Chanzo: HadeethEnc.com, Kiswahili v1.18.0
Matini ya Kiarabu
عَنْ أَبِي بُرْدَةَ الْأَنْصَارِيِّ رَضيَ اللهُ عنهُ أَنَّهُ سَمِعَ رَسُولَ اللهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ يَقُولُ: «لَا يُجْلَدُ أَحَدٌ فَوْقَ عَشَرَةِ أَسْوَاطٍ إِلَّا فِي حَدٍّ مِنْ حُدُودِ اللهِ».
Tafsiri
Imepokelewa kutoka kwa Abuu Huraira -radhi za Allah ziwe juu yake- yakuwa yeye alimsikia Mtume -rehema na amani ziwe juu yake- akisema: "Hapigwi mtu zaidi ya viboko kumi isipokuwa kama itakuwa katika kutelekeza sheria miongoni mwa sharia za Mwenyezi Mungu".
Ufafanuzi
Amekataza Mtume rehema na amani ziwe juu yake kupigwa mtu yeyote zaidi ya viboko kumi isipokuwa katika maasi, na pia hakuna maelekezo yoyote yaliyokuja katika sheria kueleza idadi maalumu ya viboko au kipigo au adhabu maalumu, na makusudio yake haizidishwi katika kipigo cha kuadabisha zaidi ya viboko kumi, kama kumpiga mke au mtoto.
Mafunzo
- Mipaka ya Mwenyezi Mungu Mtukufu aliyoiamrisha au aliyoikataza inaadhabu zinazokomesha hayo, ima zimepangwa katika sheria, au zinarudi kukadiriwa kwake katika masilahi anayoyaona hakimu.
- Kutia adabu kunakuwa kwa kiasi kidogo, kwa kiasi cha kuelekeza na kuhofisha, kusizidishwe zaidi ya viboko kumi ikibidi kufanya hivyo, na kilichobora zaidi ni kuwaadabisha pasina kuwapiga, bali kwa kuwaelekeza, na kuwafundisha, na kuwaongoza, na kuwatia hamasa, hilo huleta msukumo mkubwa wa kukubali na upole katika kujifunza, na hali katika nafasi hii hutofautiana sana, inapasa mtu afanye kinachofaa.
Ufafanuzi: العربية
نهى النبيُّ صلى الله عليه وسلم أن يجلد أحد أكثر من عشرة أسواط إلا في المعاصي، وليس المراد ما ورد فيه من الشارع عدد محدد من الجلد أو الضرب أو العقوبة المخصوصة، والمراد لا يُزاد في ضرب التأديب على عشرة أسواط، كجلد الزوجة والابن.
- حدود الله تعالى التي أمر بها أو نهى عنها لها عقوبات تردع عنها، إما مقدرة من الشارع، أو راجعة في تقديرها إلى المصلحة التي يراها الحاكم.
- التأديب يكون خفيفًا بقدر التوجيه والتخويف، فلا يزاد فيه على عشرة أسواط إن احتيج لذلك، والأولى تأديبهم بدون الضرب، بل بالتوجيه، والتعليم، والإرشاد، والتشويق، فهو أدعى للقبول واللطف في التعليم، والأحوال في هذا المقام تختلف كثيرًا، فينبغي فعل الأصلح.