Chanzo: HadeethEnc.com, Kiswahili v1.18.0
Matini ya Kiarabu
عَنْ أَبِي بَرْزَةَ الأَسْلَمِيِّ رضي الله عنه قَالَ: قَالَ رَسُولُ اللهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ: «لَا تَزُولُ قَدَمَا عَبْدٍ يَوْمَ القِيَامَةِ حَتَّى يُسْأَلَ عَنْ عُمُرِهِ فِيمَا أَفْنَاهُ، وَعَنْ عِلْمِهِ فِيمَ فَعَلَ، وَعَنْ مَالِهِ مِنْ أَيْنَ اكْتَسَبَهُ وَفِيمَ أَنْفَقَهُ، وَعَنْ جِسْمِهِ فِيمَ أَبْلَاهُ».
Tafsiri
Imepokelewa kutoka kwa Abuu Barza Al Aslamia -Radhi za Allah ziwe juu yake- amesema: Amesema Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake-: "Hautonyanyuka unyayo wa mja siku ya Kiyama mpaka aulizwe kuhusu umri wake aliumaliza katika mambo yapi? Na kuhusu elimu yake aliifanyia kazi katika nini? Na kuhusu mali yake ni wapi aliichuma? Na aliitoa katika mambo gani? Na kuhusu mwili wake aliumaliza katika mambo yapi?"
Ufafanuzi
Ameeleza Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- yakuwa hatovuka mtu yeyote kisimamo cha hesabu siku ya Kiyama kwenda peponi au motoni mpaka aulizwe kuhusu mambo kadhaa: La kwanza: Maisha yake aliyatumia na kuyamaliza katika nini? La pili: Elimu yake, je aliitafuta kwa lengo la kupata radhi za Allah? na je aliifanyia kazi? na je aliifikisha kwa wenye kustahiki? La tatu: Mali yake ni wapi aliichuma, je ni katika halali au haramu? Na aliitoa katika mambo gani, ni katika yale yenye kumridhisha Allah au yenye kumchukiza?. La nne: Mwili wake na nguvu zake na afya yake na ujana wake, aliutumia na kuumaliza katika mambo gani?
Mafunzo
- Himizo la kutumia fursa ya uhai katika yale yenye kumridhisha Allah Mtukufu.
- Neema za Allah kwa waja ni nyingi, na atamuuliza kila mmoja kuhusu neema aliyoishi nayo, hivyo anatakiwa aiweke kila neema ya Allah katika yale yenye kumridhisha.
Ufafanuzi: العربية
أَخْبَرَ النبيُّ صلى الله عليه وسلم أنّه لا يُجاوِزُ أحدٌ مِن الناس مَوقِفَ الحسابِ يوم القيامة إلى جنةٍ أو نارٍ حتى يُسألَ عن أمور: الأول: حياتِه فِيمَ أَفْنَاها وقضاها؟ الثاني: عِلْمِهِ هل طلبه لله؟ وهل عمل به؟ وهل بلّغه لمستحقه؟ الثالث: مَالِهِ مِنْ أَيْنَ اكْتَسَبَهُ أمن حلال أم حرام؟ وَفِيمَ أَنْفَقَهُ فيما يرضي الله أو ما يسخطه؟ الرابع: جِسْمِهِ وقوّته وعافيته وشبابه فيمَ أَبْلَاه واستخدمه؟
- الحث على اغتنام الحياة فيما يرضي الله تعالى.
- نعم الله على العباد كثيرة، وسيسأله عن النعيم الذي كان فيه، فعليه أن يضع نعم الله فيما يرضيه.