Hadithi

Uislamu ni ushuhudie kuwa hapana Mola apasaye kuabudiwa kwa haki isipokuwa Mwenyezi Mungu, nakuwa Muhammadi ni Mjumbe wa Mwenyezi Mungu, na usimamishe sala, na utoe zake, na ufunge Ramadhani, na uhiji katika nyumba tukufu ikiwa utapata uwezo wa kuifikia

Chanzo: HadeethEnc.com, Kiswahili v1.18.0

SahihiImepokelewa Imamu Muslim

Matini ya Kiarabu

عن عمر بن الخطاب رضي الله عنه قال: بَيْنَمَا نَحْنُ عِنْدَ رَسُولِ اللهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ ذَاتَ يَوْمٍ إِذْ طَلَعَ عَلَيْنَا رَجُلٌ شَدِيدُ بَيَاضِ الثِّيَابِ، شَدِيدُ سَوَادِ الشَّعَرِ، لَا يُرَى عَلَيْهِ أَثَرُ السَّفَرِ، وَلَا يَعْرِفُهُ مِنَّا أَحَدٌ، حَتَّى جَلَسَ إِلَى النَّبِيِّ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ، فَأَسْنَدَ رُكْبَتَيْهِ إِلَى رُكْبَتَيْهِ، وَوَضَعَ كَفَّيْهِ عَلَى فَخِذَيْهِ، وَقَالَ: يَا مُحَمَّدُ، أَخْبِرْنِي عَنِ الْإِسْلَامِ، فَقَالَ رَسُولُ اللهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ: «الْإِسْلَامُ أَنْ تَشْهَدَ أَنْ لَا إِلَهَ إِلَّا اللهُ، وَأَنَّ مُحَمَّدًا رَسُولُ اللهِ، وَتُقِيمَ الصَّلَاةَ، وَتُؤْتِيَ الزَّكَاةَ، وَتَصُومَ رَمَضَانَ، وَتَحُجَّ الْبَيْتَ إِنِ اسْتَطَعْتَ إِلَيْهِ سَبِيلًا» قَالَ: صَدَقْتَ، قَالَ: فَعَجِبْنَا لَهُ، يَسْأَلُهُ وَيُصَدِّقُهُ، قَالَ: فَأَخْبِرْنِي عَنِ الْإِيمَانِ، قَالَ: «أَنْ تُؤْمِنَ بِاللهِ، وَمَلَائِكَتِهِ، وَكُتُبِهِ، وَرُسُلِهِ، وَالْيَوْمِ الْآخِرِ، وَتُؤْمِنَ بِالْقَدَرِ خَيْرِهِ وَشَرِّهِ» قَالَ: صَدَقْتَ، قَالَ: فَأَخْبِرْنِي عَنِ الْإِحْسَانِ، قَالَ: «أَنْ تَعْبُدَ اللهَ كَأَنَّكَ تَرَاهُ، فَإِنْ لَمْ تَكُنْ تَرَاهُ فَإِنَّهُ يَرَاكَ» قَالَ: فَأَخْبِرْنِي عَنِ السَّاعَةِ، قَالَ: «مَا الْمَسْؤُولُ عَنْهَا بِأَعْلَمَ مِنَ السَّائِلِ» قَالَ: فَأَخْبِرْنِي عَنْ أَمَارَتِهَا، قَالَ: «أَنْ تَلِدَ الْأَمَةُ رَبَّتَهَا، وَأَنْ تَرَى الْحُفَاةَ الْعُرَاةَ الْعَالَةَ رِعَاءَ الشَّاءِ يَتَطَاوَلُونَ فِي الْبُنْيَانِ» قَالَ: ثُمَّ انْطَلَقَ، فَلَبِثْتُ مَلِيًّا ثُمَّ قَالَ لِي: «يَا عُمَرُ، أَتَدْرِي مَنِ السَّائِلُ؟» قُلْتُ: اللهُ وَرَسُولُهُ أَعْلَمُ، قَالَ: «فَإِنَّهُ جِبْرِيلُ، أَتَاكُمْ يُعَلِّمُكُمْ دِينَكُمْ».

