يس

Yasin

aya 83Ya MakkaJuzuu 22

Mahmoud Khalil Al-HussaryHafswi kutoka kwa Aswim - Murattal

Mipangilio ya kusoma

Mwongozo wa rangi za tajwidi

Majina, mifano na mitindo tofauti ya mistari ya chini hutambulisha hukumu, pamoja na rangi. Mifano imechukuliwa kutoka maandishi ya Qur'ani yaliyochapishwa.

Ghunna
وَمِمَّا2:3
Kundi la Ikhfaa
يُنفِقُونَ2:3
Kundi la Idghaam
هُدًى لِّلْمُتَّقِينَ2:2
Iqlaab
أَلِيمٌۢ بِمَا2:10
Qalqala
رَزَقْنَـٰهُمْ2:3
Madd: harakati 2
ٱلرَّحْمَـٰنِ1:1
Madd: harakati 2, 4 au 6
ٱلرَّحِيمِ1:1
Madd: harakati 4 au 5
بِمَآ2:4
Madd: harakati 6
ٱلضَّآلِّينَ1:7
Hamzatul wasli
ٱللَّهِ1:1
Lam shamsiyya
ٱلرَّحْمَـٰنِ1:1
Herufi zisizotamkwa
ٱلصَّلَوٰةَ2:3

Alama za tajwidi: cpfair/quran-tajweed (CC BY 4.0), zimetokana na ReciteQuran.com na misahafu ya tajwidi ya Dar al-Maarifah; nafasi zake zimeoanishwa na maandishi ya sasa ya Tanzil.

Utangulizi wa sura: Tafsir ya As-Sa'di (Kiarabu)

تفسير سورة يس

[وهي] مكية

بسم الله الرحمن الرحيم

Tafsir ya As-Sa'di, Kiarabu v1.0.0, QuranEnc.com

بِسْمِ ٱللَّهِ ٱلرَّحْمَـٰنِ ٱلرَّحِيمِ

Tafsiri ya Kiswahili - Kituo cha Tafsiri cha Rowwad. Toleo: 1.0.5. Ilisasishwa mwisho: 2025-12-17. QuranEnc.com

  1. 1

    يسٓ

    Ya Sin.[1]

    Tanbihi

    [1] Herufi hizi "Ya, Sin" na herufi nyinginezo za mkato zilizo mwanzoni mwa sura mbalimbali zinaonyesha hali ya ushindi wa Qur-ani. Kwani, washirikina walipewa changamoto kwayo, lakini wakashindwa na hawakuweza kuipinga, ilhali inajumuisha herufi hizi zinazounda lugha ya Kiarabu. Kwa hivyo, kutoweza kwa Waarabu kuleta kitu kama hicho - ingawa walikuwa ndio watu wenye ufasaha zaidi - kunaonyesha kwamba Qur-ani ni ufunuo (wahyi) kutoka kwa Mwenyezi Mungu.

    Chaguo za aya
    Fungua ukurasa wa aya 1 Kagua kisomo changu: Majaribio
    Dokezo la faragha
  2. 2

    وَٱلْقُرْءَانِ ٱلْحَكِيمِ

    (Ninaapa) kwa Qur-ani yenye hekima!

    Chaguo za aya
    Fungua ukurasa wa aya 2 Kagua kisomo changu: Majaribio
    Dokezo la faragha
  3. 3

    إِنَّكَ لَمِنَ ٱلْمُرْسَلِينَ

    Hakika wewe ni miongoni mwa waliotumwa.

    Chaguo za aya
    Fungua ukurasa wa aya 3 Kagua kisomo changu: Majaribio
    Dokezo la faragha
  4. 4

    عَلَىٰ صِرَٰطٍ مُّسْتَقِيمٍ

    Juu ya njia iliyonyooka.

    Chaguo za aya
    Fungua ukurasa wa aya 4 Kagua kisomo changu: Majaribio
    Dokezo la faragha
  5. 5

    تَنزِيلَ ٱلْعَزِيزِ ٱلرَّحِيمِ

    Uteremsho wa Mwenye nguvu, Mwingi wa kurehemu.

    Chaguo za aya
    Fungua ukurasa wa aya 5 Kagua kisomo changu: Majaribio
    Dokezo la faragha
  6. 6

    لِتُنذِرَ قَوْمًا مَّآ أُنذِرَ ءَابَآؤُهُمْ فَهُمْ غَـٰفِلُونَ

    Ili uwaonye watu ambao baba zao hawakuonywa, basi wao wamekuwa wenye kughafilika.

    Chaguo za aya
    Fungua ukurasa wa aya 6 Kagua kisomo changu: Majaribio
    Dokezo la faragha
  7. 7

    لَقَدْ حَقَّ ٱلْقَوْلُ عَلَىٰٓ أَكْثَرِهِمْ فَهُمْ لَا يُؤْمِنُونَ

    Bila ya shaka kauli imekwisha thibiti juu ya wengi katika wao, kwa hivyo hawaamini.

    Chaguo za aya
    Fungua ukurasa wa aya 7 Kagua kisomo changu: Majaribio
    Dokezo la faragha
  8. 8

    إِنَّا جَعَلْنَا فِىٓ أَعْنَـٰقِهِمْ أَغْلَـٰلًا فَهِىَ إِلَى ٱلْأَذْقَانِ فَهُم مُّقْمَحُونَ

    Tumeweka makongwa shingoni mwao, yakawafika videvuni. Kwa hivyo vichwa vyao viko juu tu.

