Hadithi

Walikuwa wana wa Israeli wakiongozwa na Manabii, kila anapokufa nabii anafuatiwa na nabii mwingine, na hakika hakuna nabii baada yangu, na watafuata Makhalifa (viongozi) baada yangu, na watakithiri

Chanzo: HadeethEnc.com, Kiswahili v1.18.0

SahihiWamekubaliana Bukhari na Muslim juu ya usahihi wake

Matini ya Kiarabu

عَنْ أَبِي حَازِمٍ قَالَ: قَاعَدْتُ أَبَا هُرَيْرَةَ رضي الله عنه خَمْسَ سِنِينَ، فَسَمِعْتُهُ يُحَدِّثُ عَنِ النَّبِيِّ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ، قَالَ: «كَانَتْ بَنُو إِسْرَائِيلَ تَسُوسُهُمُ الأَنْبِيَاءُ، كُلَّمَا هَلَكَ نَبِيٌّ خَلَفَهُ نَبِيٌّ، وَإِنَّهُ لاَ نَبِيَّ بَعْدِي، وَسَيَكُونُ خُلَفَاءُ فَيَكْثُرُونَ» قَالُوا: فَمَا تَأْمُرُنَا؟ قَالَ: «فُوا بِبَيْعَةِ الأَوَّلِ فَالأَوَّلِ، أَعْطُوهُمْ حَقَّهُمْ، فَإِنَّ اللَّهَ سَائِلُهُمْ عَمَّا اسْتَرْعَاهُمْ».

Tafsiri

Kutoka kwa Abuu Haazim amesema: Nilikaa karibu na Abuu Huraira kwa muda wa miaka hamsini, nikamsikia akihadithia kutoka kwa Mtume rehema na amani ziwe juu yake, akisema: "Walikuwa wana wa Israeli wakiongozwa na Manabii, kila anapokufa nabii anafuatiwa na nabii mwingine, na hakika hakuna nabii baada yangu, na watafuata Makhalifa (viongozi) baada yangu, na watakithiri" Wakasema: Unatuamrisha nini? Akasema: "Timizeni ahadi ya utiifu ya moja baada ya nyingine, wapeni haki zao, kwani Mwenyezi Mungu atawauliza walikuongozeni vipi".

Ufafanuzi

Ameeleza Mtume rehema na amani ziwe juu yake yakuwa wana wa Israeli walikuwa wakiongozwa na Manabii, na wakisimamia mambo yao kama wanavyofanya viongozi na watawala kwa raia, kila unapodhihiri ufisadi Mwenyezi Mungu anawatumia Nabii kwa ajili ya kunyoosha mambo yao na kuondoa yale waliyoyabadilisha katika hukumu. Na hakika hakuna Nabii baada yangu ili afanye kama waliyokuwa wakiyafanya wale, na watakuja baada yangu watawala, na watakuwa wengi, na utatokea mzozano na kuhitilafiana baina yao. Maswahaba radhi za Allah ziwe juu yao wakamuuliza Mtume rehema na amani ziwe juu yake: Unatuamrisha tufanye nini? Akasema: Atakapochaguliwa kiongozi baada ya kiongozi; uteuzi wa kiongozi wa kwanza ndio uteuzi sahihi na ni wajibu kuutimiza na kuuheshimu, na uteuzi wa pili ni batili na ni haramu kwake kuukataa, na wapeni haki zao, na muwatii na muishi nao kwa usikivu na utii isipokuwa katika maasi, kwani Mwenyezi Mungu atawauliza na atawahesabu kwa yale wanayokufanyieni.

Mafunzo

  • Nikuwa ni lazima kwa raia kuwa na nabii au kiongozi mwenye kusimamia mambo yao, na mwenye kuwapeleka katika njia iliyonyooka.
  • Nikuwa hakuna nabii baada ya Nabii wetu Muhammadi rehema na amani ziwe juu yake.
  • Tahadhari ya kujitoa kwa yule ambaye umethibiti uongozi wake kwa njia ya kisheria.
  • Haifai kuweka makubaliano ya kuwachagua viongozi wawili kwa wakati mmoja.
  • Ukubwa wa majukumu ya uongozi, kwa sababu Mwenyezi Mungu atamuuliza kuhusu raia wake.
  • Amesema bin Hajari: Kutanguliza jambo la dini kuliko jambo la dunia; kwa sababu Mtume rehema na amani ziwe juu yake aliamrisha kutimiza haki ya kiongozi kwakuwa ndani yake kuna kuipa nguvu dini na kuzuia fitina na shari; na kuchelewesha swala kudai haki yake haina maana ya kuidondosha, na Mwenyezi Mungu alimuahidi kuwa yeye mwenyewe atamlipa na atamtimizia hata kama ni huko Akhera.
  • Alama miongoni mwa alama za unabii wake rehema na amani ziwe juu yake, hakika walikithiri viongozi baada yake Mtume rehema na amani ziwe juu yake, na umma ukaongozwa na waliokuja kutengeneza miongoni mwao na walioharibu.
Ufafanuzi: العربية

أَخْبَرَ النبيُّ صلى الله عليه وسلم أنَّ بني إسرائيل كانت تسوسهم الأنبياء، ويَتَولَّون أمورهم كما تفعل الأمراء والولاة بالرَّعِيّة، وكلما ظهر فيهم فسادٌ بَعَث الله لهم نبيًا لهم يقيم أمرهم ويزيل ما غيّروا من أحكام. وإنه لا نبي بعدي فيَفْعَل ما كان أولئك يفعلون، وسيكون بعدي خلفاء فيَكْثرون ويحصل بينهم التنازع والخلاف. فسأل الصحابة رضي الله عنهم رسول الله صلى الله عليه وسلم: فما تأمرنا؟ فقال: فإذا بُويع الخليفةُ بعد خَليفة؛ فبيعة الأول صحيحة يجب الوفاء بها، وبيعة الثاني باطلة ويَحْرُم عليه طلبُها، وأعطوهم حقّهم، وأطيعوهم وعاشروهم بالسمع والطاعة في غير المعصية، فإن الله يسألهم ويحاسبهم على ما يفعلونه بكم.

  • أنه لا بد للرعية من نبي أو خليفة يقوم بأمرها، ويحملها على الطريق المستقيم.
  • أنه لا نبي بعد نبينا محمد صلى الله عليه وسلم.
  • التحذير من الخروج على من ثَبَتَتْ ولايته بطريقة شرعية.
  • أنه لا يجوز عقد البيعة لخليفتين في آنٍ واحد.
  • عِظَم مسؤولية الإمام، فإن الله تعالى سيسأله عن رعيته.
  • قال ابن حجر: تقديم أمر الدين على أمر الدنيا؛ لأنه صلى الله عليه وسلم أَمَرَ بتوفية حق السلطان لما فيه من إعلاء كلمة الدين وكف الفتنة والشر؛ وتأخير أمر المطالبة بحقه لا يُسقِطه، وقد وعده الله أنه يُخَلِّصه ويُوَفِّيه إياه ولو في الدار الآخرة.
  • علامة من علامات نبوته صلى الله عليه وسلم، فقد كثر الخلفاء بعده صلى الله عليه وسلم، وتوالى على الأمة المصلحون منهم والمسيؤون.

Mada

Ripoti kosa

Zaidi