Hadithi

Msiseme: Ni kwakutaka Mwenyezi Mungu na fulani, lakini semeni: Akitaka Mwenyezi Mungu kisha akataka fulani

Chanzo: HadeethEnc.com, Kiswahili v1.18.0

Sahihi kwa mkusanyiko wa njia zakeImepokelewa naAbu Daud na Nasai katika Sunan Alkubra na Ahmad

Matini ya Kiarabu

عَنْ حُذَيْفَةَ رضي الله عنه أَنَّ رَسُولَ اللهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ قَالَ: «لَا تَقُولُوا: مَا شَاءَ اللهُ وَشَاءَ فُلَانٌ، وَلَكِنْ قُولُوا: مَا شَاءَ اللهُ ثُمَّ شَاءَ فُلَانٌ».

Tafsiri

Imepokewa Kutoka kwa Hudhaifa -Radhi za Allah ziwe juu yake- yakwamba Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- amesema: "Msiseme: Ni kwakutaka Mwenyezi Mungu na fulani, lakini semeni: Akitaka Mwenyezi Mungu kisha akataka fulani".

Ufafanuzi

Amekataza Mtume Rehema na amani ziwe juu yake kwa muislamu kusema katika maneno yake: "Akitaka Mwenyezi Mungu na akitaka fulani", Au akitaka Mwenyezi Mungu na fulani; Na hii ni kwa sababu matashi ya Mwenyezi Mungu na maamuzi yake ni ya moja kwa moja na hakuna yeyote anaye shirikiana naye, Na katika matumizi ya kiunganishi "Na" hii inamaanisha kuwa kuna mtu anayeshirikiana pamoja na Mwenyezi Mungu na kuwa wako sawa katika maamuzi. Lakini aseme: Akitaka Mwenyezi Mungu, kisha fulani, Hivyo basi afanye matashi ya mja yanafuata matashi ya Mwenyezi Mungu kwa kauli yake: " Kisha" badala ya "Na", kwa sababu kiunganishi "Kisha" humaanisha kuja baada ya kitu kingine na kuchelewa pia.

Mafunzo

  • Uharamu wa kusema: " Akitaka Mwenyezi Mungu na ukitaka", na mfano wa matamshi kama haya ambayo yatamaanisha kuunganisha neno na Mwenyezi Mungu kwa kiunganishi "Na"; kwa sababu hii ni katika shirki ya matamshi.
  • Inafaa kusema: " Akitaka Mwenyezi Mungu kisha ukitaka", na mfano wa hayo ambayo yanamaanisha kuunganisha maneno kwa kiunganishi "Kisha"; kwa kuwa hakuna katazo ndani yake.
  • Hapa kumethibitishwa matashi kwa Mwenyezi Mungu, na matashi ya mja, nakuwa matashi ya mja yanafuata matashi ya Mwenyezi Mungu Mtukufu.
  • Katazo la kuwashirikisha viumbe katika matashi ya Mwenyezi Mungu hata kama ni kwa matamshi.
  • Ikiwa mtu ataitakidi kuwa matashi ya mja ni sawa na matashi ya Mwenyezi Mungu Mtukufu katika kuenea kwake na kutokuwa na mipaka, nakuwa mja ana matashi binafsi ya kwake mwenyewe, hii ni shirki kubwa, ama akiitakidi kuwa matashi ya mja yanakaribia matashi ya Mwenyezi Mungu; hii ni shirki ndogo.
Ufafanuzi: العربية

نَهَى النبيُّ صلى الله عليه وسلم أنْ يقولَ المسلمُ في كلامه: "ما شاء الله وشاء فلان"، أو ما شاء الله وفلان؛ وذلك لأنَّ مَشيئةَ الله وإرادتَه مُطْلَقَةٌ ولا يشاركه فيها أحد، وفي استخدام الواو في العطف إشعارٌ بمشاركةِ أحدٍ مع الله والتسوية بينهما. ولكن يقول: ما شاء الله، ثم شاء فلان، فيجعل مشيئةَ العبدِ تابعةً لمشيئة الله بقول: "ثم" بدلًا من "و"، لأن "ثم" تفييد التعقيب والتراخي.

  • تحريم قول: "ما شاء الله وشئت"، وما أشبه ذلك من الألفاظ مما فيه العطف على الله بالواو؛ لأنه من شرك الألفاظ والأقوال.
  • جواز قول: "ما شاء الله ثم شئت"، وما أشبه ذلك مما فيه العطف على الله بثُمَّ؛ لانتفاء المحذور فيه.
  • إثبات المشيئة لله، وإثبات المشيئة للعبد، وأن مشيئة العبد تابعة لمشيئة الله تعالى.
  • النهي عن إشراك الخلق في مشيئة الله ولو باللفظ.
  • إن اعتقد القائل أن مشيئة العبد كمشيئة الله جل وعلا مساوية لها في الشمول والإطلاق، أو أن العبد له مشيئة مستقلة فهو شرك أكبر، أما إن اعتقد أنه دونه؛ فهو شرك أصغر.

Mada

Ripoti kosa

Zaidi