Hadithi

Atakayedhuru Mwenyezi Mungu naye atamdhuru, na atakayewatia watu ugumu Mwenyezi Mungu naye atamtilia ugumu

Chanzo: HadeethEnc.com, Kiswahili v1.18.0

Ni nzuri (Hasan)Imepokelewa na Abu Daud, Tirmidhiy, Ibn Majah na Ahmad

Matini ya Kiarabu

عن أبي صِرْمة رضي الله عنه أن رسول الله صلى الله عليه وسلم قال: «مَنْ ضَارَّ ضَارَّ اللهُ بِهِ، وَمَنْ شَاقَّ شَقَّ اللهُ عَلَيْهِ».

Tafsiri

kutoka kwa Abuu Swirma -Radhi za Allah ziwe juu yake- Yakwamba Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- amesema: "Atakayedhuru Mwenyezi Mungu naye atamdhuru, na atakayewatia watu ugumu Mwenyezi Mungu naye atamtilia ugumu".

Ufafanuzi

Ametahadharisha Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- kutomuingizia madhara muislamu, au kumtia tabu katika jambo lolote katika mambo yake; Yeye mwenyewe au mali yake au familia yake, nakuwa atakayefanya hivyo basi Mwenyezi Mungu atamlipa na atamuadhibu kwa jinsi alivyomfanyia mwenzake.

Mafunzo

  • Uharamu wa kumdhuru muislamu na kumtia tabu.
  • Allah huwalipizia kisasi waja wake.
Ufafanuzi: العربية

حَذَّرَ النبيُّ صلى الله عليه وسلم مِن إدخالِ المَضَرَّة على المسلم، أو إلحاق المَشَقَّة به في أي أمر من أموره؛ في نفسه أو ماله أو أهله، وأنَّ من فعل ذلك فإن الله يُجازيه ويعاقبُه من جِنْسِ عملِه.

  • تحريم الإضرار بالمسلم وإلحاق المشقة به.
  • انتقام الله لعباده.

Mada

Ripoti kosa

Zaidi