Hadithi

Kila kiungo kwa watu kina sadaka

Chanzo: HadeethEnc.com, Kiswahili v1.18.0

SahihiWamekubaliana Bukhari na Muslim juu ya usahihi wake

Matini ya Kiarabu

عَنْ أَبِي هُرَيْرَةَ رَضِيَ اللَّهُ عَنْهُ قَالَ: قَالَ رَسُولُ اللَّهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ: «كُلُّ سُلاَمَى مِنَ النَّاسِ عَلَيْهِ صَدَقَةٌ، كُلَّ يَوْمٍ تَطْلُعُ فِيهِ الشَّمْسُ يَعْدِلُ بَيْنَ الِاثْنَيْنِ صَدَقَةٌ، وَيُعِينُ الرَّجُلَ عَلَى دَابَّتِهِ فَيَحْمِلُ عَلَيْهَا أَوْ يَرْفَعُ عَلَيْهَا مَتَاعَهُ صَدَقَةٌ، وَالكَلِمَةُ الطَّيِّبَةُ صَدَقَةٌ، وَكُلُّ خُطْوَةٍ يَخْطُوهَا إِلَى الصَّلاَةِ صَدَقَةٌ، وَيُمِيطُ الأَذَى عَنِ الطَّرِيقِ صَدَقَةٌ».

Tafsiri

Imepokelewa kutoka kwa Abuu Huraira -Radhi za Allah ziwe juu yake- amesema: Amesema Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake-: "Kila kiungo kwa watu kina sadaka, kila siku inayochomozewa jua: Ukafanya uadilifu kati ya watu wawili ni sadaka, na ukimsaidia mtu katika mnyama wake ukambeba kumpandisha au ukamnyanyulia mzigo wake ni sadaka, na neno zuri ni sadaka, na kwa kila hatua unayokwenda kuelekea msikitini ni sadaka, na ukiondoa maudhi njiani ni sadaka".

Ufafanuzi

Mtume rehema na amani ziwe juu yake ameeleza kuwa kila Muislamu ni wajibu kila siku kuhesabu kila kiungo cha mifupa yake kuwa ni sadaka ya hiyari kwa Mwenyezi Mungu Mtukufu na kuwa ni njia ya kumshukuru kwa neema ya afya, na kwamba amevifanya viungo vyake kuwa na maungio yanayomuwezesha kukunja na kukunjua, Sadaka hii inafanywa na matendo yote mema na haitegemei kutoa pesa, na miongoni mwake: Uadilifu wako na kusuluhisha kwako kati ya wagomvi wawili ni sadaka, Na katika kumsaidia kwako asiyejiweza kupanda katika mnyama wake, ukambeba, au ukamnyanyulia mzigo, ni sadaka. na neno zuri kuanzia kumtaja Mwenyezi Mungu na dua na salamu na mengineyo, ni sadaka, na kwa kila hatua unayoipiga kwenda katika swala, ni sadaka, na kuondoa kila yanayoudhi katika njia ni sadaka.

Mafunzo

  • Muundo wa mifupa na viungo vya mwanadamu ni moja ya neema kubwa za Mwenyezi Mungu juu yake, hivyo kila mfupa peke yake unahitaji kutolewa sadaka kwa niaba yake ili itimie kushukuru neema hiyo.
  • Himizo la kurudia upya shukurani kila siku ili neema hizo zidumu.
  • Himizo la kudumu kufanya ibada za sunna na sadaka kila siku.
  • Fadhila ya kusuluhisha baina ya watu.
  • Himizo la mtu kumsaidia ndugu yake; kwani msaada wake kwake ni sadaka.
  • Himizo la kuhudhuria swala za pamoja na kuziendea, na kuimarisha misikiti kwa hilo.
  • Uwajibu wa kuheshimu njia wanazopita waumini kwa kuepuka yanayo waudhi au kuwadhuru.
Ufafanuzi: العربية

بَيَّنَ النبيُّ صلى الله عليه وسلم أنَّ على كلِّ مسلم مُكلَّف كلّ يوم بعدد كل مفصل من مفاصل عظامه صدقة تطوع لله تعالى على سبيل الشكر له على العافية، وأن جعل عظامه مفاصل يتمكن بها من القبض والبسط، وأنّ تلك الصدقة تتأدّى بأعمال البر كلها ولا تتوقف على إعطاء مال، ومنها: عدلك وإصلاحك بيـن متخاصمين صدقةٌ، وفي إعانتك لعاجز في دابته فتحمله عليها أو ترفع له متاعه صدقةٌ، والكلمة الطيبة من ذكر ودعاء وسلام وغيرها صدقةٌ، وبكل خطوةٍ تمشيها إلى الصلاة صدقةٌ، وإزالة ما يُتَأذّى به عن الطريق صدقةٌ.

  • تركيب عظام الآدمي وسلامتها من أعظم نعم الله تعالى عليه، فيحتاج كل عظم منها إلى تصدق عنه بخصوصه ليتم شكر تلك النعمة.
  • الترغيب في تجديد الشكر كل يوم لدوام تلك النعم.
  • الترغيب في المداومة على النوافل والصدقات كل يوم.
  • فضل الإصلاح بين الناس.
  • الحث على معونة الرجل أخاه؛ لأن معونته إياه صدقة.
  • الحث على حضور الجماعات والمشي إليها، وعمارة المساجد بذلك.
  • وجوب احترام طرق المسلمين بتجنب ما يؤذيهم أو يضر بهم.

Mada

Ripoti kosa

Zaidi