Chanzo: HadeethEnc.com, Kiswahili v1.18.0
Matini ya Kiarabu
عَنْ مَعْقِلِ بْنِ يَسَارٍ رضي الله عنه أَنَّ رَسُولَ اللهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ قَالَ: «الْعِبَادَةُ فِي الْهَرْجِ كَهِجْرَةٍ إِلَيَّ».
Tafsiri
Kutoka kwa Ma'qal bin Yasari -radhi za Allah ziwe juu yake- hakika Mtume rehema na amani za Allah ziwe juu yake alisema: "Kufanya ibada katika (nyakati) za vita vurugu na mauaji ni kama kuhama kuja kwangu".
Ufafanuzi
Ameelekeza Mtume rehema na amani ziwe juu yake katika nyakati za vurugu na fitina na mauaji na kuparaganyika kwa mambo ya watu katika ibada na kushikamana nayo, na kwamba malipo yake ni kama kuhama kwenda kwa Mtume rehema na amani ziwe juu yake, na hii ni kwa sababu watu hughafilika nayo, na hawatengi muda ila mtu mmoja mmoja.
Mafunzo
- Himizo la kufanya ibada na kuelekea kwa Mwenyezi Mungu Mtukufu nyakati za fitina; kwa ajili ya kujilinda na fitina, na kujihifadhi na ufisadi.
- Kumebainishwa fadhila za kufanya ibada nyakati za fitina na nyakati za watu kughafilika.
- Inapaswa kwa muislamu ajitenge mbali na mazingira ya fitina na kughafilika.
Ufafanuzi: العربية
أَرْشَدَ النبيُّ صلى الله عليه وسلم في زمن الهَرْج والفتنة والقتل واختلاط أمور الناس إلى العبادة والتمسك بها، وأنّ أجرها كهجرة إلى النبي صلى الله عليه وسلم، وذلك لأن الناس يغفلون عنها، ويشتغلون عنها، ولا يتفرغ لها إلا أفراد.
- الحث على العبادة والإقبال على الله تعالى أيام الفتن؛ تَحَصُّنًا من الفتن، وحِفْظًا من الفساد.
- بيان فضل العبادة في الفتن وأوقات الغفلة.
- ينبغي للمسلم اعتزال مواطن الفتن والغفلة.