Hadithi

Hakika zitatokea fitina, kisha tambueni kuwa fitina ya aliyekaa ndani inanafuu kuliko anayetembea, na anayetembea ndani yake inanafuu kuliko anayeikimbilia,

Chanzo: HadeethEnc.com, Kiswahili v1.18.0

SahihiImepokelewa Imamu Muslim

Matini ya Kiarabu

عَنْ عُثْمَانَ الشَّحَّامِ، قَالَ: انْطَلَقْتُ أَنَا وَفَرْقَدٌ السَّبَخِيُّ إِلَى مُسْلِمِ بْنِ أَبِي بَكْرَةَ وَهُوَ فِي أَرْضِهِ، فَدَخَلْنَا عَلَيْهِ فَقُلْنَا: هَلْ سَمِعْتَ أَبَاكَ يُحَدِّثُ فِي الْفِتَنِ حَدِيثًا؟ قَالَ: نَعَمْ، سَمِعْتُ أَبَا بَكْرَةَ رضي الله عنه يُحَدِّثُ، قَالَ: قَالَ رَسُولُ اللهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ: «إِنَّهَا سَتَكُونُ فِتَنٌ، أَلَا ثُمَّ تَكُونُ فِتْنَةٌ الْقَاعِدُ فِيهَا خَيْرٌ مِنَ الْمَاشِي فِيهَا، وَالْمَاشِي فِيهَا خَيْرٌ مِنَ السَّاعِي إِلَيْهَا، أَلَا فَإِذَا نَزَلَتْ أَوْ وَقَعَتْ فَمَنْ كَانَ لَهُ إِبِلٌ فَلْيَلْحَقْ بِإِبِلِهِ، وَمَنْ كَانَتْ لَهُ غَنَمٌ فَلْيَلْحَقْ بِغَنَمِهِ، وَمَنْ كَانَتْ لَهُ أَرْضٌ فَلْيَلْحَقْ بِأَرْضِهِ»، قَالَ فَقَالَ رَجُلٌ: يَا رَسُولَ اللهِ أَرَأَيْتَ مَنْ لَمْ يَكُنْ لَهُ إِبِلٌ وَلَا غَنَمٌ وَلَا أَرْضٌ؟ قَالَ: «يَعْمِدُ إِلَى سَيْفِهِ فَيَدُقُّ عَلَى حَدِّهِ بِحَجَرٍ، ثُمَّ لِيَنْجُ إِنِ اسْتَطَاعَ النَّجَاءَ، اللهُمَّ هَلْ بَلَّغْتُ؟ اللهُمَّ هَلْ بَلَّغْتُ؟ اللهُمَّ هَلْ بَلَّغْتُ؟»، قَالَ: فَقَالَ رَجُلٌ: يَا رَسُولَ اللهِ أَرَأَيْتَ إِنْ أُكْرِهْتُ حَتَّى يُنْطَلَقَ بِي إِلَى أَحَدِ الصَّفَّيْنِ، أَوْ إِحْدَى الْفِئَتَيْنِ، فَضَرَبَنِي رَجُلٌ بِسَيْفِهِ، أَوْ يَجِيءُ سَهْمٌ فَيَقْتُلُنِي؟ قَالَ: «يَبُوءُ بِإِثْمِهِ وَإِثْمِكَ، وَيَكُونُ مِنْ أَصْحَابِ النَّارِ».

Tafsiri

Kutoka kwa Othman As Shaham, amesema:Niliondoka mimi pamoja na Farqad As Sabakhi kwenda kwa Muslim bin Abii Bakara naye akiwa katika mji wake, tukaingia kwake na tukasema: Hivi uliwahi kumsikia baba yako akisimulia hadithi yoyote kuhusu fitina? Akasema: Ndiyo, Nilimsikia Abuu Bakra radhi za Allah ziwe juu yake akihadithia, akasema: Alisema Mtume rehema na amani ziwe juu yake: "Hakika zitatokea fitina, kisha tambueni kuwa fitina ya aliyekaa ndani inanafuu kuliko anayetembea, na anayetembea ndani yake inanafuu kuliko anayeikimbilia, tambueni itakapoteremka au ikatokea basi atakayekuwa na ngamia basi na amfuate ngamia wake, na atakayekuwa na mbuzi basi na amfuate mbuzi wake, na atakayekuwa na ardhi basi na aende katika ardhi yake", anasema, akasema mtu mmoja: Ewe Mjumbe wa Mwenyezi Mungu wasemaje ikiwa mtu hana ngamia wala mbuzi wala ardhi? Akasema: "Basi achukue panga lake na apige upande wa makali yake katika jiwe, kisha aokoke akiweza kuokoka, ewe Allah je nimefikisha? ewe Allah je nimefikisha? ewe Allah je nimefikisha?" Akasema: Akasema mtu mmoja: Ewe Mjumbe wa Mwenyezi Mungu wasemaje endapo nitalazimishwa mpaka nikapelekwa katika moja kati ya safu mbili, au moja kati ya makundi mawili, mtu mmoja akanipiga kwa panga lake, au ukanilenga mshale ukaniua? Akasema: "Yeye ndiye atakayebeba dhambi zake na dhambi zako, na atakuwa miongoni mwa watu wa motoni".

