Chanzo: HadeethEnc.com, Kiswahili v1.18.0
Matini ya Kiarabu
عَنْ أَبِي هُرَيْرَةَ رضي الله عنه أَنَّ رَسُولَ اللهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ قَالَ: «أَلَا أَدُلُّكُمْ عَلَى مَا يَمْحُو اللهُ بِهِ الْخَطَايَا، وَيَرْفَعُ بِهِ الدَّرَجَاتِ؟» قَالُوا بَلَى يَا رَسُولَ اللهِ قَالَ: «إِسْبَاغُ الْوُضُوءِ عَلَى الْمَكَارِهِ، وَكَثْرَةُ الْخُطَا إِلَى الْمَسَاجِدِ، وَانْتِظَارُ الصَّلَاةِ بَعْدَ الصَّلَاةِ، فَذَلِكُمُ الرِّبَاطُ».
Tafsiri
Imepokelewa kutoka kwa Abuu Huraira -Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake- yakwamba Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- amesema: "Je! nikujulisheni mambo ambayo yakifanyika Allah hufuta madhambi na hupandisha daraja kwa mambo hayo?" wakasema: Ndiyo, ewe Mtume wa Allah, akasema: "Kutawadha vizuri wakati wa baridi, na kuzidisha hatua kwenda msikitini, na kusubiria swala baada ya swala huko ndiko kuizuia nafsi katika mambo ya kheri."
Ufafanuzi
Mtume rehema na amani ziwe juu yake, aliwauliza maswahaba zake iwapo wanataka awaongoze katika matendo yatakayowapelekea kupata msamaha wa madhambi, na kufutwa kwake kutoka katika vitabu vya Malaika wenye kuhifadhi, na kupata daraja za juu Peponi? Maswahaba wakasema: Ndio tunataka hivyo. Akasema: Ya kwanza: Kueneza na kukamilisha udhu kwa shida; kama vile baridi, ukosefu wa maji, na maumivu ya mwili, na maji ya moto. Pili: Kupiga hatua nyingi - ambazo ni kati ya miguu miwili- kwenda misikiti iliyo mbali na nyumbani, na kurudi rudi kila wakati. Tatu: Kungoja wakati wa Swala, na moyo kuambatana nayo, na kujitayarisha kwa ajili yake, na kukaa msikitini kwa ajili yake kungojea jamaa, anaposwali hungojea mahali pake pa kuswali kwa ajili ya swala nyingine. Kisha akaeleza rehema na amani ziwe juu yake kuwa mambo haya ndiyo Jihadi ya kweli; Kwa sababu yanaziba njia za Shetani juu ya nafsi, na yanatenza nguvu matamanio, na yanaizuia isiingiwe na wasi wasi, hivyo kundi la Mwenyezi Mungu likashinda majeshi ya Shetani kupitia hayo; na hii ndiyo Jihadi kubwa zaidi, kwakuwa imekuwa kama kikosi cha jeshi upande wa maadui.
Mafunzo
- Umuhimu wa kuihifadhi swala ya jamaa msikitini, na kuzipa kipaumbele swala na kutozipuuza.
- Uzuri wa uwasilishaji wake Mtume rehema na amani ziwe juu yake wa mada na kuwatia kwake hamu Maswahaba zake, kwani alianza kuwatajia ujira mkubwa kwa njia ya kuuliza swali, na hii ni njia mojawapo ya ufundishaji.
- Faida ya kuwasilisha suala kwa maswali na majibu: Ili mazungumzo yakite ndani ya nafsi kwa sababu ya utata wake kisha kuyatolea ufafanuzi.
- Amesema An-Nawawi, Mwenyezi Mungu amrehemu: Hiyo ndio Jihadi: Maana yake ni Jihadi iliyohimizwa, na asili ya neno (Ribat) ni kufunga kitu, kana kwamba mtu amejifunga kwa ajili ya ibada hizi, na imesemwa kuwa: Ni Jihadi bora, kama ilivyosemwa: Jihadi ni jihadi ya nafsi, na inawezekana kuwa ni Jihadi nyepesi inayowezekana, yaani: ni aina mojawapo ya Jihadi.
- Neno “Ribat” lilirudiwa na kufafanuliwa kwa ufafanuzi (Alif na Lam); Hii ni kwa ajili ya utukufu wa matendo haya.
Ufafanuzi: العربية
سَألَ النبيُّ صلى الله عليه وسلم أصحابَه هل يُريدون أنْ يدلَّهم على أعمال تكون سببًا في مغفرة الذنوب، ومحوها من كُتب الحفظة، وعلو المنازل في الجنة؟ قال الصحابة: نعم نريد ذلك. قال: الأول: استيعاب وإتمام الوضوء على مشقة؛ كَبردٍ، وقلة ماء، وألم جسم، وماء حار. الثاني: كثرة الخُطا -وهي ما بين القدمين- إلى المساجد ببعد الدار، وكثرة التكرار. الثالث: انتظار وقت الصلاة، وتعلُّق القلب بها، والتأهب لها، والجلوس لها في المسجد لانتظار الجماعة، فإذا صلاها انتظر في مصلاه صلاةً أخرى. ثم بيَّنَ صلى الله عليه وسلم أنَّ هذه الأمور هي المرابطة الحقيقية؛ لأنها تسد طرق الشيطان على النفس، وتقهر الهوى، وتمنعها من قبول الوساوس، فيغلب بها حزبُ الله جنودَ الشيطان؛ وذلك هو الجهاد الأكبر، فكانت بمنزلة الرباط على ثغر العدو.
- أهمية المحافظة على صلاة الجماعة في المسجد، والاهتمام بالصلوات وعدم التشاغل عنها.
- حسن عرض النبي صلى الله عليه وسلم وتشويقه لأصحابه حيث بدأهم بثواب عظيم على طريقة السؤال، وهذه طريقة من طرق التعليم.
- فائدة عرض المسألة بالسؤال والجواب: أن يكون الكلام أوقع في النفس بحكم الإبهام والتبيين.
- قال النووي رحمه الله: فذلكم الرباط أي: الرباط المرغَّب فيه، وأصل الرباط الحبس على الشيء، كأنه حبس نفسه على هذه الطاعة، وقيل: إنه أفضل الرباط كما قيل: الجهاد جهاد النفس، ويحتمل أنه الرباط المتيسر الممكن، أي: إنه من أنواع الرباط.
- كررت كلمة "الرباط" وعرفت ب(ال) التعريف؛ ذلك تعظيمٌ لشأن هذه الأعمال.