Hadithi

Mfano wa aliyesimama katika mipaka ya Mwenyezi Mungu na mwenye kuingia ndani yake, ni kama mfano wa watu waliotengeneza boti (safina)

Chanzo: HadeethEnc.com, Kiswahili v1.18.0

SahihiImepokelewa na Al-Bukhaariy

Matini ya Kiarabu

عَنِ النُّعْمَانِ بْنِ بَشِيرٍ رَضِيَ اللَّهُ عَنْهُمَا عَنِ النَّبِيِّ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ قَالَ: «مَثَلُ القَائِمِ عَلَى حُدُودِ اللَّهِ وَالوَاقِعِ فِيهَا، كَمَثَلِ قَوْمٍ اسْتَهَمُوا عَلَى سَفِينَةٍ، فَأَصَابَ بَعْضُهُمْ أَعْلاَهَا وَبَعْضُهُمْ أَسْفَلَهَا، فَكَانَ الَّذِينَ فِي أَسْفَلِهَا إِذَا اسْتَقَوْا مِنَ المَاءِ مَرُّوا عَلَى مَنْ فَوْقَهُمْ، فَقَالُوا: لَوْ أَنَّا خَرَقْنَا فِي نَصِيبِنَا خَرْقًا وَلَمْ نُؤْذِ مَنْ فَوْقَنَا، فَإِنْ يَتْرُكُوهُمْ وَمَا أَرَادُوا هَلَكُوا جَمِيعًا، وَإِنْ أَخَذُوا عَلَى أَيْدِيهِمْ نَجَوْا، وَنَجَوْا جَمِيعًا».

Tafsiri

Kutoka kwa Nuumaan bin bashiri Radhi za Allah ziwe juu yao, kutoka kwa Mtume Rehema na amani ziwe juu yake amesema: "Mfano wa aliyesimama katika mipaka ya Mwenyezi Mungu na mwenye kuingia ndani yake, ni kama mfano wa watu waliotengeneza boti (safina), wakawa baadhi yao wako juu ya safina na wengine wako chini yake, na wakawa wale walioko chini yake wanapohitajia maji wanakwenda kwa wale walioko juu yao, wakasema: Lau kama tungetoboa katika sehemu yetu kitobo wala tusingewaudhi walioko juu yetu, ikiwa watawaacha watekeleze walilolikusudia wataangamia wote, na ikiwa watawashika na kuwazuia wataokoka na wataokoka wote".

Ufafanuzi

Mtume Rehema na amani ziwe juu yake amepiga mfano wa wale wenye kusimama katika mipaka ya Mwenyezi Mungu, wenye msimamo katika amri ya Mwenyezi Mungu, wenye kuamrisha mema na kukataza maovu, na mfano wa wenye kutumbukia katika mipaka ya Mwenyezi Mungu wenye kuacha mema, na kufanya maovu, na athari ya hilo katika kusalimika jamii, ni sawa na mfano wa watu waliopanda boti, wakagawana nafasi nani akae juu na nani akae chini ya boti, wengine wakapata nafasi ya kukaa juu na wengine wakapata nafasi ya kukaa chini, na wakawa hawa walioko chini wanapotaka kuchota maji wanakwenda kwa wale walioko juu yao, Kisha wale wa chini wakasema: Lau tungeli toboa tundu mahali petu chini ili tusiwaudhi walio juu yetu, basi lau walio juu wangewaacha kufanya hivyo, basi meli ingewazamisha wote, na lau wangeliwakataza na kuwazuia, makundi yote mawili yangeokoka.

Mafunzo

  • Umuhimu wa kuamrisha mema na kukataza maovu katika kuzihifadhi jamii na kusalimika kwake.
  • Miongoni mwa njia ya ufundishaji ni kupiga mifano, kwa ajili ya kusogeza uelewa wa akili kwa picha ya kitu chenye kueleweka.
  • Kufanya uovu kwa wazi na kuto kukemea madhara yake yanarudi katika jamii nzima.
  • Kuangamia kwa jamii kunaambatana na kuwaacha waovu wakiendelea kutapakaza maovu katika Ardhi.
  • Kufanya mambo kimakosa na nia ikawa njema hili halitoshi kurekebisha matendo.
  • Majukumu katika jamii ya kiislamu ni ya watu wote, hayaegemezwi kwa mtu maalum.
  • Kuadhibiwa kwa watu wote kwa sababu ya madhambi ya wachache, ikiwa hayatokemewa.
  • Waovu hudhihirisha maovu yao kwa sura ya kheri katika jamii kama walivyo wanafiki.
Ufafanuzi: العربية

ضَرَبَ النبيُّّ صلى الله عليه وسلم مَثَلًا للقائمين بحدود الله، المستقيمين على أمر الله، الآمرين بالمعروف، الناهين عن المنكر، ومثل الواقعين في حدود الله التاركين للمعروف، المرتكبين للمنكر، وأثر ذلك في نجاة المجتمع، كمثل قوم ركبوا في سفينة، فاقترعوا على مَن يَجلس أعلى السفينة ومَن يَجلس أسفلَها، فنال بعضُهم أعلاها، وبعضُهم أسفلَها، وكان الذين في الأسفل إذا أرادوا جَلْبَ الماءِ مَرُّوا على من فوقهم، فقال الذين في الأسفل: لو أنَّا خَرَقْنا خرقًا في مكاننا في الأسفل نستقي منه، حتى لا نؤذي من فوقنا، فلو تركهم مَن بالأعلى يَفعلون ذلك، لَغَرِقَت السفينةُ بهم جميعًا، ولو قاموا بنهيهم عن ذلك ومنعوهم، لنجى الفريقان جميعًا.

  • أهمية الأمر بالمعروف والنهي عن المنكر في حفظِ المجتمعات ونجاتِها.
  • من طُرُقِ التعليم ضَرْبُ الأمثال، لتقريب المعاني للعقول بصورة المحسوس.
  • فِعْلُ المنكرِ الظاهرِ مع عدم الإنكار عليه مفسدةٌ تعود على الجميع بالضرر.
  • هلاك المجتمع مُتَرَتِّب على ترك أصحاب المنكر يعيثون في الأرض فسادًا.
  • التصرف الخاطئ والنية الحسنة لا تكفي في صلاح العمل.
  • المسؤولية في المجتمع المسلم مشتركة لا تُناط بفرد بعينه.
  • تعذيب العامة بذنوب الخاصة إن لم تُنكر.
  • أصحاب المنكرات يُظهرون مُنكرَهم في قالب خير للمجتمع كما أهل النفاق.

Mada

Ripoti kosa

Zaidi