Hadithi

Hakuna kujidhuru wala kusababisha madhara, na atakayedhuru Allah naye atamdhuru, na atakayemtia mtu uzito Mwenyezi Mungu atamtia uzito naye

Chanzo: HadeethEnc.com, Kiswahili v1.18.0

Ni sahihi kwa ushahidi wake mbalimbaliImepokelewa na Addar- Alqutni

Matini ya Kiarabu

عن أبي سعيد الخدري رضي الله عنه أن رسول الله صلى الله عليه وسلم قال: «لَا ضَرَرَ وَلَا ضِرَارَ، مَنْ ضَارَّ ضَرَّهُ اللَّهُ، وَمَنْ شَاقَّ شَقَّ اللَّهُ عَلَيْهِ».

Tafsiri

Imepokewa Kutoka kwa Abuu Saidi Al-Khudri -Radhi za Allah ziwe juu yake- yakwamba Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- amesema: "Hakuna kujidhuru wala kusababisha madhara, na atakayedhuru Allah naye atamdhuru, na atakayemtia mtu uzito Mwenyezi Mungu atamtia uzito naye".

Ufafanuzi

Amebainisha Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- kuwa ni lazima kuzuia madhara kwa aina zake zote na sababu zake zote kwako na kwa wengine,ni haramu kwa yeyote kujiudhi mwenyewe na mwingine kwa kiwango sawa. Na ni haramu kwake kukabiliana na madhara kwa madhara; kwa sababu madhara hayaondoshwi kwa madhara, isipokuwa kama itakua katika njia ya kulipiza kisasi pasina kuvuka mipaka. Kisha akabainisha Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- adhabu pale yanapotokea madhara kwa mtu mwenye kuwadhuru watu, na pale zinapotokea tabu kwa mtu mwenye kuwatia watu tabu.

Mafunzo

  • Katazo la kulipiza kwa zaidi ya vile ulivyofanyiwa.
  • Mwenyezi Mungu hakuwaamrisha waja wake lolote lenye kuwadhuru.
  • Katazo la kujidhuru au kudhuru ima kwa kauli au kitendo au kuacha.
  • Malipo hulingana na kitendo, atakayedhuru Mwenyezi Mungu naye atamdhuru, na atakaye tia ugumu Mwenyezi Mungu naye atamtia ugumu.
  • Katika kanuni za sheria: Ni "Madhara huondoshwa", Hivyo, sheria haikubaliani na madhara, na inakataza kujidhuru.
Ufafanuzi: العربية

بَيَّنَ النبيُّ صلى الله عليه وسلم أنه يَجِبُ دفعُ الضررِ بمختلف أنواعه ومظاهره عن النفس وعن الآخرين، فلا يَحِلُّ لأحدٍ أن يُؤذيَ نفسَه أو غيرَه على حد سواء. ولا يَحلُّ له أن يقابِلَ الضررَ بالضرر؛ لأن الضررَ لا يُزال بالضرر إلا على سبيل القصاص دون تعدٍّ. ثم بيَّنَ النبيُّ صلى الله عليه وسلم الوعيدَ بحصول الضرر لمن يَضرُّ بالناس، وبحصول المشقة لمن يَشقُّ على الناس.

  • النهي عن المجازاة بأكثر من المِثْل.
  • لم يأمر اللهُ عبادَه بشيء يضرُّهم.
  • تحريم الضرر والضرار بالقول أو بالفعل أو بالترك.
  • الجزاء من جنس العمل، فمن ضارَّ ضارَّه الله، ومن شاقَّ شاقَّه الله.
  • من قواعد الشريعة: أن "الضرر يُزال"، فالشريعة لا تُقِرُّ الضرر، وتنكر الإضرار.

Mada

Ripoti kosa

Zaidi