Chanzo: HadeethEnc.com, Kiswahili v1.18.0
Matini ya Kiarabu
عَنْ عَائِشَةَ أُمِّ المُؤْمِنين رَضِيَ اللَّهُ عَنْهَا، قَالَتْ: مَا رَأَيْتُ النَّبِيَّ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ مُسْتَجْمِعًا قَطُّ ضَاحِكًا، حَتَّى أَرَى مِنْهُ لَهَوَاتِهِ، إِنَّمَا كَانَ يَتَبَسَّمُ.
Tafsiri
Imepokelewa kutoka kwa Aisha mama wa waumini radhi za Allah ziwe juu yake, amesema: Sikumuona Mtume -rehema amani ziwe juu yake- katu akipitiliza kucheka mpaka kionekane Kilimi ndani ya mdomo wake, bali alikuwa akitabasamu.
Ufafanuzi
Alieleza Aisha radhi za Allah ziwe juu yake kuwa Mtume rehema amani ziwe juu yake alikuwa hapitilizi kucheka mpaka kionekane kilimi chake, nacho ni kinyama kinachoning'inia juu ya koo, bali alikuwa akitabasam.
Mafunzo
- Kulikuwa kucheka kwa Mtume rehema amani ziwe juu yake ni kutabasam anaporidhia au kufurahishwa na jambo.
- Amesema bin Hajari: Sikuwahi kumuona akipitiliza katika kucheka kiasi cha kucheka kicheko kamili kwa kujiachia mzima mzima kwa kicheko.
- Kukithirisha kucheka na kunyanyua sauti kwa kujikohoza hii si miongoni mwa sifa za watu wema.
- Kukithirisha kucheka kunaondoa haiba ya mtu na heshima yake mbele ya ndugu zake.
Ufafanuzi: العربية
أَخْبَرَتْ عائشةُ رضي الله عنها أنَّ النبيَّ صلى الله عليه وسلم لم يكن مُبالِغًا في الضحك حتى تُرى لَهَاتُهُ، وهي اللَّحْمَة المُتعلِّقة في أعلى الحَلْق، إنما كان يَتَبَسّم.
- كان رسول الله صلى الله عليه وسلم ضَحِكُهُ التبسم إذا رضي أو أُعْجِب بشيء.
- قال ابن حجر: ما رأيته مُستجْمِعًا من جهة الضحك بحيث يضحك ضَحِكًا تامًّا مُقبِلًا بِكُلّيته على الضحك.
- كثرة الضحك وارتفاع الصوت بالقهقهة ليس من صفات الصالحين.
- كثرة الضحك تُذهِب هيبةَ الرجل ووقارَه بين إخوانه.