    Chaguo za aya
    Fungua ukurasa wa aya 8 Kagua kisomo changu: Majaribio
    Dokezo la faragha
  9. 9

    وَجَعَلْنَا مِنۢ بَيْنِ أَيْدِيهِمْ سَدًّا وَمِنْ خَلْفِهِمْ سَدًّا فَأَغْشَيْنَـٰهُمْ فَهُمْ لَا يُبْصِرُونَ

    Tumeweka kizuizi mbele yao, na kizuizi nyuma yao. Na tumewafunika macho yao, kwa hivyo hawaoni.

    Chaguo za aya
    Fungua ukurasa wa aya 9 Kagua kisomo changu: Majaribio
    Dokezo la faragha
  10. 10

    وَسَوَآءٌ عَلَيْهِمْ ءَأَنذَرْتَهُمْ أَمْ لَمْ تُنذِرْهُمْ لَا يُؤْمِنُونَ

    Ni sawa sawa kwao ukiwaonya au usiwaonye, hawataamini.

    Chaguo za aya
    Fungua ukurasa wa aya 10 Kagua kisomo changu: Majaribio
    Dokezo la faragha
  11. 11

    إِنَّمَا تُنذِرُ مَنِ ٱتَّبَعَ ٱلذِّكْرَ وَخَشِىَ ٱلرَّحْمَـٰنَ بِٱلْغَيْبِ ۖ فَبَشِّرْهُ بِمَغْفِرَةٍ وَأَجْرٍ كَرِيمٍ

    Hakika wewe unamwonya mwenye kufuata ukumbusho, na akamcha Arrahman (Mwingi wa rehema), kwa ghaibu. Basi mbashirie huyo msamaha na ujira mwema.

    Chaguo za aya
    Fungua ukurasa wa aya 11 Kagua kisomo changu: Majaribio
    Dokezo la faragha
  12. 12

    إِنَّا نَحْنُ نُحْىِ ٱلْمَوْتَىٰ وَنَكْتُبُ مَا قَدَّمُوا۟ وَءَاثَـٰرَهُمْ ۚ وَكُلَّ شَىْءٍ أَحْصَيْنَـٰهُ فِىٓ إِمَامٍ مُّبِينٍ

    Hakika Sisi tunawafufua wafu na tunayaandika wanayoyatanguliza, na wanayoyaacha nyuma. Na kila kitu tumekihifadhi katika daftari la asili lenye kubainisha.

    Chaguo za aya
    Fungua ukurasa wa aya 12 Kagua kisomo changu: Majaribio
    Dokezo la faragha
  13. 13

    وَٱضْرِبْ لَهُم مَّثَلًا أَصْحَـٰبَ ٱلْقَرْيَةِ إِذْ جَآءَهَا ٱلْمُرْسَلُونَ

    Na wapigie mfano wa wakazi wa mji walipojiwa na Mitume.

    Chaguo za aya
    Fungua ukurasa wa aya 13 Kagua kisomo changu: Majaribio
    Dokezo la faragha
  14. 14

    إِذْ أَرْسَلْنَآ إِلَيْهِمُ ٱثْنَيْنِ فَكَذَّبُوهُمَا فَعَزَّزْنَا بِثَالِثٍ فَقَالُوٓا۟ إِنَّآ إِلَيْكُم مُّرْسَلُونَ

    Tulipowatumia wawili, wakawakanusha. Basi tukawazidishia nguvu kwa mwingine wa tatu. Wakasema: "Hakika sisi tumetumwa kwenu."

    Chaguo za aya
    Fungua ukurasa wa aya 14 Kagua kisomo changu: Majaribio
    Dokezo la faragha
  15. 15

    قَالُوا۟ مَآ أَنتُمْ إِلَّا بَشَرٌ مِّثْلُنَا وَمَآ أَنزَلَ ٱلرَّحْمَـٰنُ مِن شَىْءٍ إِنْ أَنتُمْ إِلَّا تَكْذِبُونَ

    Wakasema: "Nyinyi si chochote ila ni watu kama sisi. Na Mwingi wa Rehema hakuteremsha kitu. Nyinyi mnasema uongo tu."

    Chaguo za aya
    Fungua ukurasa wa aya 15 Kagua kisomo changu: Majaribio
    Dokezo la faragha
  16. 16

    قَالُوا۟ رَبُّنَا يَعْلَمُ إِنَّآ إِلَيْكُمْ لَمُرْسَلُونَ

    Wakasema: "Mola wetu Mlezi anajua kwamba hakika sisi tumetumwa kwenu."

    Chaguo za aya
    Fungua ukurasa wa aya 16 Kagua kisomo changu: Majaribio
    Dokezo la faragha
  17. 17

    وَمَا عَلَيْنَآ إِلَّا ٱلْبَلَـٰغُ ٱلْمُبِينُ

    Wala si juu yetu ila kufikisha ujumbe ulio wazi."

    Chaguo za aya
    Fungua ukurasa wa aya 17 Kagua kisomo changu: Majaribio
    Dokezo la faragha
  18. 18

    قَالُوٓا۟ إِنَّا تَطَيَّرْنَا بِكُمْ ۖ لَئِن لَّمْ تَنتَهُوا۟ لَنَرْجُمَنَّكُمْ وَلَيَمَسَّنَّكُم مِّنَّا عَذَابٌ أَلِيمٌ

    Wakasema: "Sisi hakika sisi tunaona mkosi kwenu. Ikiwa hamtaacha basi kwa yakini tutakupigeni mawe, na mtapata adhabu chungu kutoka kwetu."

