Hadithi

Gaweni mirathi kwa wastahiki wake, itakayobakia basi mwenye kustahiki zaidi upande wa mwanaume ni wa kiume

Chanzo: HadeethEnc.com, Kiswahili v1.18.0

SahihiWamekubaliana Bukhari na Muslim juu ya usahihi wake

Matini ya Kiarabu

عَنِ ابْنِ عَبَّاسٍ رَضِيَ اللَّهُ عَنْهُمَا عَنِ النَّبِيِّ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ قَالَ: «أَلْحِقُوا الفَرَائِضَ بِأَهْلِهَا، فَمَا بَقِيَ فَلِأَوْلَى رَجُلٍ ذَكَرٍ».

Tafsiri

Imepokelewa kutoka kwa bin Abbas -radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yao -kutoka kwa Mtume wa Mwenyezi Mungu -rehema na amani za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake - amesema: "Gaweni mirathi kwa wastahiki wake, itakayobakia basi mwenye kustahiki zaidi upande wa mwanaume ni wa kiume".

Ufafanuzi

Anawaamrisha Mtume rehema na amani ziwe juu yake wenye kusimamia ugawaji wa mirathi wazigawe kwa wastahiki wake kwa mgao wa uadilifu wa kisheria kama alivyotaka Mwenyezi Mungu Mtukufu, ataanza kwa kuwapa wale wenye fungu lililokadiriwa tayari kisheria, kulingana na mafungu yao katika kitabu cha Mwenyezi Mungu, nayo ni: Theluthi mbili, na theluthi moja, na sudusu (moja ya sita) na nusu, na robo, thumunu (moja ya nane), mali itakayobakia baada ya hapo, hiyo atapewa ndugu wa karibu na maiti katika wanaume, na ndugu hao huitwa aswaba (warithi wasio na mipaka).

Mafunzo

  • Hadithi hii ni kanuni katika ugawaji wa urithi.
  • Nikuwa ugawaji wa mirathi huanza na wale wanaostahiki kurithi waliopangiwa viwango.
  • Kuwa mali iliyobakia baada ya hao wenye kiwango cha kisheria ni ya ndugu wa mwanaume.
  • Kumtanguliza ndugu wa karibu kisha anayefuata, hatakiwi kurithi ndugu wa mbali kama baba mdogo, pamoja nakuwa ndugu wa karibu wapo kama baba.
  • Ndugu asiye na kiwango katika sheria hana haki ya kurithi endapo mali itamalizika, ikawa haikubakia chochote.
Ufafanuzi: العربية

يأمر النبي صلى الله عليه وسلم القائمين على قسمة التركة أن يوزعوها على مستحقيها بالقسمة العادلة الشرعية كما أراد الله تعالى، فيعطى أصحاب الفروض المقدرة فروضهم في كتاب الله، وهي الثلثان والثلث والسدس والنصف والربع والثمن، فما بقى بعدها، فإنه يعطى إلى من هو أقرب إلى الميت من الرجال، ويسمون العصبة.

  • الحديث قاعدة في قسمة التركة.
  • أن قسمة الفرائض تكون بالبداءة بأهل الفرائض.
  • أن ما بقي بعد الفروض للعصبة.
  • تقديم الأقرب فالأقرب فلا يرث عاصب بعيد كالعم، مع وجود عاصب قريب كالأب.
  • أنه لا شيء للعاصب إذا استغرقت الفروض التركة، أي لم يبق منها شيئًا.

Mada

Ripoti kosa

Zaidi