Chanzo: HadeethEnc.com, Kiswahili v1.18.0
SahihiImepokelewa na Al-Bukhaariy
Matini ya Kiarabu
عَنْ أَبِي بَكْرَةَ رَضِيَ اللهُ عَنْهُ أَنَّهُ سَمِعَ رَسُولَ اللهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ يَقُولُ: «لَنْ يُفْلِحَ قَوْمٌ وَلَّوْا أَمْرَهُمُ امْرَأَةً».
Tafsiri
Imepokelewa kutoka kwa Abuu Bakra -radhi za Allah ziwe juu yake- yakuwa yeye alimsikia Mtume -rehema na amani ziwe juu yake- akisema: "Hawatofanikiwa watu waliomkabidhi utawala wao mwanamke".
Ufafanuzi
Amebainisha Mtume rehema na amani ziwe juu yake ya kwamba hawatofanikiwa watu kwa kupata wanayoyataka pindi watakapomtawalisha na kummilikisha mwanamke swala la hukumu au usimamizi wa dola au wizara.
Mafunzo
- Wanawake hawasimamii uongozi wala hukumu kwa watu, na mfano wa hayo katika usimamizi wa majukumu makuu, ama mambo maalumu kama usimamizi wa mali za wakfu au mayatima au ukuu wa shule na mfano wa hayo hakuna tatizo.
- Kumebainishwa udhaifu mkubwa wa mwanamke, na kwamba hashirikiani na wanaume katika usimamizi mkuu, na kwamba kusimamia kwake mfano wa majukumu hayo ni sababu ya kukosa mafanikio.
- Mwenyezi Mungu alimuumba mwanamke, na akamuwekea tabia zinazotofautiana na tabia za mwanaume, kuna mambo hayafai kusimamiwa na mwanamke; kulingana na tabia yake ya kipekee, vile vile kuna mambo hayafai kusimamiwa na mwanaume; kulingana na tabia yake ya kipekee.
- Kufanikiwa kulikokanushwa: Ni kufanikiwa kuliko tajwa katika ulimi wa sheria, nako ni kupatikana kwa kheri za dunia na akhera, na haimaanishi ustawi wa ufalme kuwa watu wanampendeza Mwenyezi Mungu, yeyote asiyemtii Mwenyezi Mungu si miongoni mwa waliofanikiwa, hata kama yuko katika hali nzuri zaidi katika kile kinachoonekana miongoni mwa mambo yake ya kidunia.
- Hakuna maana yoyote ya kumshusha hadhi mwanamke katika hadithi hii, lakini ni maelekezo ya uwezo wake sahihi unaomfaa kwake.
Ufafanuzi: العربية
بيَّن النبي صلى الله عليه وسلم أنه لن يظفر قوم بما يطلبون إذا وَلَّوا وملَّكوا المرأةَ أمرَهم من قضاء أو ولاية عامة أو وزارة.
- النساء لا يلين الإمارة ولا القضاء بين الناس، ونحو ذلك من الولايات العامة، أما الأمور الخاصة كولاية وقف أو يتامى أو إدارة مدرسة ونحو ذلك فلا بأس.
- بيان قصور ضعف المرأة، وأنها لا تشارك الرجل في الولايات العامة، وأن توليها مثل ذلك سبب لعدم الفلاح.
- خلق الله المرأة، وجعل لها طبيعة تختلف عن طبيعة الرجل، فثمّة أمور لا يصلح أن تقوم بها المرأة؛ نظرًا لطبيعتها الخاصة، وكذلك ثمة أمور لا يصلح أن يقوم بها الرجل؛ نظرًا لطبيعتها الخاصة.
- الفلاح المنفي: هو الفلاح في لسان الشرع، وهو تحصيل خير الدنيا والآخرة، ولا يلزم من ازدهار الملك أن يكون القوم في مرضاة الله، ومن لم يكن في طاعة الله، فليس من المفلحين، ولو كان في أحسن حال فيما يبدو من أمر دنياه.
- ليس في هذا الحديث انتقاص للمرأة، ولكنه توجيه لقدراتها التوجيه الصحيح المناسب لها.