    Chaguo za aya
    Fungua ukurasa wa aya 18 Kagua kisomo changu: Majaribio
    Dokezo la faragha
  19. 19

    قَالُوا۟ طَـٰٓئِرُكُم مَّعَكُمْ ۚ أَئِن ذُكِّرْتُم ۚ بَلْ أَنتُمْ قَوْمٌ مُّسْرِفُونَ

    Wakasema: "Mkosi wenu mnao wenyewe! Je! Ni kwa kuwa mnakumbushwa? Ama nyinyi ni watu waliopindukia mipaka."

    Chaguo za aya
    Fungua ukurasa wa aya 19 Kagua kisomo changu: Majaribio
    Dokezo la faragha
  20. 20

    وَجَآءَ مِنْ أَقْصَا ٱلْمَدِينَةِ رَجُلٌ يَسْعَىٰ قَالَ يَـٰقَوْمِ ٱتَّبِعُوا۟ ٱلْمُرْسَلِينَ

    Na akaja mtu mbio kutokea upande wa mbali wa mjini, akasema: "Enyi watu wangu! Wafuateni hawa waliotumwa.

    Chaguo za aya
    Fungua ukurasa wa aya 20 Kagua kisomo changu: Majaribio
    Dokezo la faragha
  21. 21

    ٱتَّبِعُوا۟ مَن لَّا يَسْـَٔلُكُمْ أَجْرًا وَهُم مُّهْتَدُونَ

    Wafuateni ambao hawakutakini ujira, hali ya kuwa wenyewe wameongoka.

    Chaguo za aya
    Fungua ukurasa wa aya 21 Kagua kisomo changu: Majaribio
    Dokezo la faragha
  22. 22

    وَمَا لِىَ لَآ أَعْبُدُ ٱلَّذِى فَطَرَنِى وَإِلَيْهِ تُرْجَعُونَ

    Na kwa nini nisimuabudu yule aliyeniumba na kwake nitarejeshwa?

    Chaguo za aya
    Fungua ukurasa wa aya 22 Kagua kisomo changu: Majaribio
    Dokezo la faragha
  23. 23

    ءَأَتَّخِذُ مِن دُونِهِۦٓ ءَالِهَةً إِن يُرِدْنِ ٱلرَّحْمَـٰنُ بِضُرٍّ لَّا تُغْنِ عَنِّى شَفَـٰعَتُهُمْ شَيْـًٔا وَلَا يُنقِذُونِ

    Je, niishike miungu mingine badala yake? Arrahmani (Mwingi wa Rehema) akinitakia madhara uombezi wa hao hautanifaa kitu, wala hawataniokoa.

    Chaguo za aya
    Fungua ukurasa wa aya 23 Kagua kisomo changu: Majaribio
    Dokezo la faragha
  24. 24

    إِنِّىٓ إِذًا لَّفِى ضَلَـٰلٍ مُّبِينٍ

    Basi hakika mimi hapo nitakuwa katika upotovu ulio dhahiri.

    Chaguo za aya
    Fungua ukurasa wa aya 24 Kagua kisomo changu: Majaribio
    Dokezo la faragha
  25. 25

    إِنِّىٓ ءَامَنتُ بِرَبِّكُمْ فَٱسْمَعُونِ

    Hakika mimi nimemuamini Mola wenu Mlezi, basi nisikilizeni!"

    Chaguo za aya
    Fungua ukurasa wa aya 25 Kagua kisomo changu: Majaribio
    Dokezo la faragha
  26. 26

    قِيلَ ٱدْخُلِ ٱلْجَنَّةَ ۖ قَالَ يَـٰلَيْتَ قَوْمِى يَعْلَمُونَ

    Akaambiwa: "Ingia Peponi!" Akasema: "Laiti kuwa watu wangu wangelijua.

    Chaguo za aya
    Fungua ukurasa wa aya 26 Kagua kisomo changu: Majaribio
    Dokezo la faragha
  27. 27

    بِمَا غَفَرَ لِى رَبِّى وَجَعَلَنِى مِنَ ٱلْمُكْرَمِينَ

    Jinsi Mola wangu Mlezi alivyonisamehe, na akanifanya miongoni mwa walioheshimiwa."

    Chaguo za aya
    Fungua ukurasa wa aya 27 Kagua kisomo changu: Majaribio
    Dokezo la faragha
  28. 28

    ۞ وَمَآ أَنزَلْنَا عَلَىٰ قَوْمِهِۦ مِنۢ بَعْدِهِۦ مِن جُندٍ مِّنَ ٱلسَّمَآءِ وَمَا كُنَّا مُنزِلِينَ

    Na hatukuwateremshia kaumu yake baada yake jeshi kutoka mbinguni, wala si wenye kuteremsha.

    Chaguo za aya
    Fungua ukurasa wa aya 28 Kagua kisomo changu: Majaribio
    Dokezo la faragha
  29. 29

    إِن كَانَتْ إِلَّا صَيْحَةً وَٰحِدَةً فَإِذَا هُمْ خَـٰمِدُونَ

    Haukuwa ila ukelele mmoja tu, na mara walizimwa!