Ufafanuzi

Othman Ash Shaham na Farqad As-Sabakhi walimuuliza Muslim mtoto wa Swahaba mtukufu Abuubakra radhi za Allah ziwe juu yake: Je alisikia kutoka kwa baba yake hadithi kutoka kwa Mtume rehema na amani ziwe juu yake katika fitina na vita itakayotokea baina ya waislamu? Akasema: Naam, alieleza Mtume rehema na amani ziwe juu yake ya kwamba itatokea fitina baada ya kifo chake, na fitina hii aliyekaa na kughafilika nayo ni bora kuliko anayetembea ndani yake, na anaitafuta pasina kujua, na anayetembea ndani yake ni bora kuliko anayekwenda mbio kuiendea na kuitafuta na kushiriki ndani yake. Kisha akaelekeza Mtume rehema na amani ziwe juu yake itakayeshuka na kufika fitina katika zama zake na kwake kukapatikana upenyo atakaokimbilia; atakayekuwa na ngamia anayechunga basi aifuate ngamia yake, na atakayekuwa na mbuzi anayechunga basi amfuate mbuzi wake, na atakayekuwa na ardhi na shamba basi aende shambani kwake. Bwana mmoja akasema: Ewe Mjumbe wa Mwenyezi Mungu hivi wasemaje kwa mtu ambaye hatokuwa na makimbilio kama ngamia wala mbuzi wala shamba? Akasema: Basi aende akachukue silaha yake aipige na ailainishe, kisha akimbie na ajinusuru yeye na mwanaye ikiwa ataweza kuokoka. Kisha akataka ushuhuda rehema na amani ziwe juu yake mara tatu, akasema: Ewe Allah je, nimefikisha? Ewe Allah je nimefikisha? Ewe Allah je nimefikisha?. Bwana mmoja akasema: Ewe Mjumbe wa Mwenyezi Mungu wasemaje ikiwa nitalazimishwa kushiriki pamoja na safu moja, au moja kati ya makundi mawili, akanipiga mtu kwa panga lake, au mshale ukanilenga ukaniuwa?. Akasema: Atarudi na madhambi yake na madhambi ya aliyemuuwa, na siku ya Kiyama atakuwa miongoni mwa watu wa motoni.

Mafunzo

  • Habari ya kutokea fitina na tahadhari dhidi yake, na ili watu wajiandae nayo, wasijiingize ndani yake, na wamuombe Mwenyezi Mungu subira na kuokoka dhidi ya shari zake.
  • Amesema Nawawi: Kauli yake rehema na amani ziwe juu yake: "Aliyekaa ndani yake ni bora kuliko aliyesimama", mpaka mwisho wake, maana yake ni kubainishwa hatari yake, na himizo la kuiepuka, na kuikimbia, na kwamba shari yake na fitina yake inakuwa kulingana na namna mtu alivyofungamana nayo.
  • Amesema Nawawi: Kumeondolewa dhambi kwa aliyelazimishwa atakayehudhuria huko, na ama kuuwa si halali hata kwa kulazimishwa, bali aliyelazimishwa anapata dhambi kwa lile aliloamrishwa kwa makubaliano ya wanachuoni wote.
  • Amesema bin Hajari: Na wamesema wengine: Likifanya dhulma kundi likatoka kwa kiongozi likakataa kutekeleza wajibu wake na likaanzisha vita basi ni wajibu kulipiga vita, na vile vile yakipigana makundi mawili ni wajibu kwa kila mwenye kuweza kumzuia mkosefu na kumtetea aliyepigwa, na hii ndio kauli ya jopo la wanachuoni, na wamefafanua wengine, wakasema: Kila mapigano yatakayotokea kati ya makundi mawili ya waislamu kiasi kwamba hakuna kiongozi wa umma, basi hapo mapigano hayo ni marufuku, na zinashuka hadithi zote zilizopo katika mlango huu na nyinginezo.
  • Amesema Nawawi: Na wametofautiana wanachuoni katika mapigano ya fitina, kundi miongoni mwao wakasema: Hakuna kupigana katika fitina ya waislamu, hata wakiingia ndani ya nyumba yake, na wakataka kumuuwa, hairuhusiwi kwake kujihami; kwa sababu kamtaka hilo kwa ufahamu potofu, na hii ni kauli ya Abii Bakra Swahaba radhi za Allah ziwe juu yake na wengineo, na amesema bin Omari na Imrani bin Huswaini radhi za Allah ziwe juu yao: Haingii hapa, lakini akikusudia kujihami, kauli zote hizi mbili zimeafikiana juu ya kuacha kuingia katika fitina zote za Uislamu. Na wamesema Maswahaba wengi na wanafunzi wao na wanachuoni wote wa Uislamu: Ni wajibu kumtetea mwenye haki katika fitina, na kusimama naye kwa kupigana na adui jeuri, kama alivyosema Mtukufu: "Basi lipigeni kundi linalodhulumu mpaka lirejee kwenye amri ya Mwenyezi Mungu..." mpaka mwisho wa aya, na kauli hii ndiyo sahihi, na hadithi hii inafasiriwa kwa yule ambaye hajabainikiwa na haki, au juu ya makundi mawili dhalimu, na hakuna lolote lililoelewa vibaya aya au hadithi miongoni mwao.
Ufafanuzi: العربية

