Hadithi

Mkono unakatwa kwa robo Dinari na kuendelea

Chanzo: HadeethEnc.com, Kiswahili v1.18.0

SahihiWamekubaliana Bukhari na Muslim juu ya usahihi wake

Matini ya Kiarabu

عَنْ عَائِشَةَ أُمِّ المؤْمنينَ رَضيَ اللهُ عنها قَالَت: قَالَ النَّبِيُّ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ: «تُقْطَعُ اليَدُ فِي رُبُعِ دِينَارٍ فَصَاعِدًا».

Tafsiri

Kutoka kwa Aisha -radhi za Allah ziwe juu yake- amesema: Amesema Mtume -rehema na amani ziwe juu yake-: "Mkono unakatwa kwa robo Dinari na kuendelea".

Ufafanuzi

Amebainisha Mtume rehema na amani ziwe juu yake kuwa mwizi unakatwa mkono wake kwa kuiba robo Dinari ya dhahabu, na zaidi ya hapo, na kiwango chake kinalingana na kiasi cha Gramu 1.06 ya dhahabu.

Mafunzo

  • Wizi ni katika madhambi makubwa.
  • Ameweka mpaka Mwenyezi Mungu Mtukufu wa adhabu ya mwizi, nayo ni kukata mkono wake, kama ilivyo katika kauli yake Mtukufu: "Na mwizi mwanaume na mwizi mwanamke basi ikateni mikono yao" [Maaida: 38], na mafundisho ya Mtume rehema na amani ziwe juu yake yamebainisha sharti za kukata huku.
  • Makusudio ya mkono katika hadithi ni kukikata kiganja katika maungio yake kati yake na muundi wa mkono.
  • Na miongoni mwa hekima katika kukata mkono wa mwizi, ni kulinda mali za watu, na kumkomesha mtu mwingine katika watu wanaofanya uadui katika mali za watu.
  • Dinari ni uzito wa dhahabu, na inalingana kwa sasa na (Gramu 4.25) kwa kipimo cha 24; hivyo robo Dinari inalingana na gramu moja na kitu.
Ufafanuzi: العربية

بيَّن النبيُّ صلى الله عليه وسلم أن السارق تقطع يده بسرقة ربع دينار من الذهب، وما زاد على ذلك، ويعادل ما قيمته تساوي قيمة 1.06 غرامًا من الذهب.

  • السرقة من كبائر الذنوب.
  • حدد الله سبحانه وتعالى عقوبة السارق، وهي قطع يده؛ كما في قوله تعالى: {والسارق والسارقة فاقطعوا أيديهما} [المائدة: 38]، وقد بينت السنة شروط هذا القطع.
  • المراد باليد في الحديث قطع الكف من مفصله بينه وبين العضد.
  • من الحكمة في قطع يد السارق، حماية أموال الناس، وردع غيره من المعتدين.
  • الدينار مثقال من الذهب، ويعادل حاليا (4.25 جم) عيار 24؛ فربع الدينار يعادل جرامًا وشيئًا.

Mada

Ripoti kosa

Zaidi