Hadithi

Halitoacha kuendelea kudhihiri kundi katika Umma wangu, mpaka iwajie amri ya Mwenyezi Mungu nao wakiwa katika kudhihiri huko

Chanzo: HadeethEnc.com, Kiswahili v1.18.0

SahihiWamekubaliana Bukhari na Muslim juu ya usahihi wake

Matini ya Kiarabu

عَنِ المُغِيرَةِ بْنِ شُعْبَةَ رَضِيَ اللَّهُ عَنْهُ عَنِ النَّبِيِّ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ قَالَ: «لاَ يَزَالُ طَائِفَةٌ مِنْ أُمَّتِي ظَاهِرِينَ، حَتَّى يَأْتِيَهُمْ أَمْرُ اللَّهِ وَهُمْ ظَاهِرُونَ».

Tafsiri

Kutoka kwa Mughira bin Shuuba -radhi za Allah ziwe juu yake- kutoka kwa Mtume -rehema na amani ziwe juu yake- amesema: "Halitoacha kuendelea kudhihiri kundi katika Umma wangu, mpaka iwajie amri ya Mwenyezi Mungu nao wakiwa katika kudhihiri huko".

Ufafanuzi

Ameeleza Mtume rehema na amani ziwe juu yake ya kuwa hawatoacha watu katika Umma wake kuendelea kuwepo, na kuwashinda wanaopingana nao, na hilo litaendelea mpaka iwajie amri ya Mwenyezi Mungu kwa kuchukuliwa roho zao mwisho wa zama za dunia kabla ya kusimama kwa Kiyama.

Mafunzo

  • Muujiza wa wazi wa Mtume rehema na amani ziwe juu yake, kwani wasifu huu bado unaendelea Alhamdulillaah, kwanzia zama za Mtume rehema na amani ziwe juu yake mpaka hivi sasa, na bado utaendelea mpaka ije amri ya Mwenyezi Mungu iliyotajwa katika hadithi.
  • Fadhila za kuwa na msimamo katika haki na kuifanyia kazi, na himizo juu ya hilo.
  • Kudhihiri kwa dini kuna aina mbili: Ima kudhihiri kwa hoja na ubainifu na uwazi, na ima kudhihiri kwa dola na mhimili, na kudhihiri kulikobakia ni kwa hoja na ubainifu; kwa sababu hoja ya Uislamu ni Qur'ani, nayo iko wazi na inavitawala vitabu vingine visivyokuwa hiyo, lakini aina ya pili ya kudhihiri, ni kudhihiri kwa nguvu ya dola na mhimili, na hii inategemea kulingana na imani na kuwa na nguvu katika ardhi.
Ufafanuzi: العربية

أخبر النبي صلى الله عليه وسلم أنه لن يزال قوم من أمتي ظاهرين على الناس، غالبون على من خالفهم، وذلك حتى يأتيهم أمر الله بقبض أرواحهم في آخر زمن الدنيا قبل قيام الساعة.

  • معجزة ظاهرة للنبي صلى الله عليه وسلم، فإن هذا الوصف ما زال بحمد الله من زمن النبي صلى الله عليه وسلم إلى الآن، ولا يزال حتى يأتي أمر الله المذكور في الحديث.
  • فضل الثبات على الحق والعمل به، والحث على ذلك.
  • ظهور الدين نوعان إما ظهور بالحجة والبيان والوضوح وإما ظهور بالقوة والسنان، والظهور باق بالحجة والبيان؛ لأن حجة الإسلام هي القرآن، وهو ظاهر ومهيمن على كل ما عداه، ولكن النوع الثاني من الظهور، ظهور القوة والسنان فهذا بحسب الإيمان والتمكين في الأرض.

Mada

Ripoti kosa

Zaidi