سأل عثمانُ الشحام وفرقدٌ السبخي مسلمَ ابنَ الصحابي الجليل أبي بكرة رضي الله عنه: هل سمع من أبيه حديثًا عن النبي صلى الله عليه وسلم في الفتن والقتال الذي يقع بين المسلمين؟ فقال نعم، أخبر النبي صلى الله عليه وسلم أنها ستكون فتن بعد موته، وهذه الفتن القاعد الغافل عنها خير من الماشي فيها وهو لا يستشرفها ويبحث عنها، والماشي فيها خير من المسرع إليها يبحث عنها ويشارك فيها. ثم أرشد النبي صلى الله عليه وسلم من نزلت أو وقعت الفتنة في زمنه وعنده إنْ وجد ملجأ أن يأوي إليه؛ فمن كان له إبل ترعى فليلحق بإبله، ومن كانت له غنم ترعى فليلحق بغنمه، ومن كانت له أرض ومزرعة فليلحق بأرضه. فقال رجل: يا رسول الله أرأيت من لم يكن له مأوى من إبل ولا غنم ولا أرض؟ قال: يعمد إلى سلاحه فيدقه ويعطبه، ثم ليهرب وينجوا بنفسه وولده إن استطاع النجاء. ثم أشهد صلى الله عليه وسلم ثلاثًا فقال: اللهم هل بلغت؟ اللهم هل بلغت؟ اللهم هل بلغت؟ فقال رجل: يا رسول الله أرأيت إن أجبرت أن أشارك مع أحد الصفين، أو إحدى الفئتين، فضربني رجل بسيفه، أو يجيء سهم فيقتلني؟ قال: يرجع بإثم نفسه وإثم من قتل، ويكون يوم القيامة من أصحاب النار.

  • الإخبار بوقوع الفتن للتحذير منها، وليتأهب الناس لها، فلا يخوضوا فيها، ويسألوا الله الصبر والنجاة من شرها.
  • قال النووي: قوله صلى الله عليه وسلم :(القاعد فيها خير من القائم)، إلى آخره، فمعناه بيان عظيم خطرها، والحث على تجنبها، والهرب منها، وأن شرها وفتنتها يكون على حسب التعلق بها.
  • قال النووي: رفع الإثم عن المكره على الحضور هناك، وأما القتل فلا يباح بالإكراه، بل يأثم المكره على المأمور به بالإجماع.
  • قال ابن حجر: وقال آخرون: إذا بغت طائفة على الإمام فامتنعت من الواجب عليها ونصبت الحرب وجب قتالها، وكذلك لو تحاربت طائفتان وجب على كل قادر الأخذ على يد المخطئ ونصر المصيب، وهذا قول الجمهور، وفصل آخرون، فقالوا: كل قتال وقع بين طائفتين من المسلمين حيث لا إمام للجماعة فالقتال حينئذ ممنوع، وتنزل الأحاديث التي في هذا الباب وغيره على ذلك.
  • قال النووي: وقد اختلف العلماء في قتال الفتنة، فقالت طائفة: لا يقاتل في فتن المسلمين، وإن دخلوا عليه بيته، وطلبوا قتله، فلا يجوز له المدافعة عن نفسه؛ لأن الطالب متأول، وهذا مذهب أبي بكرة الصحابي رضي الله عنه وغيره، وقال ابن عمر وعمران بن الحصين رضي الله عنهم وغيرهما: لا يدخل فيها، لكن إن قصد دفع عن نفسه، فهذان المذهبان متفقان على ترك الدخول في جميع فتن الإسلام. ‏وقال معظم الصحابة والتابعين وعامة علماء الإسلام: يجب نصر المحق في الفتن، والقيام معه بمقاتلة الباغين كما قال تعالى: {‌فَقَاتِلُوا ‌الَّتِي تَبْغِي حَتَّى تَفِيءَ إِلَى أَمْرِ اللَّهِ...} الآية، وهذا هو الصحيح، وتتأول الأحاديث على من لم يظهر له المحق، أو على طائفتين ظالمتين لا تأويل لواحدة منهما.

Mada

Ripoti kosa

Zaidi