Hadithi

Hivi mnajua ni nini kusengenya?", Wakasema: Mwenyezi Mungu na Mtume wake ndio wajuzi, akasema: "Ni kumsema ndugu yako kwa yale anayoyachukia

Chanzo: HadeethEnc.com, Kiswahili v1.18.0

SahihiImepokelewa Imamu Muslim

Matini ya Kiarabu

عن أبي هريرة رضي الله عنه أن رسول الله صلى الله عليه وسلم قال: «أَتَدْرُونَ مَا الْغِيبَةُ؟»، قَالُوا: اللهُ وَرَسُولُهُ أَعْلَمُ، قَالَ: «ذِكْرُكَ أَخَاكَ بِمَا يَكْرَهُ»، قِيلَ: أَفَرَأَيْتَ إِنْ كَانَ فِي أَخِي مَا أَقُولُ؟ قَالَ: «إِنْ كَانَ فِيهِ مَا تَقُولُ فَقَدِ اغْتَبْتَهُ، وَإِنْ لَمْ يَكُنْ فِيهِ فَقَدْ بَهَتَّهُ».

Tafsiri

Imepokewa Kutoka kwa Abuu Huraira -Radhi za Allah ziwe juu yake-yakwamba Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- amesema: "Hivi mnajua ni nini kusengenya?", Wakasema: Mwenyezi Mungu na Mtume wake ndio wajuzi, akasema: "Ni kumsema ndugu yako kwa yale anayoyachukia", Pakasemwa: Waonaje ikiwa niyasemayo yako kwa ndugu yangu? Akasema: "Yakiwa kwake uyasemayo utakuwa umemsengenya, na ikiwa hana basi utakuwa umemzulia uongo".

Ufafanuzi

Anabainisha Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- ukweli kuhusu kusengenya kuliko haramishwa, nako ni: Kumsema muislamu asiyekuwepo kwa yale anayoyachukia, sawa sawa iwe ni katika sifa zake za kimaumbile au za kitabia, mfano: Chongo, mpiga ghushi, muongo, na mfano wa hayo katika sifa mbaya, hata kama sifa hizo anazo. Ama zisipokuwa kwake sifa hizo hii ndio mbaya zaidi kuliko kusengenya, nako ni kuzua uongo, yaani: kumzulia mtu asiyokuwa nayo.

Mafunzo

  • Uzuri wa mafundisho ya Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- kiasi kwamba hutoa mafundisho kwa njia ya swali.
  • Uzuri wa adabu ya Masahaba wakiwa pamoja na Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake-, waliposema: Mwenyezi Mungu na Mtume ndio wajuzi.
  • Kauli ya muulizwaji kwa lile asilolijua: Mwenyezi Mungu ndiye Mjuzi zaidi.
  • Sheria imelinda jamii, na imehifadhi haki na udugu baina yao.
  • Kusengenya ni haramu isipokuwa katika baadhi ya hali kwa ajili ya masilahi; Na miongoni mwake: Ni kuzuia dhulma, kiasi kwamba atamtaja aliyedhulumiwa yule aliyemdhulumu kwa yule anayeweza kumchukulia haki yake, akasema: Fulani kanidhulumu, au kanifanyia jambo hili na lile, ikiwemo pia kutaka ushauri katika swala la kuoa au ushirika au ukaribu, na mfamo wake.
Ufafanuzi: العربية

يُبَيِّنُ النبيُّ صلى الله عليه وسلم حقيقة الغيبة المُحرَّمة، وهي: ذِكْرُ المسلم الغائب بما يَكره، سواء كان من صفاته الخَلْقية أو الخُلُقية، مثل: الأعور الغشاش الكذاب، ونحو ذلك من صفات الذم، ولو كانت تلك الصفة موجودة فيه. وأما إذا لم تكنْ فيه الصفةُ فهذا أشدُّ من الغيبة، وهو البُهْتَان، أي: الافتراء على الإنسان بما ليس فيه.

  • حُسْن تعليم النبي صلى الله عليه وسلم، حيث يُلقي المسائل على طريقة السؤال.
  • حُسْن أدب الصحابة مع النبي صلى الله عليه وسلم، حين قالوا: الله ورسوله أعلم.
  • قول المسؤول عن ما لا يعلمه: الله أعلم.
  • صيانة الشريعة للمجتمع بحفظ الحقوق والأخوة بينهم.
  • الغيبة محرمة إلا في بعض الأحوال للمصلحة؛ ومن ذلك: دفع الظلم، بحيث يَذكرُ المظلومُ مَن ظَلَمَه عند من يستطيع الأخذ بحقه، فيقول: ظلمني فلان، أو فعل بي كذا، ومنها: المشاورة في أمر الزواج أو المشاركة أو المجاورة، ونحو ذلك.

Mada

Ripoti kosa

Zaidi