    Chaguo za aya
    Fungua ukurasa wa aya 29 Kagua kisomo changu: Majaribio
    Dokezo la faragha
  30. 30

    يَـٰحَسْرَةً عَلَى ٱلْعِبَادِ ۚ مَا يَأْتِيهِم مِّن رَّسُولٍ إِلَّا كَانُوا۟ بِهِۦ يَسْتَهْزِءُونَ

    Nawasikitikia waja wangu. Hawajii Mtume ila wao humkejeli.

    Chaguo za aya
    Fungua ukurasa wa aya 30 Kagua kisomo changu: Majaribio
    Dokezo la faragha
  31. 31

    أَلَمْ يَرَوْا۟ كَمْ أَهْلَكْنَا قَبْلَهُم مِّنَ ٱلْقُرُونِ أَنَّهُمْ إِلَيْهِمْ لَا يَرْجِعُونَ

    Je, hawaoni umma ngapi tulizoziangamiza kabla yao? Hakika hao hawarejei tena kwao.

    Chaguo za aya
    Fungua ukurasa wa aya 31 Kagua kisomo changu: Majaribio
    Dokezo la faragha
  32. 32

    وَإِن كُلٌّ لَّمَّا جَمِيعٌ لَّدَيْنَا مُحْضَرُونَ

    Na hapana mmoja ila wote watakusanywa waletwe mbele yetu.

    Chaguo za aya
    Fungua ukurasa wa aya 32 Kagua kisomo changu: Majaribio
    Dokezo la faragha
  33. 33

    وَءَايَةٌ لَّهُمُ ٱلْأَرْضُ ٱلْمَيْتَةُ أَحْيَيْنَـٰهَا وَأَخْرَجْنَا مِنْهَا حَبًّا فَمِنْهُ يَأْكُلُونَ

    Na Ishara hiyo kwao ni ardhi iliyokufa, nasi tukaifufua, na tukatoa ndani yake nafaka, wakawa wanakula katika hizo!

    Chaguo za aya
    Fungua ukurasa wa aya 33 Kagua kisomo changu: Majaribio
    Dokezo la faragha
  34. 34

    وَجَعَلْنَا فِيهَا جَنَّـٰتٍ مِّن نَّخِيلٍ وَأَعْنَـٰبٍ وَفَجَّرْنَا فِيهَا مِنَ ٱلْعُيُونِ

    Na tukafanya ndani yake mabustani ya mitende na mizabibu, na tukatimbua chemichemi ndani yake.

    Chaguo za aya
    Fungua ukurasa wa aya 34 Kagua kisomo changu: Majaribio
    Dokezo la faragha
  35. 35

    لِيَأْكُلُوا۟ مِن ثَمَرِهِۦ وَمَا عَمِلَتْهُ أَيْدِيهِمْ ۖ أَفَلَا يَشْكُرُونَ

    Ili wale katika matunda yake, na hayo hayakufanywa na mikono yao! Basi je, hawashukuru?

    Chaguo za aya
    Fungua ukurasa wa aya 35 Kagua kisomo changu: Majaribio
    Dokezo la faragha
  36. 36

    سُبْحَـٰنَ ٱلَّذِى خَلَقَ ٱلْأَزْوَٰجَ كُلَّهَا مِمَّا تُنۢبِتُ ٱلْأَرْضُ وَمِنْ أَنفُسِهِمْ وَمِمَّا لَا يَعْلَمُونَ

    Ametakasika yule aliyeumba dume na jike vyote katika vinavyomea katika ardhi na katika nafsi zao, na katika wasivyovijua.

    Chaguo za aya
    Fungua ukurasa wa aya 36 Kagua kisomo changu: Majaribio
    Dokezo la faragha
  37. 37

    وَءَايَةٌ لَّهُمُ ٱلَّيْلُ نَسْلَخُ مِنْهُ ٱلنَّهَارَ فَإِذَا هُم مُّظْلِمُونَ

    Na usiku ni Ishara kwao. Tunauvua humo mchana, mara wao wanakuwa gizani.

    Chaguo za aya
    Fungua ukurasa wa aya 37 Kagua kisomo changu: Majaribio
    Dokezo la faragha
  38. 38

    وَٱلشَّمْسُ تَجْرِى لِمُسْتَقَرٍّ لَّهَا ۚ ذَٰلِكَ تَقْدِيرُ ٱلْعَزِيزِ ٱلْعَلِيمِ

    Na jua linakwenda kwa kiwango chake. Hayo ni makadirio ya Mwenye nguvu, Mwenye kujua vyema.

    Chaguo za aya
    Fungua ukurasa wa aya 38 Kagua kisomo changu: Majaribio
    Dokezo la faragha
  39. 39

    وَٱلْقَمَرَ قَدَّرْنَـٰهُ مَنَازِلَ حَتَّىٰ عَادَ كَٱلْعُرْجُونِ ٱلْقَدِيمِ

    Na mwezi tumeupimia vituo, mpaka unakuwa kama karara kongwe.

    Chaguo za aya
    Fungua ukurasa wa aya 39 Kagua kisomo changu: Majaribio
    Dokezo la faragha
  40. 40

    لَا ٱلشَّمْسُ يَنۢبَغِى لَهَآ أَن تُدْرِكَ ٱلْقَمَرَ وَلَا ٱلَّيْلُ سَابِقُ ٱلنَّهَارِ ۚ وَكُلٌّ فِى فَلَكٍ يَسْبَحُونَ

    Haliwi jua kuufikia mwezi, wala usiku kuupita mchana. Na vyote vinaogelea katika njia zao.

