Hadithi

Atakapofika mmoja wenu katika kikao basi na atoe salamu, na akitaka kunyanyuka pia atoe salamu, kwani ya mwanzo haina haki zaidi kuliko ya mwisho

Chanzo: HadeethEnc.com, Kiswahili v1.18.0

Ni nzuri (Hasan)Imepokelewa na Abu Daud, Tirmidhiy na Nasai katika kitabu Alkubraa na Ahmad

Matini ya Kiarabu

عَنْ أَبِي هُرَيْرَةَ رَضيَ اللهُ عنهُ قَالَ: قَالَ رَسُولُ اللَّهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ: «إِذَا انْتَهَى أَحَدُكُمْ إِلَى الْمَجْلِسِ فَلْيُسَلِّمْ، فَإِذَا أَرَادَ أَنْ يَقُومَ فَلْيُسَلِّمْ، فَلَيْسَتِ الْأُولَى بِأَحَقَّ مِنَ الْآخِرَةِ».

Tafsiri

Imepokelewa kutoka kwa Abuu Huraira -radhi za Allah ziwe juu yake- amesema: Amesema Mtume -rehema na amani ziwe juu yake-: "Atakapofika mmoja wenu katika kikao basi na atoe salamu, na akitaka kunyanyuka pia atoe salamu, kwani ya mwanzo haina haki zaidi kuliko ya mwisho".

Ufafanuzi

Alimuelekeza Mtume rehema na amani ziwe juu yake atakayekuja mahali walipokaa watu basi awasalimie, na akitaka kunyanyuka basi awaage jamaa zake pia kwa salamu; kwani salamu ya kwanza wakati wa kuja si bora sana kuliko salamu ya mwisho wakati wa kuondoka.

Mafunzo

  • Himizo la kusambaza salamu.
  • Himizo la kuwasalimia jamaa waliokaa wakati wa kukutana nao na wakati wa kuondoka.
  • Amesema Assanadi: Kauli yake: "Na akitaka kunyanyuka" Yaani: Kutoka katika kikao, "Salamu Ya mwanzo haina haki zaidi" Yaani: Zote mbili ni sunna halisi zinazotakiwa kufanyiwa kazi, hakuna hiyari ya kuiacha ya pili na kuthibitisha ya kwanza.
Ufafanuzi: العربية

أَرشدَ النبي صلى الله عليه وسلم من جاء لمكان جلوس الناس أن يُسلّم عليهم، فإذا أراد أن يقوم منه فليودع أهله أيضًا بالسلام؛ فليس السلام الأول عند المجيئ بأحق من السلام الآخر عند المغادرة.

  • الحث على إفشاء السلام.
  • الحث على التسليم على أهل المجلس عند اللقاء وعند الانصراف.
  • قال السندي: قوله (وإذا أراد أن يقوم) أي: من المجلس، (فليس الأول بأحق) أي: هما جميعًا سنةٌ حقيقةٌ بالعمل بها، فلا وجه لترك الثاني مع إثبات الأول.

Mada

Ripoti kosa

Zaidi