Hadithi

Atakayemuendea mpiga ramli akamuuliza kuhusu lolote hazitokubaliwa sala zake siku arobaini

Chanzo: HadeethEnc.com, Kiswahili v1.18.0

SahihiImepokelewa Imamu Muslim

Matini ya Kiarabu

عن بعض أزواج النبي صلى الله عليه وسلم عن النبي صلى الله عليه وسلم قال: «مَنْ أَتَى عَرَّافًا فَسَأَلَهُ عَنْ شَيْءٍ لَمْ تُقْبَلْ لَهُ صَلَاةٌ أَرْبَعِينَ لَيْلَةً».

Tafsiri

Kutoka kwa baadhi ya wake za Mtume -Rehema amani ziwe juu yake- kutoka kwa Mtume -Rehema amani ziwe juu yake- amesema: "Atakayemuendea mpiga ramli akamuuliza kuhusu lolote hazitokubaliwa sala zake siku arobaini".

Ufafanuzi

Anatahadharisha Mtume -Rehema amani ziwe juu yake- kuwaendea wapiga ramli na hili ni jina la kiujumla la kuhani na mtabiri wa nyota na mpiga ramli na mfano wao, katika wale wanaotumia ishara za vitanguliza ili kudai kujua elimu ya ghaibu, nakuwa kumuuliza pekee mambo ya ghaibu Mwenyezi Mungu atamnyima thawabu za swala yake siku arobaini; na hiyo ni adhabu kwake kwa kosa hili na dhambi kubwa.

Mafunzo

  • Uharamu wa ukuhani, na kwenda kwa makuhani na kuwauliza mambo ya ghaibu.
  • Mtu anaweza kunyimwa thawabu za ibada ikiwa ni adhabu kwake kwa kutenda kwake maasi.
  • Yanaingia katika hadithi hii yanayoitwa nyota na kutazamia, na kusoma viganja na vikombe hata kama ni kwa kutaka kujua pekee; kwa sababu hiyo yote ni katika ukuhani na ni katika kudai kujua elimu ya ghaibu.
  • Ikiwa haya ndiyo malipo ya mwenye kumuendea mpiga ramli, ni vipi malipo ya mpiga ramli mwenyewe?.
  • Swala za siku arobaini zinaangukia katika kutokubalika, si wajibu kuzilipa lakini hazina thawabu ndani yake.
Ufafanuzi: العربية

يُحَذِّرُ النبيُّ صلى الله عليه وسلم من إتيان العرّاف -هو اسم عام للكاهن والمُنِّجم والرَّمَّال ونحوهم، ممن يَسْتَدِلُّ على معرفة الغيب بمقدمات يستعملها -، وأنَّ مُجَرَّدَ سؤالِهِ عن شيء من أمور الغيب سيَحْرِمُه الله به ثوابَ صلاته أربعين يومًا؛ وذلك عقوبة له على هذا الإثم والذنب الكبير.

  • تحريم الكَهَانة، والذهاب إلى الكُهان وسؤالهم عن المغيبات.
  • قد يُحْرَمُ الإنسانُ مِن ثواب الطاعة عقوبة له على فعل المعصية.
  • يَدْخُلُ في الحديث ما يُسمّى بالأبراج والنظر فيها، وقراءة الكَفِّ والفنجان -ولو على سبيل الاطلاع فقط-؛ لأن ذلك كلَّه من الكهانة ومن دعوى علم الغيب.
  • إذا كان هذا جزاءَ مَن أتى العَرّاف، فكيف بجزاء العراف نفسه؟
  • صلاة أربعين يومًا تَقَعُ مُجزئة لا يَجِبُ قضاؤها، ولكن لا ثواب فيها.

Mada

Ripoti kosa

Zaidi