Hadithi

Lau kama mtu atadhamiria ubaya akiwa katika mji wa eden (Yemen) mbali huko, basi Mwenyezi Mungu angemuonjesha adhabu chungu

Chanzo: HadeethEnc.com, Kiswahili v1.18.0

SahihiImepokelewa na Ahmad na Al Hakim

Matini ya Kiarabu

عَنْ عَبْدِ اللَّهِ بْنِ مَسْعُودٍ رَضِيَ اللَّهُ عَنْهُ رَفَعَهُ: فِي قَوْلِ اللَّهِ عَزَّ وَجَلَّ: {وَمَنْ يُرِدْ فِيهِ بِإِلْحَادٍ بِظُلْمٍ نُذِقْهُ مِنْ عَذَابٍ أَلِيمٍ} [الحج: 25] قَالَ: «لَوْ أَنَّ رَجُلًا هَمَّ فِيهِ بِإِلْحَادٍ وَهُوَ بِعَدَنِ أَبْيَنَ لَأَذَاقَهُ اللَّهُ عَذَابًا أَلِيمًا».

Tafsiri

Imepokelewa kutoka kwa Abdullahi bin Masoud radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake (Hadithi Marfu'u): Katika kauli yake Aliyetakasika na kutukuka: "Na yeyote anayetaka, ndani ya Msikiti Mtukufu, kwenda kombo na haki kwa njia ya udhalimu na akamuasi Mwenyezi Mungu humo ndani, basi tutamuonjesha adhabu kali yenye kuumiza" [Al-Hajji:25] Akasema: "Lau kama mtu atadhamiria ubaya akiwa katika mji wa eden (Yemen) mbali huko, basi Mwenyezi Mungu angemuonjesha adhabu chungu".

Ufafanuzi

Ameeleza Abdallah bin Masudi radhi za Allah ziwe juu yake katika kauli yake Aliyetakasika na kutukuka: "Na yeyote anayetaka, ndani ya Msikiti Mtukufu, kwenda kombo na haki kwa njia ya udhalimu na akamuasi Mwenyezi Mungu humo ndani, basi tutamuonjesha adhabu kali yenye kuumiza" [Al-Hajji: 25], akasema: Lau mtu yeyote atawaza ndani ya nafsi yake na akaazimia kufanya jambo baya ndani ya sehemu tukufu ya Makka, likahalalishwa ndani yake aliloliharamisha Mwenyezi Mungu, kama makosa ya ulimi au kuuwa kwa makusudi, basi hiyo ni dhulma, hata kama maazimio atayaweka akiwa katika mji wa Eden huko Yemen, basi huyu atastahiki Mwenyezi Mungu amuonjeshe adhabu chungu kwa sababu ya hilo, hata kama hajalifanya, maazimio yake katika hilo yanatosha.

Mafunzo

  • Kumebainishwa umahususi wa Haramu na kuitukuza kwake.
  • Amesema Assa'diy: Na katika aya hii tukufu, kuna uwajibu wa kuiheshimu Haramu na kuitukuza sana, na tahadhari ya kudhamiria maasi ndani yake na kuyatenda.
  • Amesema Adh-dhahaku: Hakika mtu anapodhamiria ovu Makka huku akiwa katika ardhi nyingine linaandikwa juu yake kuwa ni dhambi hata kama hajalitenda.
Ufafanuzi: العربية

ذكر عبد الله بن مسعود رضي الله عنه في قول الله عز وجل: {وَمَنْ يُرِدْ فِيهِ بِإِلْحَادٍ بِظُلْمٍ نُذِقْهُ مِنْ عَذَابٍ أَلِيمٍ} [الحج: 25]، قال: لو أن أحدًا من الناس حدّث نفسه وعزم أن يعمل في حرم مكة عملًا سيئًا تسْتحلّ فيه من الحرم ما حرم الله عليك من لسان أو قتل عامدًا أن ذلك ظلم، ولو كان العزم بمدينة عدن في اليمن فإنه مستحق أن يصيبه الله بعذاب أليم لأجل ذلك، ولو لم يفعله، فيكفي في ذلك أن يعزم.

  • بيان خصوصية الحرم وتعظيمه.
  • قال السعدي: وفي هذه الآية الكريمة، وجوب احترام الحَرَم، وشدة تعظيمه، والتحذير من إرادة المعاصي فيه وفعلها.
  • قال الضَّحَّاك: إنَّ الرجل ليهِمُّ بالخطيئة بمكّة وهو بأرض أخرى فتكُتب عليه ولم يعملها.

Mada

Ripoti kosa

Zaidi