Tafsiri

Imepokewa Kutoka kwa Omar bin Khattwab -Radhi za Allah ziwe juu yake- amesema: Siku moja tukiwa tumekaa kwa Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- ghafla akatokea mtu mwenye nguo nyeupe mno, mwenye nywele nyeusi mno, haonekani kuwa na athari yoyote ya safari, na hakuna yeyote amjuaye miongoni mwetu, akaja mpaka akakaa kwa Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake-, akakunja magoti yake kwa kuyaunganisha na magoti yake mtume (Mithili ya tahiyatu) Na akaweka viganja vyake juu ya mapaja yake, na akasema: Ewe Muhammadi, nieleze kuhusu Uislamu, akasema Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake-: "Uislamu ni ushuhudie kuwa hapana Mola apasaye kuabudiwa kwa haki isipokuwa Mwenyezi Mungu, nakuwa Muhammadi ni Mjumbe wa Mwenyezi Mungu, na usimamishe sala, na utoe zake, na ufunge Ramadhani, na uhiji katika nyumba tukufu ikiwa utapata uwezo wa kuifikia" Akasema: Sadakta! (Umesema kweli), Anasema: Tukamshangaa: Anamuuliza na anamsadikisha! Akasema: Nieleze kuhusu imani. Akasema: "Nikuwa, umuamini Mwenyezi Mungu, na Malaika wake, na vitabu vyake, na Mitume wake, na siku ya mwisho, na uamini Kadari kheri yake na shari yake" Akasema: Sadakta! (Umesema kweli), akasema: Nieleza kuhusu Ihisani, akasema: "Ni umuabudu Mwenyezi Mungu kana kwamba unamuona, na ikiwa wewe humuoni basi yeye anakuona" Akasema: Nieleze kuhusu Kiyama, akasema: "Muulizwaji si mjuzi sana kama muulizaji" Akasema: Hebu nieleze kuhusu alama zake, akasema: "Ni mjakazi kuzaa bosi wake, na ukiwaona watembea peku, watembea uchi, tena masikini wachunga mbuzi, wakishindana kujenga majengo marefu." (Omar) Akasema: Kisha akaondoka, nikakaa muda mrefu kidogo, kisha Mtume akasema kuniambia: "Ewe Omari, hivi unamjua ni nani muulizaji?" Nikasema: Allah na Mtume wake ndio wajuzi zaidi, akasema: "Huyo ni Jibrili alikuja kukufundisheni dini yenu."

Ufafanuzi

Anaeleza Omari bin Khattwab -Radhi za Allah ziwe juu yake- kuwa Jibrili -Amani iwe juu yake- alijitokeza kwa Masahaba -Radhi za Allah ziwe juu yao- kwa sura ya mtu asiyejulikana, na miongoni mwa sifa zake nikuwa, nguo zake ni nyeupe mno, na nywele zake ni nyeusi mno, haonekani kuwa na athari za safari ikiwemo kuonyesha uchovu, vumbi, na nywele kutimka, na nguo kuchafuka, na hakuna yeyote amjuaye katika wote waliopo, nao wakiwa wamekaa kwa Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake-, akakaa mbele ya Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- mkao wa mwanafunzi, akamuuliza kuhusu Uislamu, akamjibu kwa nguzo hizi ambazo zimeambatana na kukiri shahada mbili, na kudumu na sala tano, na kutimiza zaka kwa wastahiki wake, na kufunga mwezi wa Ramadhani, na kutekeleza faradhi ya Hija kwa mwenye uwezo. Muulizaji akasema: Sadakta!, Masahaba wakashangaa kwa swali lake la kuonyesha kuwa hajui kitu kwa muonekano wake, kisha anamsadikisha!. Kisha akamuuliza kuhusu imani, akamjibu kwa nguzo hizi sita zilizokusanya kuamini uwepo wa Mwenyezi Mungu Mtukufu na sifa zake, na kumpwekesha kwa vitendo vyake kama kuumba, na kumpwekesha kwa ibada, nakuwa Malaika aliowaumba Allah kwa nuru ni waja waliotukuzwa hawamuasi Mwenyezi Mungu Mtukufu, na amri yake ndio wanayoifanyia kazi, na kuamini vitabu vilivyoteremshwa kwa Mitume kutoka kwa Mwenyezi Mungu Mtukufu, kama Qur'ani na Taurati na Injili na vinginevyo, na kuwaamini Mitume wenye kumfikishia Mwenyezi Mungu dini yake, miongoni mwao ni Nuhu na Ibrahim, na Mussa, na Issa, na wa mwisho wao ni Muhammadi -Rehema na amani ziwe juu yao wote- na wengineo katika Manabii na Mitume, na kuamini siku ya mwisho, na yanaingia hapa maisha baada ya kifo ikiwemo kaburi na maisha ya barzakh (Akhera), na kuamini kuwa Mwenyezi Mungu amekadiria mambo kulingana na ujuzi wake uliotangulia na hekima zake zikapelekea hivyo, na kuyaandika kwake, na matashi yake kwa mambo hayo, na kutokea kwake kwa namna aliyoikadiria Mwenyezi Mungu, na kuviumba kwake. Kisha akamuuliza kuhusu Ihisani, akamueleza kuwa Ihisani ni amuabudu Mwenyezi Mungu kana kwamba anamuona, ikiwa hatoweza kufikia daraja hili basi amuabudu Allah kana kwamba Allah anamshuhudia, daraja bora zaidi kushuhudiwa, na ndio ya juu zaidi, na ya pili ni daraja ya kuchunga (Kuleta hisia kua unamuona mbele yako). Kisha akamuuliza Kiyama ni lini? Akabainisha Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- kuwa elimu ya Kiyama ni katika elimu alizobaki nazo Mwenyezi Mungu ujuzi wake, hawezi kuijua yeyote katika viumbe, si muulizaji wala muulizwaji. Kisha akamuuliza kuhusu alama za Kiyama? Akabainisha kuwa miongoni mwa alama zake ni kukithiri kwa wajakazi (Masuria) na watoto wao, au ni wingi wa watoto kutowatii mama zao, kiasi cha kuishi nao kama watumwa wao, nakuwa wachunga mbuzi na masikini watakunjuliwa dunia katika zama za mwisho, na watafaharishana katika kuremba majengo na kuyarefusha. Kisha akaeleza Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- kuwa muulizaji ni Jibril alikuja kuwafundisha Masahaba dini tukufu.

