Chanzo: HadeethEnc.com, Kiswahili v1.18.0
Matini ya Kiarabu
عَنْ ابْنِ عَبَّاسٍ رَضِيَ اللَّهُ عَنْهُمَا أَنَّ رَسُولَ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ قَالَ: «إنَّ اللَّهَ تَجَاوَزَ لِي عَنْ أُمَّتِي الخَطَأَ وَالنِّسْيَانَ وَمَا اسْتُكْرِهُوا عَلَيْهِ».
Tafsiri
Imepokelewa kutoka kwa bin Abbas radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake na baba yake kwamba Mtume rehema na amani ziwe juu yake amesema: "Hakika Mwenyezi Mungu ameniondolea mimi kwa umma wangu (madhambi ya) kukosea na kusahau, na yale waliyolazimishwa".
Ufafanuzi
Anaeleza Mtume rehema na amani ziwe juu yake: Ya kwamba Mwenyezi Mungu ameusamehe umma wake katika hali tatu: La kwanza: Kukosea, nayo ni yale yanayotokea kwao pasina kukusudia, nayo ni muislamu kukusudia kufanya jambo lolote, kisha kitendo chake kikakutana na jambo ambalo hakulikusudia. La pili: Kusahau, nako ni muislamu kuwa na kumbukumbu ya kitu, lakini akakisahau wakati wa kufanya, hana madhambi katika hilo pia. La tatu: Kulazimishwa, mja anaweza kulazimishwa kufanya kitu ambacho hakitaki pamoja na kutoweza kuzuia kulazimishwa, na hapo pia hatopata dhambi au ubaya. Pamoja na tahadhari kuwa maudhui ya hadithi ni katika yale yalio baina ya mja na Mola wake katika kufanya maharamisho, ama kuacha maamrisho kwa kusahau hapa haiondoki, na ama kitendo chake kikiambatana na kosa la jinai hii pia haiondoki katika haki ya kiumbe, kama akiua kimakosa, atatakiwa kutoa fidia, au akaharibu gari kwa makosa atawajibika kulipa.
Mafunzo
- Upana wa huruma ya Mwenyezi Mungu Mtukufu na upole wake kwa waja wake kiasi ambacho amewaondolea madhambi pale yatakapojitokeza maasi katika hali hizi tatu.
- Fadhila ya Mwenyezi Mungu kwa Mtume rehema na amani ziwe juu yake juu ya umma wake.
- Kuondolewa dhambi haimaanishi kuondolewa hukumu au dhamana, mfano atakayesahau udhu, na akaswali kwa kudhani kuwa yuko twahara, hana dhambi katika hilo, lakini atatakiwa kutia udhu na kurudia swala.
- Lazima katika kuondolewa dhambi kwa kulazimishwa kuwe na sharti, mfano kama akiwa mlazimishaji anauwezo wa kutimiza alichotishia.
Ufafanuzi: العربية
يخبر النبي صلى الله عليه وسلم : أن الله عفا عن أمته في ثلاثة أحوال: الأولى: الخطأ، وهو ما صدر منهم دون تعمد، وهو أن يقصد المسلم بفعله شيئًا، فيصادف فعله غير ما قصده. والثانية: النسيان، وهو أن يكون المسلم متذكرًا لشيء، ولكن ينساه عند الفعل، فلا إثم في ذلك أيضًا. والثالثة: الإكراه ، فقد يُكره العبد على فعل شيء لا يريده مع عدم قدرته على دفع الإكراه، وحينئذٍ لا يقع عليه الإثم أو الحرج. مع ملاحظة أن موضوع الحديث فيما بين العبد وربه في فعل المحظور، فأما ترك المأمور نسيانًا فلا يسقط، وأما لو ترتب على فعله ذلك جناية فلا يسقط حق المخلوق، كما لو قتل خطًأ، فعليه الدية، أو أتلف سيارة خطأ فعليه الضمان.
- سعة رحمة الله -عزّ وجل- ولطفه بعباده حيث رفع عنهم الإثم إذا صدرت منهم المعصية على هذه الأحوال الثلاثة.
- فضل الله على النبي محمد صلى الله عليه وسلم وأمته.
- رفعُ الإثم لا يعني رفع الحكم أو الضمان، فمثلًا من نسي الوضوء، وصلى ظانًّا أنه متطهر، فلا إثم عليه بذلك، ولكن عليه الوضوء وإعادة الصلاة.
- لا بد في رفع الإثم بالإكراه من توفر الشروط، مثل أن يكون المكِره قادرًا على تنفيذ ما هدد به.