Hadithi

Namuapa yule ambaye nafsi ya Muhammadi iko mkononi mwake, hatonisikia yeyote katika umma huu, Myahudi wala Mkristo, kisha akafa haliyakuwa hajayaamini yale niliyotumwa kwayo, isipokuwa atakuwa ni katika watu wa motoni

Chanzo: HadeethEnc.com, Kiswahili v1.18.0

SahihiImepokelewa Imamu Muslim

Matini ya Kiarabu

عَنْ أَبِي هُرَيْرَةَ رضي الله عنه عَنْ رَسُولِ اللهِ صلى الله عليه وسلم أنه قال: «وَالَّذِي نَفْسُ مُحَمَّدٍ بِيَدِهِ لَا يَسْمَعُ بِي أَحَدٌ مِنْ هَذِهِ الْأُمَّةِ يَهُودِيٌّ وَلَا نَصْرَانِيٌّ، ثُمَّ يَمُوتُ وَلَمْ يُؤْمِنْ بِالَّذِي أُرْسِلْتُ بِهِ إِلَّا كَانَ مِنْ أَصْحَابِ النَّارِ».

Tafsiri

Imepokewa Kutoka kwa Abuu Huraira -Radhi za Allah ziwe juu yake- kutoka kwa Mtume -sala na amani ziwe juu yake- amesema: "Namuapa yule ambaye nafsi ya Muhammadi iko mkononi mwake, hatonisikia yeyote katika umma huu, Myahudi wala Mkristo, kisha akafa haliyakuwa hajayaamini yale niliyotumwa kwayo, isipokuwa atakuwa ni katika watu wa motoni".

Ufafanuzi

Anaapa Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- kuwa hakuna atayemsikia katika umma huu, Myahudi au Mkristo au mwingine yeyote utakayemfikia ujumbe wa Mtume -sala na amani ziwe juu yake- kisha akafa na hakumuamini isipokuwa atakuwa miongoni mwa watu wa motoni ataishi humo milele daima.

Mafunzo

  • Kuenea kwa ujumbe wa Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- kwa ulimwengu mzima, na ulazima wa kumfuata kwake, na kufutwa kwa sheria zote kupitia sheria yake.
  • Atakayempinga Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- hayatomfaa kitu madai yake ya kudai kumwamini Nabii mwingine katika Manabii -Amani ya Mwenyezi Mungu iwe juu yao wote-.
  • Ambaye hakumsikia Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake-, na haukumfikia ujumbe wa Uislamu huyu atapewa udhuru, na hukumu yake huko Akhera itakuwa kwa Mwenyezi Mungu Mtukufu.
  • Yanathibitika manufaa kwa Uislamu kwa mtu hata kama atasilimu muda mchache kabla ya kifo, hata kama atakuwa katika maradhi mabaya, madama tu roho haijafika kooni.
  • Kuiona kuwa ni sahihi dini ya makafiri -wakiwemo Mayahudi na Wakristo- ni ukafiri.
  • Amemtaja Myahudi na Mkristo katika hadithi kama tahadhari kwa wenye kuwaona kuwa wako sawa; na hii ni kwakuwa Mayahudi na Wakristo wana kitabu, na ikiwa ndio hivyo, basi kwa wengine wasiokuwa na kitabu ndio wanastahiki zaidi kuingia motoni, wote hao wanalazimika kuingia katika dini yake na kumtii yeye Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake-.
Ufafanuzi: العربية

يَحْلِفُ النبيُّ صلى الله عليه وسلم بالله أنه لا يَسمعُ به أَحَدٌ مِن هذه الأمة، يَهوديٌّ أو نصرانيٌّ أو غيرُهما تَبْلُغُه دعوةُ النبي صلى الله عليه وسلم ثم يموت ولم يؤمن به إلا كان من أصحاب النار خالدًا فيها أبدًا.

  • عموم رسالةِ النبيِّ صلى الله عليه وسلم إلى جميع العالم، ووجوب اتِّباعِه، ونسخ جميع الشرائع بشرعه.
  • مَن كَفَرَ بالنبي صلى الله عليه وسلم لم ينفعه زَعْمُه إيمانَه بغيرِه من الأنبياء صلوات الله عليهم أجمعين.
  • من لم يَسمع بالنبي صلى الله عليه وسلم، ولم تَبْلغْه دعوةُ الإسلام فهو معذور، وأَمْرُه في الآخرة إلى الله تعالى.
  • يتحقق الانتفاع بالإسلام وإن كان قُبيل الموت، ولو في المرض الشديد، ما لم تبلغ الروح الحلقوم.
  • تصحيح دين الكفار -ومنهم اليهود والنصارى- كُفْرٌ.
  • ذكر اليهودي والنصراني -في الحديث- تنبيهًا على من سواهما؛ وذلك لأن اليهود والنصارى لهم كتاب، فإذا كان هذا شأنهم، فغيرهم ممن لا كتاب له أولى، فكلُّهم يجب عليهم الدخول في دينه وطاعته صلى الله عليه وسلم.

Mada

Ripoti kosa

Zaidi