Hadithi

Atakayejitoa katika utiifu, na akasambaratisha umoja akafa, atakuwa amekufa kifo cha zama za ujinga

Chanzo: HadeethEnc.com, Kiswahili v1.18.0

SahihiImepokelewa Imamu Muslim

Matini ya Kiarabu

عن أبي هريرة رضي الله عنه عن النبي صلى الله عليه وسلم أنه قال: «مَنْ ‌خَرَجَ ‌مِنَ ‌الطَّاعَةِ، وَفَارَقَ الْجَمَاعَةَ فَمَاتَ، مَاتَ مِيتَةً جَاهِلِيَّةً، وَمَنْ قَاتَلَ تَحْتَ رَايَةٍ عِمِّيَّةٍ، يَغْضَبُ لِعَصَبَةٍ، أَوْ يَدْعُو إِلَى عَصَبَةٍ، أَوْ يَنْصُرُ عَصَبَةً، فَقُتِلَ، فَقِتْلَةٌ جَاهِلِيَّةٌ، وَمَنْ خَرَجَ عَلَى أُمَّتِي، يَضْرِبُ بَرَّهَا وَفَاجِرَهَا، وَلَا يَتَحَاشَى مِنْ مُؤْمِنِهَا، وَلَا يَفِي لِذِي عَهْدٍ عَهْدَهُ، فَلَيْسَ مِنِّي وَلَسْتُ مِنْهُ».

Tafsiri

Imepokewa kutoka kwa Abuu Huraira -Radhi za Allah ziwe juu yake- kutoka kwa Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- amesema: "Atakayejitoa katika utiifu, na akasambaratisha umoja akafa, atakuwa amekufa kifo cha zama za ujinga, na atakayepigana chini ya bendera kibubusa anachukia kwa sababu ya ndugu zake, au akahamasisha katika (kupendelea kwa sababu ya) udugu, au ana nusuru udugu, akauwawa, basi hicho ni kifo cha zama za ujinga, na atakayejitoa katika umma wangu, akimpiga mwema wake na muovu wake, na wala hajali muumini wake, na wala hamtimizii mwenye ahadi ahadi yake, basi huyo si miongoni mwangu na mimi si miongoni mwake".

Ufafanuzi

Amebainisha Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- kuwa atakayetoka katika kuwatii viongozi, na akaeneza fitina na kuusambaratisha umoja wa Uislamu uliokubaliana juu ya kumtii kiongozi, akafa katika hali hiyo ya faraka na kutomtii kiongozi, atakuwa kafa kifo cha watu wa zama za ujinga, ambao walikuwa hawamtii kiongozi yeyote wala hawajiungi katika kundi moja, bali walikuwa makundi makundi na wabaguzi, wakipigana wao kwa wao. Na akaeleza Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- kuwa atakayepigana chini ya bendera ambayo haiko wazi upande wa haki au batili, anachukia kwa sababu ya ubaguzi wa watu wake au kabila lake, na si kwa kuitetea dini na haki, akapigana kwa ubaguzi pasina kuwa na ujuzi na elimu, akiuawa katika hali hiyo, atakuwa ni sawa na aliye uawa katika zama za ujinga. Nakuwa atakayetoka katika Umma wake -Rehema na amani ziwe juu yake- akimpiga mwema wake, na muovu wake, na wala hajali anayoyafanya na wala haogopi adhabu zake kwa kumuuwa muumini, na wala hawatendei uadilifu makafiri waliochukua ahadi au viongozi, bali anatengua ahadi kwao, jambo hili ni katika madhambi makubwa, atakayelifanya atakuwa amestahiki ahadi hii ya adhabu kali.

Mafunzo

  • Kuwatii viongozi ni wajibu katika mambo yasiyomuasi Mwenyezi Mungu Mtukufu.
  • Kuna tahadhari kubwa kwa aliyetoka katika utiifu kwa kiongozi, na akasambaratisha umoja wa waislamu, akifa katika hali hii, atakuwa amekufa katika njia ya watu wajinga.
  • Katika hadithi kuna katazo la kupigana vita kwa sababu ya ubaguzi.
  • Ulazima wa kutimiza makubaliano.
  • Katika utiifu na kushikamana na umoja kuna heri nyingi, na amani na utulivu, na hali kutengamaa.
  • Katazo la kujifananisha na watu zama za ujinga.
  • Amri ya kushikamana na umoja wa waislamu.
Ufafanuzi: العربية

بَيَّنَ النبيُّ صلى الله عليه وسلم أنَّ مَن خَرَجَ عن طاعة ولاة الأمور، وفارق جماعة الإسلام المُتَّفِقة على بيعة الإمام، فمات على تلك الحال من المفارقة وعدم الطاعة، مات ميتة أهل جاهلية، الذين كانوا لا يطيعون أميرًا ولا يَنْضَمُّونَ إلى جماعة واحدة، بل كانوا فِرَقًا وعصائب يقاتل بعضهم بعضًا. وأخبر صلى الله عليه وسلم أنَّ مَن قاتل تحت راية لا يَستَبينُ فيها وجه الحق من الباطل، يغضب لمحض التَّعَصُّبِ لقومه أو قبيلته، لا لنصرة الدين والحق، فيقاتل تعصُّبًا بغير بصيرة وعلم، فإذا قُتِل على تلك الحال، كانت كقتلة الجاهلية. وأنَّ مَن خرج على أمته صلى الله عليه وسلم يَضربُ صالحَها، وفاجرَها، ولا يبالي بما يفعله ولا يخاف عقوبتَه مِن قَتْلِ مؤمنِها، ولا يفي لأصحاب العهد من الكفار أو ولاة الأمور بعهدِهم بل يَنقضُها، فهو ليس مني ولست منه.

  • النهي عن التشبه بأحوال أهل الجاهلية.
  • وجوب طاعة ولاة الأمور في غير معصية الله عز وجل.
  • التحذير شديد لمن خرج عن طاعة الإمام، وفارق جماعة المسلمين، فإذا مات على هذه الحال، مات ميتة جاهلية.
  • النهي عن قتال العصبية.
  • وجوب الوفاء بالعهود.
  • في الطاعة ولزوم الجماعة الخير الكثير، والأمن والطمأنينة، وصلاح الأحوال.
  • هذا الوعيد في الحديث يدل على أن هذه الأعمال من كبائر الذنوب.

Mada

Ripoti kosa

Zaidi