    Chaguo za aya
    Fungua ukurasa wa aya 40 Kagua kisomo changu: Majaribio
    Dokezo la faragha
  41. 41

    وَءَايَةٌ لَّهُمْ أَنَّا حَمَلْنَا ذُرِّيَّتَهُمْ فِى ٱلْفُلْكِ ٱلْمَشْحُونِ

    Na ni Ishara kwao kwamba Sisi tuliwapakia dhuria zao katika jahazi lililosheheni.

    Chaguo za aya
    Fungua ukurasa wa aya 41 Kagua kisomo changu: Majaribio
    Dokezo la faragha
  42. 42

    وَخَلَقْنَا لَهُم مِّن مِّثْلِهِۦ مَا يَرْكَبُونَ

    Na tukawaumbia kutoka mfano wake wanavyovipanda.

    Chaguo za aya
    Fungua ukurasa wa aya 42 Kagua kisomo changu: Majaribio
    Dokezo la faragha
  43. 43

    وَإِن نَّشَأْ نُغْرِقْهُمْ فَلَا صَرِيخَ لَهُمْ وَلَا هُمْ يُنقَذُونَ

    Na tukitaka, tunawazamisha, wala hapana wa kuwasaidia, wala hawaokolewi.

    Chaguo za aya
    Fungua ukurasa wa aya 43 Kagua kisomo changu: Majaribio
    Dokezo la faragha
  44. 44

    إِلَّا رَحْمَةً مِّنَّا وَمَتَـٰعًا إِلَىٰ حِينٍ

    Isipokuwa kwa rehema zitokazo kwetu na starehe kwa muda.

    Chaguo za aya
    Fungua ukurasa wa aya 44 Kagua kisomo changu: Majaribio
    Dokezo la faragha
  45. 45

    وَإِذَا قِيلَ لَهُمُ ٱتَّقُوا۟ مَا بَيْنَ أَيْدِيكُمْ وَمَا خَلْفَكُمْ لَعَلَّكُمْ تُرْحَمُونَ

    Na wanapoambiwa: Jilindeni kutokana na yaliyoko mbele yenu na yaliyoko nyuma yenu, ili mpate kurehemewa...

    Chaguo za aya
    Fungua ukurasa wa aya 45 Kagua kisomo changu: Majaribio
    Dokezo la faragha
  46. 46

    وَمَا تَأْتِيهِم مِّنْ ءَايَةٍ مِّنْ ءَايَـٰتِ رَبِّهِمْ إِلَّا كَانُوا۟ عَنْهَا مُعْرِضِينَ

    Na haiwafikii Ishara yoyote katika Ishara za Mola wao Mlezi isipokuwa wao huwa ni wenye kuipa mgongo.

    Chaguo za aya
    Fungua ukurasa wa aya 46 Kagua kisomo changu: Majaribio
    Dokezo la faragha
  47. 47

    وَإِذَا قِيلَ لَهُمْ أَنفِقُوا۟ مِمَّا رَزَقَكُمُ ٱللَّهُ قَالَ ٱلَّذِينَ كَفَرُوا۟ لِلَّذِينَ ءَامَنُوٓا۟ أَنُطْعِمُ مَن لَّوْ يَشَآءُ ٱللَّهُ أَطْعَمَهُۥٓ إِنْ أَنتُمْ إِلَّا فِى ضَلَـٰلٍ مُّبِينٍ

    Na wanapoambiwa: "Toeni katika aliyokupeni Mwenyezi Mungu", wale waliokufuru huwaambia wale walioamini: Je, tuwalishe wale ambao Mwenyezi Mungu angependa angeliwalisha mwenyewe? Nyinyi hammo isipokuwa katika upotovu ulio dhahiri.

    Chaguo za aya
    Fungua ukurasa wa aya 47 Kagua kisomo changu: Majaribio
    Dokezo la faragha
  48. 48

    وَيَقُولُونَ مَتَىٰ هَـٰذَا ٱلْوَعْدُ إِن كُنتُمْ صَـٰدِقِينَ

    Na wanasema: Ahadi hii itatokea lini, ikiwa nyinyi ni wakweli?

    Chaguo za aya
    Fungua ukurasa wa aya 48 Kagua kisomo changu: Majaribio
    Dokezo la faragha
  49. 49

    مَا يَنظُرُونَ إِلَّا صَيْحَةً وَٰحِدَةً تَأْخُذُهُمْ وَهُمْ يَخِصِّمُونَ

    Hawangojei isipokuwa ukelele mmoja tu utakaowachukua nao wamo kuzozana.

    Chaguo za aya
    Fungua ukurasa wa aya 49 Kagua kisomo changu: Majaribio
    Dokezo la faragha
  50. 50

    فَلَا يَسْتَطِيعُونَ تَوْصِيَةً وَلَآ إِلَىٰٓ أَهْلِهِمْ يَرْجِعُونَ

    Basi hawataweza kuusia, wala kwa watu wao hawarejei.

    Chaguo za aya
    Fungua ukurasa wa aya 50 Kagua kisomo changu: Majaribio
    Dokezo la faragha
  51. 51

    وَنُفِخَ فِى ٱلصُّورِ فَإِذَا هُم مِّنَ ٱلْأَجْدَاثِ إِلَىٰ رَبِّهِمْ يَنسِلُونَ

    Na litapulizwa baragumu, mara watatoka makaburini wakikimbilia kwa Mola wao Mlezi.

