Hadithi

Amesema Mwenyezi Mungu Mtukufu: Watu wa aina tatu mimi ndiye mgomvi wao siku ya Kiyama

Chanzo: HadeethEnc.com, Kiswahili v1.18.0

SahihiImepokelewa na Al-Bukhaariy

Matini ya Kiarabu

عَنْ أَبِي هُرَيْرَةَ رَضِيَ اللَّهُ عَنْهُ عَنِ النَّبِيِّ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ قَالَ: «قَالَ اللَّهُ تَعَالَى: ثَلاَثَةٌ أَنَا خَصْمُهُمْ يَوْمَ القِيَامَةِ: رَجُلٌ أَعْطَى بِي ثُمَّ غَدَرَ، وَرَجُلٌ بَاعَ حُرًّا فَأَكَلَ ثَمَنَهُ، وَرَجُلٌ اسْتَأْجَرَ أَجِيرًا فَاسْتَوْفَى مِنْهُ وَلَمْ يُعْطِهِ أَجْرَهُ».

Tafsiri

Imepokelewa kutoka kwa Abuu Huraira radhi za Allah ziwe juu yake kutoka kwa Mtume rehema na amani ziwe juu yake amesema: "Amesema Mwenyezi Mungu Mtukufu: Watu wa aina tatu mimi ndiye mgomvi wao siku ya Kiyama: Mtu aliyetoa (kiapo) kwa jina langu kisha akafanya usaliti, na mtu aliyemuuza mtu huru kisha akala thamani yake, na mtu aliyempa kazi mwajiriwa, akatimiza majukumu yake na hakumpa malipo yake".

Ufafanuzi

Ameeleza Mtume rehema na amani ziwe juu yake ya kwamba Mwenyezi Mungu Mtukufu amesema: Watu wa aina tatu mimi ndiye nitakayepambana nao siku ya Kiyama, na nitakayekuwa mgomvi wake basi nitapambana naye na kumshinda: Wa kwanza: Atakayetoa kiapo na akaapa kwa jina la Mwenyezi Mungu, na akachukua ahadi kisha akaitengua na kufanya hiana. Wa pili: Atakayemuuza mtu huru kwa kumfanya kuwa mtumwa na akala thamani yake na akakitumia kiwango cha pesa aliyopata. Wa tatu: Atakayemuajiri muajiriwa katika kazi, akamtimizia kazi yake na hakumpa thamani ya kazi yake.

Mafunzo

  • Hadithi hii ni miongoni mwa yale anayoyapokea Mtume rehema na amani ziwe juu yake kutoka kwa Mola wake, na huitwa Hadithil-Qudsi au Ilaahi (Hadithi takatifu), nayo ni ile ambayo lafudhi yake na maana yake inatoka kwa Mwenyezi Mungu, isipokuwa haina umaalumu kama wa Qur'ani ambao imesifika nao, kama kisomo chake kuwa ni ibada, nakuwa na twahara wakati wa kusoma, na kutoa changamoto na mengineyo.
  • Amesema Assindi: Imesemwa: Kutaja aina tatu haimaanishi ni hizi pekee; kwa sababu yeye Mtukufu ni mpinzani wa madhalimu wote, bali ni kwa ajili ya kuwatilia mkazo watu hawa.
  • Amesema bin Jauzi: Mtu huru ni mja wa Mwenyezi Mungu, hivyo, atakayemtendea kosa la jinai basi mgomvi wake ni bwana yake, ambaye ni Mwenyezi Mungu.
  • Amesema Al-Khattwabi: Kumzingatia mtu kuwa yuko huru hutokea kwa mambo mawili: Amuache huru kisha afiche hilo au akane. La pili: Amtumikishe kwa lazima baada ya kumuacha huru , na la kwanza ndio baya zaidi. Nikasema: Na hadithi ya mlango huu iliyoyaeleza ni mabaya mno; kwa sababu pamoja na kuficha kumuacha huru au kukana kuna kutenda kwa muktadha wa hayo, kama kumuuza na kula thamani yake, na ndio maana ahadi ya adhabu ikawa kubwa.
Ufafanuzi: العربية

أخبر النبي صلى الله عليه وسلم أن الله تعالى قال: ثلاثة أصناف أنا خصمهم يوم القيامة، ومن كنت خصمَه خصمتُه وغلبتُه: الأول: من أعطى يمينه وحلف بالله، وعاهد عهدًا ثم نقضه وغدر. الثاني: من باع رجلًا حرًّا على أنه عبد فأكل ثمنه وتصرّف بقيمته. الثالث: من استأجر أجيرًا لعمل، فاستوفى منه العمل ولم يعطِه ثمن عمله.

  • هذا الحديث مما يرويه النبي صلى الله عليه وسلم عن ربه، ويسمى بالحديث القدسي أو الإلهي، وهو الذي لفظه ومعناه من الله، غير أنه ليست فيه خصائص القرآن التي امتاز بها عما سواه، من التعبد بتلاوته والطهارة له والتحدي والإعجاز وغير ذلك.
  • قال السندي: قيل: ذكر الثلاثة ليس للتخصيص؛ لأنه تعالى خصْمٌ لجميع الظالمين بل للتشديد على هؤلاء الثلاثة.
  • قال ابن الجوزي: الحر عبد الله، فمن جنى عليه فخصمه سيده، الذي هو الله.
  • قال الخطابي: اعتباد الحر يقع بأمرين: أن يعتقه ثم يكتم ذلك أو يجحد. والثاني أن يستخدمه كرهًا بعد العتق، والأول أشدهما. قلت: وحديث الباب أشد؛ لأن فيه مع كتم العتق أو جحده العمل بمقتضى ذلك من البيع وأكل الثمن فمن ثم كان الوعيد عليه أشد.

Mada

Ripoti kosa

Zaidi