Mafunzo

  • Uzuri wa tabia za Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake-, kwani alikuwa akikaa na wanafunzi wake, nao wakikaa kwake.
  • Sheria ya kuwa mpole kwa muulizaji na kumsogeza karibu, ili aweze kuuliza bila wasi wasi wala uoga.
  • Kuwa na adabu na mwalimu kama alivyofanya Jibril -Amani iwe juu yake-, kiasi kwamba alikaa mbele ya Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- mkao wa adabu ili ajifunze toka kwake.
  • Nguzo za Uislamu ni tano, na misingi ya Imani ni sita.
  • Linapokutana neno Uislamu na Imani Uislamu hutafirisiwa kwa mambo ya dhahiri (yenye kuonekana) na Imani kwa mambo yasiyoonekana.
  • Kumebainishwa kuwa dini ina daraja tofauti, daraja la kwanza: Ni Uislamu, la pili: Imani, na la tatu: Ihisani, na ndio la juu zaidi kuliko yote.
  • Kimsingi muulizaji hua si mjuzi, na ujinga ndio msukumo wa kuuliza, ndio maana Masahaba walishangaa kuuliza kwake na kusadikisha kwake.
  • Kuanza na la muhimu zaidi kisha linalofuata; Kwa sababu kumeanzwa na shahada mbili katika tafsiri ya Uislamu, na kumeanzwa na kumuamini Mwenyezi Mungu katika tafsiri ya imani.
  • Inafaa mjuzi kuwauliza wajuzi mambo anayoyafahamu kwa lengo la kuwafundisha wengine.
  • Elimu ya Kiyama ni katika elimu alizobaki nazo Allah.
Ufafanuzi: العربية