    Chaguo za aya
    Fungua ukurasa wa aya 51 Kagua kisomo changu: Majaribio
    Dokezo la faragha
  52. 52

    قَالُوا۟ يَـٰوَيْلَنَا مَنۢ بَعَثَنَا مِن مَّرْقَدِنَا ۜ ۗ هَـٰذَا مَا وَعَدَ ٱلرَّحْمَـٰنُ وَصَدَقَ ٱلْمُرْسَلُونَ

    Watasema: Ole wetu! Ni nani aliyetufufua kwenye malazi yetu? Haya ndiyo aliyoyaahidi Mwingi wa Rehema na wakasema kweli Mitume.

    Chaguo za aya
    Fungua ukurasa wa aya 52 Kagua kisomo changu: Majaribio
    Dokezo la faragha
  53. 53

    إِن كَانَتْ إِلَّا صَيْحَةً وَٰحِدَةً فَإِذَا هُمْ جَمِيعٌ لَّدَيْنَا مُحْضَرُونَ

    Haitakuwa isipokuwa ukelele mmoja tu, mara wote watahudhurishwa mbele yetu.

    Chaguo za aya
    Fungua ukurasa wa aya 53 Kagua kisomo changu: Majaribio
    Dokezo la faragha
  54. 54

    فَٱلْيَوْمَ لَا تُظْلَمُ نَفْسٌ شَيْـًٔا وَلَا تُجْزَوْنَ إِلَّا مَا كُنتُمْ تَعْمَلُونَ

    Basi leo nafsi yoyote haitadhulumiwa kitu, wala hamtalipwa isipokuwa yale mliyokuwa mkiyatenda.

    Chaguo za aya
    Fungua ukurasa wa aya 54 Kagua kisomo changu: Majaribio
    Dokezo la faragha
  55. 55

    إِنَّ أَصْحَـٰبَ ٱلْجَنَّةِ ٱلْيَوْمَ فِى شُغُلٍ فَـٰكِهُونَ

    Hakika watu wa Bustani ya mbinguni leo wamo shughulini, wamefurahi.

    Chaguo za aya
    Fungua ukurasa wa aya 55 Kagua kisomo changu: Majaribio
    Dokezo la faragha
  56. 56

    هُمْ وَأَزْوَٰجُهُمْ فِى ظِلَـٰلٍ عَلَى ٱلْأَرَآئِكِ مُتَّكِـُٔونَ

    Wao na wake zao wamo katika vivuli wameegemea juu ya viti vya kifahari.

    Chaguo za aya
    Fungua ukurasa wa aya 56 Kagua kisomo changu: Majaribio
    Dokezo la faragha
  57. 57

    لَهُمْ فِيهَا فَـٰكِهَةٌ وَلَهُم مَّا يَدَّعُونَ

    Watapata humo kila namna ya matunda na watapata kila watakachokitaka.

    Chaguo za aya
    Fungua ukurasa wa aya 57 Kagua kisomo changu: Majaribio
    Dokezo la faragha
  58. 58

    سَلَـٰمٌ قَوْلًا مِّن رَّبٍّ رَّحِيمٍ

    "Salama!" Hiyo ndiyo kauli itokayo kwa Mola Mlezi Mwenye kurehemu.

    Chaguo za aya
    Fungua ukurasa wa aya 58 Kagua kisomo changu: Majaribio
    Dokezo la faragha
  59. 59

    وَٱمْتَـٰزُوا۟ ٱلْيَوْمَ أَيُّهَا ٱلْمُجْرِمُونَ

    Na enyi wakosefu! Jitengeni leo!

    Chaguo za aya
    Fungua ukurasa wa aya 59 Kagua kisomo changu: Majaribio
    Dokezo la faragha
  60. 60

    ۞ أَلَمْ أَعْهَدْ إِلَيْكُمْ يَـٰبَنِىٓ ءَادَمَ أَن لَّا تَعْبُدُوا۟ ٱلشَّيْطَـٰنَ ۖ إِنَّهُۥ لَكُمْ عَدُوٌّ مُّبِينٌ

    Je, sikuagana nanyi, enyi wanadamu, kuwa msimuabudu Shetani? Hakika yeye ni adui dhahiri kwenu.

    Chaguo za aya
    Fungua ukurasa wa aya 60 Kagua kisomo changu: Majaribio
    Dokezo la faragha
  61. 61

    وَأَنِ ٱعْبُدُونِى ۚ هَـٰذَا صِرَٰطٌ مُّسْتَقِيمٌ

    Na ya kwamba mniabudu Mimi? Hii ndiyo Njia iliyonyooka.

    Chaguo za aya
    Fungua ukurasa wa aya 61 Kagua kisomo changu: Majaribio
    Dokezo la faragha
  62. 62

    وَلَقَدْ أَضَلَّ مِنكُمْ جِبِلًّا كَثِيرًا ۖ أَفَلَمْ تَكُونُوا۟ تَعْقِلُونَ

    Na bila ya shaka yeye amekwisha lipoteza kundi kubwa miongoni mwenu. Je, hamkuwa mkifikiri?

    Chaguo za aya
    Fungua ukurasa wa aya 62 Kagua kisomo changu: Majaribio
    Dokezo la faragha
  63. 63

    هَـٰذِهِۦ جَهَنَّمُ ٱلَّتِى كُنتُمْ تُوعَدُونَ

    Hii basi ndiyo Jahannamu mliyokuwa mkiahidiwa.

