yake yakwamba yeye siku moja alimtafuta mdai wake, akajificha, kisha akampata, akasema: Hakika mimi nina hali ngumu, akasema: Je, unamuapa Mwenyezi Mungu juu ya hilo? Akasema: Ndio, ninamuapa Mwenyezi Mungu juu ya hilo. Akasema: Kwani mimi nilimsikia Mtume rehema na amani ziwe juu yake akisema: "Atakayependa Mwenyezi Mungu amuokoe na Matatizo ya siku ya Kiyama, basi amtatulie shida mwenye hali ngumu au ampunguzie".

Ufafanuzi

Abuu Qatada Al-Answari radhi za Allah ziwe juu yake alikuwa akimtafuta mdaiwa wake aliyekuwa akijificha, akampata, mdaiwa akasema: Mimi nina hali ngumu, na sina mali ya kulipa deni lako. Abuu Qatada radhi za Allah ziwe juu yake akamtaka aape kwa jina la Mwenyezi Mungu kuwa hana mali? Akaapa kwa jina la Mwenyezi Mungu kuwa ni mkweli katika hayo anayoyasema. Akasema Abuu Qatada radhi za Allah ziwe juu yake kuwa yeye alimsikia Mtume rehema na amani ziwe juu yake akisema: Atakayependezwa na akafurahishwa kuwa Mwenyezi Mungu amuokoe na misukosuko ya siku ya Kiyama na matatizo yake na vitisho vyake, basi amtatulie shida mwenye hali ngumu, kwa kumpa muda mrefu na acheleweshe kumdai deni lake, au apunguze sehemu ya deni au amsamehe deni lote.

Mafunzo

  • Inapendeza kumpa muda mwenye hali ngumu mpaka atakapopata wepesi, au kumpunguzia deni lote au baadhi yake.
  • Atakayemtatulia muumini sehemu katika matatizo ya dunia basi naye Mwenyezi Mungu atamtatulia sehemu katika matatizo ya siku ya Kiyama, na malipo huenda sawa matendo.
  • Kanuni: Faradhi ni bora kuliko sunna, lakini katika baadhi ya nyakati sunna huwa bora kuliko faradhi, na kumuondolea deni mwenye hali ngumu ni sunna, na kumvumilia na kuacha kumdai ni faradhi, na hapa sunna ni bora kuliko faradhi.
  • Hadithi hii ni kwa yule mwenye hali ngumu ya kimaisha, huyu ndiye anayepewa udhuru, ama kumzungusha mtu anayekudai hali yakuwa una mali, imekuja kutoka kwa Mtume rehema na amani ziwe juu yake alisema: "Ucheleweshaji wa kulipa deni kwa mtu mwenye uwezo ni dhulma".
Ufafanuzi: العربية

كان أبو قتادة الأنصاري رضي الله عنه يبحث عن مَدِيْنٍ له يَخْتَبِئ عنه، فوجده، فقال الغَريم: إني مُعسر، وليس عندي مال لأقضي دينك. فاستحلفه أبو قتادة رضي الله عنه بالله أنه لا مال عنده؟ فحلف بالله أنه صادق فيما يقول. فقال أبو قتادة رضي الله عنه إنه سمع النبي صلى الله عليه وسلم يقول: مَن سرّه وأفرحه أن ينجيَه الله من كُرب يوم القيامة وشدائدها وأهوالها، فلينفِّس عن معسر، بأن يَمُدَّ ويؤخّر المطالبة بالدَّيْن، أو يُسقط بعض الدين أو كله.

  • استحباب إنظار المُعْسر إلى مَيْسرة، أو وضع الدَّين عنه، كله أو بعضه.
  • من نَفَّس عن مؤمن من كُرب الدنيا نَفَّس الله عليه من كُرَب يوم القيامة، والجزاء من جِنس العمل.
  • القاعدة: أن الفرائض أفضل من النوافل، لكن في بعض الأحيان تكون النافلة أفضل من الفريضة، وإسقاط الدين عن المعسر نافلة، والصبر عليه والانتظار وعدم المطالبة هذا فريضة، والنافلة أفضل من الفريضة هنا.
  • الحديث في حق من كان معسرًا، فهذا معذور، أما المُماطِل الذي عنده مال، فقد جاء عن النبي صلى الله عليه وسلم أنه قال: "مَطْلُ الغني ظُلْم".

Mada

Ripoti kosa

Zaidi