يُخبِرُ عمر بن الخطاب رضي الله عنه أنّ جبريل عليه السلام خرج على الصحابة رضي الله عنهم بصورةِ رجلٍ لا يُعرف، ومن صفاته أنّ ثيابَه شديدة البياض، وشعرَه شديد السواد، لا يُرى عليه أَثَرُ السَّفَر من ظهور التعب، والغبار، وتفرُّق الشَّعَر، واتساخ الثياب، ولا يَعرفه أحدٌ من الحاضرين، وهم جلوس عند النبي صلى الله عليه وسلم، فَجَلسَ بين يدي النبي صلى الله عليه وسلم جِلْسَة المُتَعلِّم، فسأله عن الإسلام، فأجابه بهذه الأركان التي تتضمن الإقرار بالشهادتين، والمحافظة على الصلوات الخمس، وأداء الزكاة لمستحقيها، وصيام شهر رمضان، وأداء فريضة الحج على المستطيع. فقال السائل: صدقت، فاستغرب الصحابةُ من سؤالِه الدَّالِّ على عَدَمِ معرفتِه فيما يَظهر ثم تصديقِه. ثم سأله عن الإيمان، فأجابه بهذه الأركان الستة المتضمنة الإيمان بوجود الله تعالى وصفاته، وإفراده بأفعاله كالخلق، وإفراده بالعبادة، وأن الملائكة التي خلقها الله من نور عباد مُكْرَمون لا يعصون الله تعالى وبأمره يعملون، والإيمان بالكتب المنزلة على الرُّسُل من عند الله تعالى، كالقرآن والتوراة والإنجيل وغيرها، وبالرسل المبلِّغين عن الله دينَه، ومنهم نوح وإبراهيم وموسى وعيسى وآخرهم محمد صلى الله عليهم وسلم، وغيرهم من الأنبياء والرسل، والإيمان باليوم الآخر، ويدخل فيه ما بعد الموت من القبر والحياة البرزخية، وأن الإنسان يُبعث بعد الموت ويُحاسب، ويكون مصيره إما إلى الجنة أو النار، والإيمان بأنَّ الله قدَّرَ الأشياء حسبما سَبَق به علمُه واقتضته حكمتُه وكتابته لذلك، ومشيئته له، ووقوعها على حسب ما قدَّرها، وخلقَه لها. ثم سأله عن الإحسان، فأخبره أن الإحسان أن يَعبُدَ اللهَ كأنه يراه، فإن لم يَتَحقَّق له الوصولُ إلى هذه المنزلة فلْيَعبُدِ اللهَ تعالى كأنَّ اللهَ يُشاهدُه، فالأولى منزلة المشاهدة، وهي أعلى، والثانية منزلة المراقبة. ثم سأله متى الساعة؟ فبيَّن النبيُّ صلى الله عليه وسلم أنَّ عِلْمَ الساعة ممّا استأثر الله بعلمه، فلا يعلمه أحد من الخلق، لا المسؤول عنها ولا السائل. ثم سأله عن علامات الساعة؟ فبين أنَّ مِن علاماتِها كثرةَ السراري وأولادِها، أو كثرةَ عقوقِ الأولاد لأمهاتِهم يعاملونهن معاملة الإماء، وأن رعاةَ الغنم والفقراء تُبسط لهم الدنيا في آخر الزمان، فيتفاخرون في زخرفة المباني وتشييدِها. ثم أخبر النبيُّ صلى الله عليه وسلم أنَّ السائل هو جبريل جاء لتعليم الصحابة هذا الدين الحنيف.

  • حُسْن خُلُقِ النبي صلى الله عليه وسلم، وأنه يجلس مع أصحابه ويجلسون إليه.
  • مشروعية الرفق بالسائل وتقريبه، ليتمكن من السؤال غير مُنْقَبِضٍ ولا خائف.
  • الأدب مع المعلِّم كما فعل جبريل عليه السلام، حيث جلس أمام النبي صلى الله عليه وسلم جِلْسَة المتأدِّب ليأخذ منه.
  • أركان الإسلام خمسة، وأصولَ الإيمان ستة.
  • عند اجتماع الإسلام والإيمان يُفسَّر الإسلام بالأمور الظاهرة، والإيمان بالأمور الباطنة.
  • بيان أن الدين درجات متفاوتة، فالدرجة الأولى :الإسلام، والثانية :الإيمان، والثالثة: الإحسان، وهو أعلاها.
  • الأصل في السائل عدم العلم، والجهل هو الباعث على السؤال، لذلك عَجِب الصحابةُ من سؤالِه وتصديقِه.
  • البدء بالأهمِّ فالأهمِّ؛ لأنَّه بُدىء بالشهادَتين في تفسير الإسلام، وبُدىء بالإيمان بالله في تفسير الإيمان.
  • سؤال أهل العلم ما لا يجهله السائل، ليعلم غيره.
  • علم الساعة مِمَّا استأثر الله بعلمه.

Mada

Ripoti kosa

Zaidi