    Chaguo za aya
    Fungua ukurasa wa aya 63 Kagua kisomo changu: Majaribio
    Dokezo la faragha
  64. 64

    ٱصْلَوْهَا ٱلْيَوْمَ بِمَا كُنتُمْ تَكْفُرُونَ

    Ingieni humo leo kwa vile mlivyokuwa mkikufuru.

    Chaguo za aya
    Fungua ukurasa wa aya 64 Kagua kisomo changu: Majaribio
    Dokezo la faragha
  65. 65

    ٱلْيَوْمَ نَخْتِمُ عَلَىٰٓ أَفْوَٰهِهِمْ وَتُكَلِّمُنَآ أَيْدِيهِمْ وَتَشْهَدُ أَرْجُلُهُم بِمَا كَانُوا۟ يَكْسِبُونَ

    Leo tunaviziba vinywa vyao, na iseme nasi mikono yao, na itoe ushahidi miguu yao kwa waliyokuwa wakiyachuma.

    Chaguo za aya
    Fungua ukurasa wa aya 65 Kagua kisomo changu: Majaribio
    Dokezo la faragha
  66. 66

    وَلَوْ نَشَآءُ لَطَمَسْنَا عَلَىٰٓ أَعْيُنِهِمْ فَٱسْتَبَقُوا۟ ٱلصِّرَٰطَ فَأَنَّىٰ يُبْصِرُونَ

    Na tungelipenda, tungeliyafutilia mbali macho yao, wakawa wanaiwania njia. Lakini wangeionaje?

    Chaguo za aya
    Fungua ukurasa wa aya 66 Kagua kisomo changu: Majaribio
    Dokezo la faragha
  67. 67

    وَلَوْ نَشَآءُ لَمَسَخْنَـٰهُمْ عَلَىٰ مَكَانَتِهِمْ فَمَا ٱسْتَطَـٰعُوا۟ مُضِيًّا وَلَا يَرْجِعُونَ

    Na tungelitaka, tungewageuza sura hapo hapo walipo, basi wasingeweza kwenda wala kurudi.

    Chaguo za aya
    Fungua ukurasa wa aya 67 Kagua kisomo changu: Majaribio
    Dokezo la faragha
  68. 68

    وَمَن نُّعَمِّرْهُ نُنَكِّسْهُ فِى ٱلْخَلْقِ ۖ أَفَلَا يَعْقِلُونَ

    Na tunayemzeesha, tunamrudisha nyuma katika umbo. Basi je, hawazingatii?

    Chaguo za aya
    Fungua ukurasa wa aya 68 Kagua kisomo changu: Majaribio
    Dokezo la faragha
  69. 69

    وَمَا عَلَّمْنَـٰهُ ٱلشِّعْرَ وَمَا يَنۢبَغِى لَهُۥٓ ۚ إِنْ هُوَ إِلَّا ذِكْرٌ وَقُرْءَانٌ مُّبِينٌ

    Wala hatukumfundisha (Muhammad) mashairi, wala hayatakikani kwake hayo. Haukuwa huu isipokuwa ni ukumbusho na Qur-ani inayobainisha.

    Chaguo za aya
    Fungua ukurasa wa aya 69 Kagua kisomo changu: Majaribio
    Dokezo la faragha
  70. 70

    لِّيُنذِرَ مَن كَانَ حَيًّا وَيَحِقَّ ٱلْقَوْلُ عَلَى ٱلْكَـٰفِرِينَ

    Ili imwonye aliye hai, na neno litimie juu ya makafiri.

    Chaguo za aya
    Fungua ukurasa wa aya 70 Kagua kisomo changu: Majaribio
    Dokezo la faragha
  71. 71

    أَوَلَمْ يَرَوْا۟ أَنَّا خَلَقْنَا لَهُم مِّمَّا عَمِلَتْ أَيْدِينَآ أَنْعَـٰمًا فَهُمْ لَهَا مَـٰلِكُونَ

    Je, hawaoni kwamba tumewaumbia kutokana na iliyofanya mikono yetu wanyama wa mifugo, na wao wakawa wenye kuwamiliki.

    Chaguo za aya
    Fungua ukurasa wa aya 71 Kagua kisomo changu: Majaribio
    Dokezo la faragha
  72. 72

    وَذَلَّلْنَـٰهَا لَهُمْ فَمِنْهَا رَكُوبُهُمْ وَمِنْهَا يَأْكُلُونَ

    Na Sisi tukawadhalilishia. Basi baadhi yao wako wanaowapanda, na baadhi yao wanawala.

    Chaguo za aya
    Fungua ukurasa wa aya 72 Kagua kisomo changu: Majaribio
    Dokezo la faragha
  73. 73

    وَلَهُمْ فِيهَا مَنَـٰفِعُ وَمَشَارِبُ ۖ أَفَلَا يَشْكُرُونَ

    Na wao wanapata kwao manufaa na vinywaji. Basi je, hawashukuru?

    Chaguo za aya
    Fungua ukurasa wa aya 73 Kagua kisomo changu: Majaribio
    Dokezo la faragha
  74. 74

    وَٱتَّخَذُوا۟ مِن دُونِ ٱللَّهِ ءَالِهَةً لَّعَلَّهُمْ يُنصَرُونَ

    Na wameishika miungu mingine badala ya Mwenyezi Mungu ili ati wapate kusaidiwa!

