Hadithi

Nimeamrishwa nipambane na watu mpaka washuhudie kuwa hapana Mola apasaye kuabudiwa kwa haki isipokuwa Mwenyezi Mungu nakuwa Muhammadi ni Mjumbe wa Mwenyezi Mungu, na wasimamishe swala, na watoe zaka

Chanzo: HadeethEnc.com, Kiswahili v1.18.0

SahihiWamekubaliana Bukhari na Muslim juu ya usahihi wake

Matini ya Kiarabu

عَنِ ابْنِ عُمَرَ رضي الله عنهما أَنَّ رَسُولَ اللَّهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ قَالَ: «أُمِرْتُ أَنْ أُقَاتِلَ النَّاسَ حَتَّى يَشْهَدُوا أَنْ لاَ إِلَهَ إِلَّا اللَّهُ، وَأَنَّ مُحَمَّدًا رَسُولُ اللَّهِ، وَيُقِيمُوا الصَّلاَةَ، وَيُؤْتُوا الزَّكَاةَ، فَإِذَا فَعَلُوا ذَلِكَ عَصَمُوا مِنِّي دِمَاءَهُمْ وَأَمْوَالَهُمْ إِلَّا بِحَقِّ الإِسْلاَمِ، وَحِسَابُهُمْ عَلَى اللَّهِ».

Tafsiri

Na imepokewa kutoka kwa bin Omari -Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake yeye na baba yake -kwamba Mtume wa Mwenyezi Mungu -Rehema na Amani ziwe juu yake - amesema: "Nimeamrishwa nipambane na watu mpaka washuhudie kuwa hapana Mola apasaye kuabudiwa kwa haki isipokuwa Mwenyezi Mungu nakuwa Muhammadi ni Mjumbe wa Mwenyezi Mungu, na wasimamishe swala, na watoe zaka, pindi watakapofanya hivyo watakuwa wamezikinga kutokana nami damu zao na mali zao isipokuwa kwa haki ya uislamu na hesabu yao itakuwa juu ya Mwenyezi Mungu Mtukufu".

Ufafanuzi

Anaeleza Mtume rehema na amani ziwe juu yake kuwa Mwenyezi Mungu alimuamrisha kupigana na washirikina mpaka washuhudie kuwa hapana muabudiwa kwa haki isipokuwa Mwenyezi Mungu peke yake asiye na mshirika, na wamshuhudilie Muhammadi rehema na amani ziwe juu yake utume, na kuyafanyia kazi makusudio ya shahada hii, ikiwemo kuhifadhi swala tano usiku na mchana, na wawape zaka za faradhi wastahiki wake. Wakifanya mambo haya basi Uislamu utakinga damu zao na mali zao, haitokuwa halali kuwaua isipokuwa watakapofanya uhalifu au kosa la jinai watakalostahiki kwalo kuuawa kwa mujibu wa hukumu za Uislamu, kisha siku ya Kiyama Mwenyezi Mungu atasimamia hesabu yao kwani yeye ndiye ajuaye siri zao.

Mafunzo

  • Hukumu zote huenda kulingana na kile kichodhihiri, na Allah ndiye msimamizi wa siri.
  • Umuhimu wa kufikisha ujumbe wa tauhidi nakuwa ndio ujumbe wa kwanza katika ufikishaji.
  • Hadithi hii haimaanishi kuwalazimisha washirikina kuingia katika Uislamu, bali wamepewa uhuru wa kuchagua kati ya kuingia katika Uislamu au kutoa Jizia (Kodi); ikiwa watakataa na wakataka kuzuia ujumbe wa Uislamu, kukawa hakuna namna nyingine zaidi ya kuwapiga vita kwa mujibu wa hukumu za kiislamu.
Ufafanuzi: العربية

يُخْبِرُ النبيُّ صلى الله عليه وسلم أنَّ اللهَ أمرَه بمقاتلة المشركين حتى يشهدوا بأن لا معبود بحق إلا الله وحده لا شريك له، ويشهدوا لمحمد صلى الله عليه وسلم بالرسالة، والعمل بمقتضى هذه الشهادة من المحافظة على الصلوات الخمس في اليوم والليلة، ويعطوا الزكاة المفروضة لمستحقيها. فإذا فعلوا هذه الأمورَ فإنَّ الإسلام يَعْصِمُ دماءَهم وأموالَهم، فلا يَحِلُّ قتلُهم إلا إذا ارتكبوا جريمة أو جناية يستحقون عليها القتل بموجب أحكام الإسلام، ثم يوم القيامة يتولى الله تعالى حسابَهم حيث يعلم سرائرَهم.

  • الأحكام إنما تَجْرِي على الظواهر، والله يتولَّى السرائر.
  • أهمية الدعوة إلى التوحيد وأنه أول ما يُبدأ به في الدعوة.
  • لا يعني هذا الحديث إكراه المشركين على الدخول في الإسلام، بل هم مُخَيَّرون بين الدخول في الإسلام أو دفع الجزية؛ فإنْ أبوا إلا مَنع الدعوة إلى الإسلام، فليس إلا المقاتلة بموجب أحكام الإسلام.

Mada

Ripoti kosa

Zaidi