Chanzo: HadeethEnc.com, Kiswahili v1.18.0
Matini ya Kiarabu
عَنْ ابنِ عُمَرَ رَضيَ اللهُ عنهما عَنْ رَسُولِ اللهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ قَالَ: «مَنِ اقْتَنَى كَلْبًا إِلَّا كَلْبَ ضَارٍ أَوْ مَاشِيَةٍ نَقَصَ مِنْ عَمَلِهِ كُلَّ يَوْمٍ قِيرَاطَانِ»، قَالَ سَالِمٌ: وَكَانَ أَبُو هُرَيْرَةَ يَقُولُ: «أَوْ كَلْبَ حَرْثٍ»، وَكَانَ صَاحِبَ حَرْثٍ.
Tafsiri
Na imepokelewa kutoka kwa bin Omari -radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake yeye na baba yake -kwamba Mtume wa Mwenyezi Mungu -rehema na amani ziwe juu yake- amesema: "Atakayefuga mbwa isipokuwa mbwa wa mawindo au wa mifugo, basi yatapungua katika matendo yake kila siku kiratu (shehena) mbili", Amesema Salim: Na alikuwa Abuu Huraira akisema: "Au mbwa wa shamba", Naye akawa na shamba.
Ufafanuzi
Ametahadharisha Mtume rehema na amani ziwe juu yake kufuga mbwa, isipokuwa kwa haja ya kuwinda, au kulinda mifugo na mazao, na atakayemfuga pasina haja hizo zitapungua katika thawabu za matendo yake kila siku shehena mbili; ambazo ujazo wake unajulikana mbele ya Mwenyezi Mungu Mtukufu.
Mafunzo
- Hifai kwa muislamu kufuga mbwa, isipokuwa katika hali zilizotajwa.
- Kukatazwa kufuga mbwa; kwa sababu ya hasara na madhara mengi yanayopatikana ndani yake, kwani imethibiti kutoka kwa Mtume rehema na amani ziwe juu yake kuwa Malaika hawaingii nyumba ambayo kuna mbwa ndani yake; na ni kwa sababu mbwa ananajisi nzito ambayo hakuna kinachoweza kuiondosha isipokuwa kurudiarudia kuosha kwa maji na udongo.
Ufafanuzi: العربية
حذّر النبيُّ صلى الله عليه وسلم من اقتناء الكلاب، إلا لحاجة الصيد، أو حراسة الماشية والزروع، ومن اقتناه لغير ذلك نقص من ثواب عمله كل يوم قيراطان؛ وهو مقدار معلوم عند الله تعالى.
- لا يجوز للمسلم أن يقتني الكلب، إلا فيما استثني.
- منع اقتناء الكلاب؛ لما فيه من المفاسد والمضار الكثيرة، فقد ثبت عن النبي صلى الله عليه وسلم أن الملائكة لا تدخل بيتًا فيه كلب؛ ولما فيه من النجاسة الغليظة التي لا يزيلها إلا تكرار الغسل بالماء والتراب.