Hadithi

Usikasirike

Chanzo: HadeethEnc.com, Kiswahili v1.18.0

SahihiImepokelewa na Al-Bukhaariy

Matini ya Kiarabu

عن أبي هريرة رضي الله عنه: أَنَّ رَجُلًا قَالَ لِلنَّبِيِّ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ: أَوْصِنِي، قَالَ: «لَا تَغْضَبْ» فَرَدَّدَ مِرَارًا قَالَ: «لَا تَغْضَبْ».

Tafsiri

Imepokewa Kutoka kwa Abuu Huraira -Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake-: Ya kwamba mtu mmoja alisema kumwambia Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake-: Niusie, akasema: " Usikasirike" Akarudia mara kadhaa, akasema: "Usikasirike".

Ufafanuzi

Mmoja kati ya Masahaba -Radhi za Allah ziwe juu yao- alimuomba Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- amjulishe katika jambo litakalomnufaisha, akamuamrisha asikasirike, na maana ya hapa nikuwa aziepuke sababu zinazoweza kumpelekea katika kukasirika, na aidhibiti nafsi yake na hasira zinapompata, asiendelee na hasira zake mpaka kufikia kuuwa au kupiga au kutoa matusi na mfano wa hayo. Na yule bwana akarejea tena kuomba usia mara kadhaa, hakumzidishia Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- katika usia zaidi ya "Usikasirike"

Mafunzo

  • Tahadhari dhidi ya hasira na sababu zake, kwani ndio chanzo kikuu cha shari, na kujikinga nayo ni chanzo cha kheri.
  • Kuchukia kwa ajili ya Mwenyezi Mungu kama kuchukia wakati yanapofanyika maharamisho yake ni miongoni mwa hasira nzuri.
  • Kurudia maneno wakati wa haja mpaka ayaelewe msikilizaji na atambue umuhimu wake.
  • Ubora wa kuomba usia kutoka kwa msomi.
Ufafanuzi: العربية

طَلبَ أحدُ الصحابة رضوان الله عليهم من النبي صلى الله عليه وسلم أن يَدُلَّه على شيء ينفعه، فأمره ألّا يغضب، ومعنى ذلك أن يَجتنبَ الأسبابَ التي تحمله على الغضب، وأن يَضبطَ نفسَه إذا حَصَل له الغضب، فلا يَتَمادى مع غضبه بالقتل أوالضرب أوالسب ونحو ذلك. وردَّدَ الرجلُ طَلَبَ الوصيةِ مَرَّات، فلم يَزِدْه صلى الله عليه وسلم في الوصية على "لا تغضب".

  • التحذير من الغضب وأسبابه، فإنه جِماعُ الشر، والتحرُّزُ منه جماعُ الخير.
  • الغضب لله كالغضب عند انتهاك محارم الله من الغضب المحمود.
  • تَكرار الكلام عند الحاجة حتى يَعِيَه السامعُ ويُدرك أهميتَه.
  • فضيلة طلب الوصية من العالِم.

Mada

Ripoti kosa

Zaidi