Hadithi

Umma wangu wote wataingia peponi isipokuwa atakaye kataa

Chanzo: HadeethEnc.com, Kiswahili v1.18.0

SahihiImepokelewa na Al-Bukhaariy

Matini ya Kiarabu

عن أبي هريرة رضي الله عنه أن رسول الله صلى الله عليه وسلم قال: «كُلُّ أُمَّتِي يَدْخُلُونَ الْجَنَّةَ إِلَّا مَنْ أَبَى»، قَالُوا: يَا رَسُولَ اللهِ، وَمَنْ يَأْبَى؟ قَالَ: «مَنْ أَطَاعَنِي دَخَلَ الْجَنَّةَ، وَمَنْ عَصَانِي فَقَدْ أَبَى».

Tafsiri

Imepokewa Kutoka kwa Abuu Huraira -Radhi za Allah ziwe juu yake- yakwamba Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- amesema: "Umma wangu wote wataingia peponi isipokuwa atakaye kataa" Wakasema: Ewe Mjumbe wa Mwenyezi Mungu, na ni nani atakaye kataa? Akasema: "Atakaye nitii ataingia peponi, na atakaye niasi atakuwa amekataa".

Ufafanuzi

Anaeleza Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- yakwamba umma wake wote wataingia peponi isipokuwa atakaye kataa!. Masahaba -Radhi za Allah ziwe juu yao- wakasema: Ni nani atakaye kataa ewe Mjumbe wa Allah?! Akawajibu -Rehema na amani ziwe juu yake-: Kuwa atakayejisalimisha na akafuata na akamtii Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- ataingia peponi, na ama atakaye asi na akawa hakujisalimisha katika sheria atakuwa kakataa mwenyewe kuingia peponi kwa sababu ya matendo yake mabaya.

Mafunzo

  • Nikuwa kumtii Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- ni katika kumtii Mwenyezi Mungu, na kumuasi kwake ni sehemu ya kumuasi Mwenyezi Mungu.
  • Kumtii Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- hupelekea kuipata pepo, na kumuasi kwake kunapelekea kuingia motoni.
  • Habari njema kwa watiifu walioko katika umma huu, nakuwa wote wataingia peponi isipokuwa atakayemuasi Mwenyezi Mungu na Mtume wake.
  • Huruma yake Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- kwa umma wake, na pupa yake katika kuwaongoa.
Ufafanuzi: العربية

يُخبرُ النبيُّ صلى الله عليه وسلم أنَّ كلَّ أُمَّتِه يدخلون الجنة إلا مَن امتنع! فقال الصحابة رضي الله عنهم: ومَن يمتنع يا رسول الله؟! فأجابهم عليه الصلاة والسلام: أنَّ مَن انقاد واتَّبع وأطاعَ الرسولَ صلى الله عليه وسلم دَخَلَ الجنة، وأما مَن عصى ولم يَنْقَدْ للشرع فقد امتنع من دخول الجنة بأعمالِه السيئة.

  • أن طاعة الرسول صلى الله عليه وسلم من طاعة الله، ومعصيته من معصية الله.
  • طاعة النبي صلى الله عليه وسلم توجب الجنة، ومعصيته توجب النار.
  • بشارة للطائعين من هذه الأمة، وأنهم كلَّهم يدخلون الجنة إلا من عصى الله ورسوله.
  • شفقته صلى الله عليه وسلم على أُمته، وحرصه على هدايتهم.

Mada

Ripoti kosa

Zaidi