Hadithi

Atakayependa kukunjuliwa katika riziki yake, na acheleweshewe ajali yake, basi na aunge udugu wake

Chanzo: HadeethEnc.com, Kiswahili v1.18.0

SahihiWamekubaliana Bukhari na Muslim juu ya usahihi wake

Matini ya Kiarabu

عن أنس بن مالك رضي الله عنه أن رسول الله صلى الله عليه وسلم قال: «مَنْ أَحَبَّ أَنْ يُبْسَطَ لَهُ فِي رِزْقِهِ، وَيُنْسَأَ لَهُ فِي أَثَرِهِ، فَلْيَصِلْ رَحِمَهُ».

Tafsiri

Imepokewa kutoka kwa Anas bin Maliki -Radhi za Allah ziwe juu yake- : Yakwamba Mtume wa Mwenyezi Mungu -Rehema na amani ziwe juu yake Amesema: "Atakayependa kukunjuliwa katika riziki yake, na acheleweshewe ajali yake, basi na aunge udugu wake".

Ufafanuzi

Anahimiza Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- juu ya kuwaunga ndugu wa karibu kwa kuwatembelea na takrima za mwili na mali na mengineyo, nakuwa kufanya hilo ni sababu ya kukunjuliwa riziki, na kupewa umri mrefu.

Mafunzo

  • Ndugu wa karibu ni wale wa upande wa baba na mama, na kadiri anavyokuwa wa karibu zaidi ndivyo anavyokuwa bora zaidi kwa kuungwa udugu.
  • Malipo huendana na matendo, atakayeunga udugu wake kwa wema na ihisani, naye pia Mwenyezi Mungu atamuunga katika umri wake na riziki yake.
  • Kuunga udugu ni sababu ya kukunjuliwa riziki na kupanuliwa kwake, na ni sababu ya umri mrefu, hata kama kifo na riziki vina muda maalum isipokuwa hili linaweza kuwa ni baraka katika riziki na umri, akafanya mengi katika umri wake na yenye manufaa zaidi kuliko atakavyofanya mwingine, na wanasema wanachuoni; ziada katika riziki na umri ni zaida ya uhalisia. Na Allah ndiye Mjuzi zaidi.
Ufafanuzi: العربية

يَحُثُّ النبيُّ صلى الله عليه وسلم على صِلة الأقاربِ بالزيارة والإكرام البدني والمالي وغير ذلك، وأنها سببٌ في سَعة الرزق وطول العمر.

  • الرَّحِم هم الأقارب من جهة الأب والأم، وكلما كان أقرب كان أولى بالصلة.
  • الجزاء من جنس العمل، فمَن وَصَل رَحِمَه بالبر والإحسان، وَصَله الله في عُمْره ورزقه.
  • صلة الرحم سببٌ لِبَسْطِ الرِّزق وتوسيعه، وسببٌ لطول العمر، وإن كان الأجلُ والرزقُ محددًا إلا أنه قد يكون بركة في الرزق والعمر، فيفعل في عمره أكثر وأنفع مما يفعله غيرُه، وقيل زيادة الرزق والعمر زيادة حقيقية. والله أعلم.

Mada

Ripoti kosa

Zaidi