Hadithi
Adabu za kuvaa.
Chanzo: HadeethEnc.com, Kiswahili v1.18.0
matokeo 7
- 2985
“Msivae hariri wala dibaji (Sufi) wala msinywe katika vyombo vya dhahabu au vya fedha, wala msile katika vyombo vilivyotengenezwa kwa dhahabu na fedha, kwani ni vyao (Makafiri) katika dunia na sisi ni vyetu Akhera
SahihiWamekubaliana Bukhari na Muslim juu ya usahihi wake - 2986
Atakayevaa hariri duniani hatoivaa Akhera
SahihiWamekubaliana Bukhari na Muslim juu ya usahihi wake - 3356
Mtakapo vaa, na mtakapo tawadha, basi anzeni na kuliani kwenu
SahihiImepokelewa na Ibnu Maajah - Imepokelewa na Imamu Tirmidhiy - Imepokelewa na Abuu Daud - Imepokelewa na Ahmad - 4964
Kikoi cha muislamu kifikie nusu ya muundi, na wala hakuna tabu wala hakuna ubaya kikiwa kati yake na kati ya fundo mbili za miguu, kitakachokuwa chini ya fundo mbili basi hicho ni motoni, na atakayeburuza kikoi chake kwa kiburi hatomtazama Mwenyezi Mungu
SahihiImepokelewa na Abu Daud, Ibn Majah na Ahmad - 5370
Hamtazami Mwenyezi Mungu mwenye kuburuza nguo yake kwa kiburi
SahihiWamekubaliana Bukhari na Muslim juu ya usahihi wake - 8904
Asiangalie mwanaume katika uchi wa mwanaume mwenzie, wala mwanamke kutazama uchi wa mwanamke mwenzie
SahihiImepokelewa Imamu Muslim - 65553
Vaeni katika nguo zenu nguo nyeupe, kwani hizo ni katika nguo zenu bora, na wavisheni kwazo maiti wenu
SahihiImepokelewa na Abu Daud, Tirmidhiy na Ibn Majah