    Chaguo za aya
    Fungua ukurasa wa aya 74 Kagua kisomo changu: Majaribio
    Dokezo la faragha
  75. 75

    لَا يَسْتَطِيعُونَ نَصْرَهُمْ وَهُمْ لَهُمْ جُندٌ مُّحْضَرُونَ

    Hawataweza kuwasaidia. Bali hao ndio askari wao, watahudhurishwa.

    Chaguo za aya
    Fungua ukurasa wa aya 75 Kagua kisomo changu: Majaribio
    Dokezo la faragha
  76. 76

    فَلَا يَحْزُنكَ قَوْلُهُمْ ۘ إِنَّا نَعْلَمُ مَا يُسِرُّونَ وَمَا يُعْلِنُونَ

    Basi maneno yao yasikuhuzunishe. Hakika Sisi tunayajua wanayoyaweka siri na wanayoyadhihirisha.

    Chaguo za aya
    Fungua ukurasa wa aya 76 Kagua kisomo changu: Majaribio
    Dokezo la faragha
  77. 77

    أَوَلَمْ يَرَ ٱلْإِنسَـٰنُ أَنَّا خَلَقْنَـٰهُ مِن نُّطْفَةٍ فَإِذَا هُوَ خَصِيمٌ مُّبِينٌ

    Kwani mwanadamu haoni ya kwamba Sisi tumemuumba yeye kutokana na tone la manii? Kisha sasa yeye ndiyo amekuwa ndiye mgomvi wa dhahiri!

    Chaguo za aya
    Fungua ukurasa wa aya 77 Kagua kisomo changu: Majaribio
    Dokezo la faragha
  78. 78

    وَضَرَبَ لَنَا مَثَلًا وَنَسِىَ خَلْقَهُۥ ۖ قَالَ مَن يُحْىِ ٱلْعِظَـٰمَ وَهِىَ رَمِيمٌ

    Na akatupigia mfano, na akasahau kuumbwa kwake, akasema: Ni nani huyo atakayeihuisha mifupa nayo imekwisha mung'unyika?

    Chaguo za aya
    Fungua ukurasa wa aya 78 Kagua kisomo changu: Majaribio
    Dokezo la faragha
  79. 79

    قُلْ يُحْيِيهَا ٱلَّذِىٓ أَنشَأَهَآ أَوَّلَ مَرَّةٍ ۖ وَهُوَ بِكُلِّ خَلْقٍ عَلِيمٌ

    Sema: Ataihuisha huyo huyo aliyeiumba hapo mara ya mwanzo. Na Yeye ni Mjuzi wa kila kuumba.

    Chaguo za aya
    Fungua ukurasa wa aya 79 Kagua kisomo changu: Majaribio
    Dokezo la faragha
  80. 80

    ٱلَّذِى جَعَلَ لَكُم مِّنَ ٱلشَّجَرِ ٱلْأَخْضَرِ نَارًا فَإِذَآ أَنتُم مِّنْهُ تُوقِدُونَ

    Aliyekujaalieni kupata moto kutokana na mti wa kijani nanyi mkawa kwa huo mnawasha.

    Chaguo za aya
    Fungua ukurasa wa aya 80 Kagua kisomo changu: Majaribio
    Dokezo la faragha
  81. 81

    أَوَلَيْسَ ٱلَّذِى خَلَقَ ٱلسَّمَـٰوَٰتِ وَٱلْأَرْضَ بِقَـٰدِرٍ عَلَىٰٓ أَن يَخْلُقَ مِثْلَهُم ۚ بَلَىٰ وَهُوَ ٱلْخَلَّـٰقُ ٱلْعَلِيمُ

    Kwani aliyeziumba mbingu na ardhi hawezi kuwaumba mfano wao? Kwani! Naye ndiye Muumbaji Mkuu, Mjuzi mno.

    Chaguo za aya
    Fungua ukurasa wa aya 81 Kagua kisomo changu: Majaribio
    Dokezo la faragha
  82. 82

    إِنَّمَآ أَمْرُهُۥٓ إِذَآ أَرَادَ شَيْـًٔا أَن يَقُولَ لَهُۥ كُن فَيَكُونُ

    Hakika amri yake anapotaka kitu ni kukiambia tu: Kuwa! Na kikawa.

    Chaguo za aya
    Fungua ukurasa wa aya 82 Kagua kisomo changu: Majaribio
    Dokezo la faragha
  83. 83

    فَسُبْحَـٰنَ ٱلَّذِى بِيَدِهِۦ مَلَكُوتُ كُلِّ شَىْءٍ وَإِلَيْهِ تُرْجَعُونَ

    Basi ametakasika yule ambaye mkononi mwake umo Ufalme wa kila kitu; na kwake Yeye mtarejeshwa.

    Chaguo za aya
    Fungua ukurasa wa aya 83 Kagua kisomo changu: Majaribio
    Dokezo la faragha
Hitimisho la sura: Tafsir ya As-Sa'di (Kiarabu)

تم تفسير سورة يس. فلله تعالى الحمدُ كما ينبغي لجلاله، وله الثناء كما يليق بكماله، وله المجد كما تستدعيه عظمته وكبرياؤه، وصلى الله على محمد وسلم.

Tafsir ya As-Sa'di, Kiarabu v1.0.0, QuranEnc.com

Soma tafsir

Sura inayofuataAs-Saffatالصافات

Maandishi ya Qur'ani: Tanzil

Ripoti kosa

Zaidi