Chanzo: HadeethEnc.com, Kiswahili v1.18.0
Matini ya Kiarabu
عَنْ جَابِرٍ رَضيَ اللهُ عنهُ عَنِ النَّبِيِّ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ قَالَ: «مَنْ قَالَ: سُبْحَانَ اللهِ العَظِيمِ وَبِحَمْدِهِ، غُرِسَتْ لَهُ نَخْلَةٌ فِي الجَنَّةِ».
Tafsiri
Imepokelewa kutoka kwa Jabiri -radhi za Allah ziwe juu yake- kutoka kwa Mtume -rehema na amani ziwe juu yake- amesema: "Atakayesema: Sub-haanallaahi wabihamdi, (Ametakasika Mwenyezi Mungu Mtukufu na sifa njema ni zake) ataoteshewa mti wa mtende peponi".
Ufafanuzi
Ameeleza Mtume rehema na amani ziwe juu yake yakuwa atakayesema: "Ametakasika Mwenyezi Mungu" ninamtakasa "Mtukufu" kwa dhati yake na sifa zake na vitendo vyake "na sifa njema ni zake" zikiwa zimeambatanishwa na kuegemeza sifa za ukamilifu wake Mtukufu; atasimikiwa na kupandiwa mti wa mtende katika ardhi ya Pepo kwa kila mara atakayosema.
Mafunzo
- Himizo la kukithirisha kumtaja Mwenyezi Mungu Mtukufu, na miongoni mwake: Ni kufanya tasbihi na tahmidi (kumtukuza na kumsifu).
- Pepo ni pana, na kwamba mimea yake ni tasbihi na tahmidi (Kumtuza na kumsifu), na hii ni fadhila kutoka kwa Mwenyezi Mungu Mtukufu na neema yake.
- Umetajwa mtende pekee katika hadithi pasina miti mingine; kwa sababu ya wingi wa faida zake na uzuri wa matunda yake; na ndiyo maana Mwenyezi Mungu Mtukufu amepiga mfano wa muumini na imani yake ndani ya Qur'ani kwa mti huo.
Ufafanuzi: العربية
أخبرَ النبيُّ صلى الله عليه وسلم أنه من قال: (سبحان الله) وأنزهه (العظيم) بذاته وصفاته وأفعاله (وبحمده) مقرونًا بإضافة أوصاف الكمال له سبحانه؛ نُصبت وغرست له نخلة في أرض الجنة بكل مرة يقولها.
- الحث على الإكثار من ذكر الله تعالى، ومن ذلك: التسبيح مع التحميد.
- الجنة واسعة، وأن غراسها التسبيح والتحميد، فضلاً من الله تعالى ونعمة.
- خصت النخلة في الحديث دون غيرها من الأشجار؛ لكثرة منافعها وطيب ثمرتها؛ ولذلك ضرب الله تعالى مثل المؤمن وإيمانه بها في القرآن.