Chanzo: HadeethEnc.com, Kiswahili v1.18.0
Matini ya Kiarabu
عَنْ عُمَرَ بْنِ الْخَطَّابِ رضي الله عنه قَالَ: قَالَ رَسُولُ اللهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ: «إِنَّ اللهَ عَزَّ وَجَلَّ يَنْهَاكُمْ أَنْ تَحْلِفُوا بِآبَائِكُمْ»، قَالَ عُمَرُ: فَوَاللهِ مَا حَلَفْتُ بِهَا مُنْذُ سَمِعْتُ رَسُولَ اللهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ نَهَى عَنْهَا ذَاكِرًا وَلَا آثِرًا.
Tafsiri
Imepokewa kutoka kwa Omar Bin Khattwab- Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake- amesema: Amesema Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- "Hakika Mwenyezi Mungu Mtukufu anakukatazeni kuapa kwa baba zenu", akasema Omari: Wallahi sikuwahi kuapa tena kwa kiapo hicho tangu nilipomsikia Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- alipokataza hivyo, kwa kutamka mwenyewe wala kwa kunukuu kiapo cha mtu mwingine.
Ufafanuzi
Ameeleza Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- yakuwa Mwenyezi Mungu Mtukufu anakataza kuapa kwa baba, atakayetaka kuapa basi asiape ila kwa jina la Mwenyezi Mungu, na wala asiape kwa jina la mwingine. Kisha Omari bin Khattwab radhi za Allah ziwe juu yake akaeleza kuwa hakuwahi tena kuapa tangu alipomsikia Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- akikataza kufanya hivyo, si kwa makusudi wala kwa kunukuu kiapo cha mtu mwingine aliyeapa kinyume na Mwenyezi Mungu.
Mafunzo
- Uharamu wa kuapia kinyume na Mwenyezi Mungu, na kataja kumwapia baba kwa sababu hii ilikuwa ni katika desturi za zama za ujinga.
- Kiapo: Ni kuapa kwa jina la Mwenyezi Mungu au kwa majina yake au sifa zake katika jambo miongoni mwa mambo kwa ajili kutilia mkazo.
- Ubora wa Omari radhi za Allah ziwe juu yake kwa wepesi wake wa kutekeleza na uzuri wa uelewa wake na unyenyekevu wake.
Ufafanuzi: العربية
أَخْبَرَ النبيُّ صلى الله عليه وسلم أَنَّ اللهَ تعالى يَنهى عن الحَلِف بالآباء، فمَن أراد الحلف فلا يحلف إلا بالله، ولا يحلف بغيره. ثم ذكر عُمَرُ بن الخطاب رضي الله عنه أنَّه لم يحلِفْ بها منذُ سَمِعَ رسولَ الله صلى الله عليه وسلم ينهى عن ذلك، لا مُتعمِّدًا ولا ناقِلًا عن غيرِِه حَلِفَه بغيرِ الله.
- تحْريمُ الحلِف بغيرِ الله، وخصَّ الحلِف بِالآباء لأنَّه من عاداتِ الجَاهِلِيةِ.
- الحَلِف: هو القَسَم بالله أو بأسماء الله أو بصفات الله على أمر من الأمور لتأكيده.
- فَضِيلةُ عُمَر رضي الله عنه بِسُرْعَةِ امْتِثَالِه وَحُسْنِ فَهْمِهِ وتَوَرُّعِه.