Hadithi

Enyi watu, tubieni kwa Mwenyezi Mungu, kwani mimi ninatubia kwa siku mara mia moja

Chanzo: HadeethEnc.com, Kiswahili v1.18.0

SahihiImepokelewa Imamu Muslim

Matini ya Kiarabu

عن الْأَغَرِّ رضي الله عنه، وَكَانَ مِنْ أَصْحَابِ النَّبِيِّ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ، قَالَ: قَالَ رَسُولُ اللهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ: «يَا أَيُّهَا النَّاسُ تُوبُوا إِلَى اللهِ، فَإِنِّي أَتُوبُ فِي الْيَوْمِ إِلَيْهِ مِائَةَ مَرَّةٍ».

Tafsiri

Kutoka kwa Agharri radhi za Allah ziwe juu yake, na alikuwa katika Maswahaba wa Mtume rehema na amani ziwe juu yake, amesema: Amesema Mtume rehema na amani ziwe juu yake: "Enyi watu, tubieni kwa Mwenyezi Mungu, kwani mimi ninatubia kwa siku mara mia moja".

Ufafanuzi

Anawaamrisha Mtume rehema na amani ziwe juu yake watu kukithirisha kuomba toba na msamaha, na anajielezea mwenyewe kuwa yeye hutubia kwa Mwneyezi Mungu Mtukufu na kumuomba msamaha kwa siku zaidi ya mara mia moja, na haliyakuwa alikwisha samehewa yaliyotangulia katika madhambi yake na yajayo, na katika hilo kuna ukamilifu wa kujidhalilisha kwa Mwenyezi Mungu Aliyetakasika na kutukuka.

Mafunzo

  • Kila mmoja vyovyote itakavyokuwa nafasi yake na daraja lake katika imani, basi anahitaji kurejea kwa Mwenyezi Mungu Aliyetakasika na kutukuka, na kuikamilisha nafsi yake kwa toba, nakuwa kila mmoja hakosi mapungufu katika kutimiza haki za Mwenyezi Mungu Aliyetakasika na kutukuka: "Na tubieni kwa Mwenyezi Mungu nyote enyi waumini".
  • Toba ni kwa mambo yote, sawa sawa kwa kufanya maharamisho au madhambi au uzembe katika kutimiza wajibu.
  • Ikhlasi (kutakasa nia) katika toba ni sharti la kukubaliwa kwake, atakayeacha dhambi kwa ajili ya asiyekuwa Mwenyezi Mungu huyo bado hajatubia.
  • Amesema Nawawi: Toba ina masharti matatu: Ajivue katika maasi, na ajute kwa kuyafanya, na atie dhamira ya kweli ya kutorudi katika maasi mfano wake kabisa, na ikiwa maasi yanahusiana na haki ya binadamu basi kuna sharti la nne, nalo: Kurudisha haki aliyodhulumu kwa mwenye nayo, na kujivua nayo.
  • Tahadhari: Kuomba msamaha kwa Mtume rehema na amani ziwe juu yake hakuna maana kuwa kuna madhambi aliyafanya, lakini ni kwa sababu ya ukamilifu wa utumwa wake na kufungamana kwake na kumtaja Aliyetakasika na kutukuka, na kuvuta kwake taswira ya utukufu wa haki ya Mwenyezi Mungu Mtukufu na upungufu wa mja kwa namna yoyote atakayofanya katika kushukuru neema zake, nayo inakuwa ni sehemu ya kuwawekea sheria umma wake baada yake, na hukumu zinginezo.
Ufafanuzi: العربية

يَأْمُرُ النبيُّ صلى الله عليه وسلم الناسَ بالإكثار مِن التوبة والاستغفار، ويُخْبِرُ عن نفسه أنه يتوب إلى الله تعالى ويستغفره في اليوم أكثر من مائة مرة، وقد غُفِر له ما تقدم من ذنبه وما تأخر، وفي ذلك كمال الذُّلِّ والتعبد لله جل وعلا.

  • كلُّ أحدٍ مهما كانت مرتبته ودرجته في الإيمان، فإنَّه يحتاج إلى الرجوع إلى الله تبارك وتعالى، وتكميل نفسه بالتوبة، وأنَّ كلَّ أحدٍ لا يخلو من تقصيرٍ في القيام بحقِّ الله تبارك وتعالى: (وَتُوبُوا إِلَى اللَّهِ جَمِيعًا أَيُّهَ الْمُؤْمِنُونَ).
  • التوبة عامة سواء من فعل المحرّمات والذنوب أو من التقصير في فعل الواجبات.
  • الإخلاص في التوبة شرط في قبولها، فمن ترك ذنبًا لغير الله لا يكون تائبًا.
  • قال النووي: للتوبة ثلاثة شروط: أن يُقْلِع عن المعصية، وأن يَندم على فعلها، وأن يَعزم عزمًا جازمًا ألَّا يعود إلى مثلها أبدًا، فإن كانت المعصية تتعلق بآدمي فلها شرط رابع، وهو: رَدُّ الظلامة إلى صاحبها، أو تحصيل البراءة منه.
  • التنبيه على أن استغفار النبي صلى الله عليه وسلم لا يلزم أن يكون لذنوب ارتكبها، ولكن ذلك لكمال عبوديته وتعلقه بذكره سبحانه، واستشعاره عظم حق الله تعالى وتقصير العبد مهما عمل في شكر نعمه، وهو من باب التشريع للأمة من بعده، إلى غير ذلك من الحكم.

Mada

Ripoti kosa

Zaidi