Chanzo: HadeethEnc.com, Kiswahili v1.18.0
Matini ya Kiarabu
عَنْ أَبِي هُرَيْرَةَ رضي الله عنه: أَنَّ رَجُلًا قَالَ: يَا رَسُولَ اللهِ إِنَّ لِي قَرَابَةً أَصِلُهُمْ وَيَقْطَعُونِي، وَأُحْسِنُ إِلَيْهِمْ وَيُسِيئُونَ إِلَيَّ، وَأَحْلُمُ عَنْهُمْ وَيَجْهَلُونَ عَلَيَّ، فَقَالَ: «لَئِنْ كُنْتَ كَمَا قُلْتَ، فَكَأَنَّمَا تُسِفُّهُمُ الْمَلَّ وَلَا يَزَالُ مَعَكَ مِنَ اللهِ ظَهِيرٌ عَلَيْهِمْ مَا دُمْتَ عَلَى ذَلِكَ».
Tafsiri
Imepokelewa kutoka kwa Abuu Huraira -radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake-: Yakwamba mtu mmoja alisema: Ewe Mjumbe wa Mwenyezi Mungu, hakika mimi nina ndugu wa karibu, ninawaunga lakini wao wananitenga, ninawafanyia wema lakini wao wanatendea ubaya, na ninakuwa mpole kwao lakini wao wananifanyia ujeuri, basi akasema: "Ikiwa kama utakuwa kama ulivyosema, basi ni kana kwamba unawalisha majivu ya moto (dhambi wanazozipata ni kama mtu anayekula majivu ya moto), na bado anaendelea kuwa pamoja nawe msaidizi kutoka kwa Mwenyezi Mungu dhidi yao, madam bado uko katika hali hiyo".
Ufafanuzi
Mtu mmoja alilalamika kwa Mtume rehema na amani ziwe juu yake kuwa ana ndugu wa karibu wa ukoo anaamiliana nao kwa wema ila wao wanaamiliana naye kinyume na hivyo; anawaunga na kuwatembelea ila wao wanamtenga, na anawatendea ihisani kwa wema na uadilifu ila wao wanamtendea ubaya kwa ujeuri na ukaidi, na anakuwa mpole kwao na kuwasamehe ila wao wanampuuza kwa kumfanyia mabaya katika kauli na vitendo, je, aendelee kuwaunga udugu pamoja na hayo yote yaliyotajwa? Mtume rehema na amani ziwe juu yake akasema kumwambia: Ikiwa ni hivyo kama ulivyoeleza basi wewe unawafedhehesha na kuwadharaulisha katika nafsi zao, ni kana kwamba unawalisha majivu ya moto; kwa wingi wa wema wako na kwa ubaya wa matendo yao mbele ya nafsi zao, na bado anaendelea kuwa pamoja nawe msaidizi kutoka kwa Mwenyezi Mungu dhidi yao, na wao waendelee katika kukutendea ubaya.
Mafunzo
- Kuukabili ubaya kwa wema ni sehemu ya kumfanya muovu arejee katika haki, kama alivyosema Mtukufu: "Zuia (ubaya) kwa lile lililo jema, punde yule ambaye baina yako na yeye kuna uadui atakuwa kama rafiki mwandani"
- Kutekeleza amri ya Mwenyezi Mungu hata kama kutatokea maudhi ni sababu ya kupata msaada wa Mwenyezi Mungu kwa mja muumini.
- Kukata udugu ni maumivu na ni adhabu katika dunia, na ni madhambi na hesabu siku ya Kiyama.
- Ni wajibu kwa muislamu ataraji malipo katika amali yake njema, na wala yasimkatishe maudhi ya watu na kumtenga kwao kukamuachisha ibada yake nzuri.
- Si muunga udugu yule anayelipa wema wa yule aliyemuunga udugu, lakini muunga udugu wa kweli ni yule ambaye ukikatwa udugu wake yeye anauunga.
Ufafanuzi: العربية
اشتَكَى رَجُلٌ للنبيِّ صلى الله عليه وسلم بأنّ له قرابةً ورَحِمًا يَتَعامَل معهم بالحُسنى وهم يُعامِلونه بضد ذلك؛ فيَصِلُهم ويأتِيْهم وهم يَقْطَعونه، ويُحسن إليهم بالبر والوفاء ويُسيئون إليه بالجَوْر والجَفَاء، ويَحلم ويعفو عنهم ويَجهلون عليه بالقبيح من القول والفعل، فهل يَستَمِرُّ بالصِّلَة لهم مع ما ذُكِر؟ فقال له النبيُّ صلى الله عليه وسلم: إنْ كان كما ذَكَرتَ فإنك تُخزِيهم وتَحْقِرُهم في أنفسهم، وكأنك تُطعِمُهم الرَّمَاد الحارّ؛ لكثرة إحسانك وقبيح فِعلِهم عند أنفسهم، ولا يزال معك من عند الله مُعين لك عليهم، ودافِع عنك أذاهم ما دُمْتَ على ما ذَكرتَ من إحسانك إليهم، وظَلُّوا هم على إساءتهم إليك.
- مقابلة الإساءة بالإحسان مَظِنّة رجوع المسيء إلى الحق، كما قال تعالى: (ادفع بالتي هي أحسن فإذا الذي بينك وبينه عداوة كأنه ولي حميم).
- امتثال أمْر الله ولو حصل له أذى سببٌ لعون الله للعبد المؤمن.
- قطيعة الرحم أَلَمٌ وعذابٌ في الدنيا، وإثمٌ وحساب في الآخرة.
- ينبغي على المسلم أنْ يَحتَسِب في عمله الصالح، ولا يقطعه أذى الناس وقطيعتُهم عن عادته الطيبة.
- ليس الواصلُ لِرَحِمِهِ مَن يُكافِئ مَن وَصَله، ولكن الواصل حقيقة هو الذي إذا قُطِعَتْ رَحِمُه وَصَلَها.