Hadithi

Fanyeni haraka kufanya matendo kuna fitina nzito kama kipande cha usiku wa giza,

Chanzo: HadeethEnc.com, Kiswahili v1.18.0

SahihiImepokelewa Imamu Muslim

Matini ya Kiarabu

عَنْ أَبِي هُرَيْرَةَ رضي الله عنه أَنَّ رَسُولَ اللهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ قَالَ: «بَادِرُوا بِالْأَعْمَالِ فِتَنًا كَقِطَعِ اللَّيْلِ الْمُظْلِمِ، يُصْبِحُ الرَّجُلُ مُؤْمِنًا وَيُمْسِي كَافِرًا، أَوْ يُمْسِي مُؤْمِنًا وَيُصْبِحُ كَافِرًا، يَبِيعُ دِينَهُ بِعَرَضٍ مِنَ الدُّنْيَا».

Tafsiri

Imepokelewa kutoka kwa Abuu Huraira -Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake- yakwamba Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- amesema: "Fanyeni haraka kufanya matendo kuna fitina nzito kama kipande cha usiku wa giza, anaamka mtu akiwa muislamu anafika jioni akiwa kafiri, na anashinda akiwa muumini anaamka asubuhi akiwa kafiri, anauza dini yake kwa thamani ndogo ya dunia"

Ufafanuzi

Mtume rehema na amani ziwe juu yake anamtaka Muumini kufanya hima na kufanya mambo mengi ya kheri kabla hayajashindikana, na akashughulishwa na kuja kwa fitna na mambo yenye kutatiza yanayoweza kuzuia kufanya matendo mema, na kuyaziba, na hali ni kwamba, ni giza kama kipande cha usiku ambao ndani yake haki imechanganyika na batili, na kukawawia vigumu watu kutofautisha baina yake, na kwa sababu ya ukali wake (Fitina hiyo), mtu huchanganyikiwa kiasi cha kuamka muumini, na kufika jioni ni kafiri, kushinda Muumini na kufika asubuhi kawa kafiri, anaiacha dini yake kwa starehe za muda mfupi za dunia.

Mafunzo

  • Ni lazima kushikamana na dini, na kwenda mbio katika matendo mema kabla ya vikwazo kuzuia hilo.
  • Hii ni ishara ya mfuatano wa majaribu yenye kupoteza katika zama za mwisho, na kwamba wakati wowote fitina moja inapotoweka, fitina ingine linafuata.
  • Ikiwa dini ya mtu ni dhaifu na akaiacha kwa kubadilishana na mambo ya kidunia, kama vile pesa au vitu vingine, hii ni sababu ya kupotoka kwake, kuacha dini, na kuingia kwake kwenye vishawishi na fitina.
  • Kuna ushahidi katika Hadithi kwamba matendo mema ni njia ya kuokoka na fitina.
  • Kuna aina mbili za fitina: Fitina ya shubuha (Mambo yenye utata), na tiba yake ni elimu, na fitina ya matamanio, na tiba yake ni imani na subira.
  • Hadithi inaashiria kuwa mwenye matendo kidogo, fitina kwake ni nyepesi zaidi, na mwenye matendo mengi anatakiwa asihadaike na alichonacho, bali aongeze zaidi.
Ufafanuzi: العربية

يَحُثُّ النبيُّ صلى الله عليه وسلم المؤمنَ بالمسارعة والإكثار من الأعمال الصالحة قبل تعذُّرِها والاشتغال عنها بمجيء الفتن والشبهات التي تمنع منها، وتصد عنها، وهي مظلمة كقطع الليل، يختلط فيها الحق بالباطل، فيصعب على الناس التمييز بينهما، ومن شدتها يتخبط الإنسان حتى إنه يصبح مؤمنًا ويمسي كافرًا، ويمسي مؤمنًا ويصبح كافرًا، يترك دينه بمتاع من الدنيا زائل.

  • وجوب التمسُّك بالدين، والمبادرة إلى العمل الصالح قبل أن تَحوْل الموانع دونه.
  • الإشارة إلى تتابع الفتن المضلة آخر الزمان، وأنه كلما ذهبت فتنة أعقبتها فتنة أخرى.
  • إذا ضَعُف دين الإنسان وتنازل عنه مقابل الأمور الدنيوية من مال أو غيره كان ذلك سببًا في انحرافه وتركه للدين وانسياقه مع الفتن.
  • في الحديث دليل على أن الأعمال الصالحة سبب للنجاة من الفتن.
  • الفتن قسمان: فتن شبهات وعلاجها العلم، وفتن شهوات وعلاجها الإيمان والصبر.
  • في الحديث إشارة إلى أن مَن قلَّ عمله كانت الفتنة إليه أسرع، وأن من كثر عمله ينبغي ألّا يغتر بما عنده بل يستزيد.

Mada

Ripoti kosa

Zaidi