Hadithi

Watafufuliwa watu siku ya Kiyama wakiwa peku, uchi, hawajatahiriwa

Chanzo: HadeethEnc.com, Kiswahili v1.18.0

SahihiWamekubaliana Bukhari na Muslim juu ya usahihi wake

Matini ya Kiarabu

عَنْ عَائِشَةَ أُمِّ المُؤْمنين رَضيَ اللهُ عنها قَالَتْ: سَمِعْتُ رَسُولَ اللهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ يَقُولُ: «يُحْشَرُ النَّاسُ يَوْمَ الْقِيَامَةِ حُفَاةً عُرَاةً غُرْلًا» قُلْتُ: يَا رَسُولَ اللهِ النِّسَاءُ وَالرِّجَالُ جَمِيعًا يَنْظُرُ بَعْضُهُمْ إِلَى بَعْضٍ؟ قَالَ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ: «يَا عَائِشَةُ، الْأَمْرُ أَشَدُّ مِنْ أَنْ يَنْظُرَ بَعْضُهُمْ إِلَى بَعْضٍ».

Tafsiri

Kutoka kwa Aisha radhi za Allah ziwe juu yake- amesema: Nilimsikia Mtume rehema na amani ziwe juu yake- akisema: "Watafufuliwa watu siku ya Kiyama wakiwa peku, uchi, hawajatahiriwa" Nikasema: Ewe Mjumbe wa Mwenyezi Mungu, wanawake na wanaume wote pamoja, kila mmoja anamtazama mwenzake? Akasema rehema na amani ziwe juu yake: "Ewe Aisha, jambo litakuwa kubwa mno, kuliko hata mtu kushughulika kumtazama mwenzake".

Ufafanuzi

Amesimulia Mtume rehema na amani ziwe juu yake baadhi ya yale yatakayokuwa siku ya Kiyama, na kwamba watakusanywa watu baada ya kufufuliwa kutoka makaburini mwao kwa ajili ya hesabu, na hali yao ni kwamba watakuwa miguu peku bila viatu, miili yao ikiwa uchi bila nguo wala kizuizi, na wakiwa hawajatahiriwa kama siku waliyozaliwa na mama zao, aliposikia mama wa Waumini Aisha radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake akasema kwa kustaajabu: Ewe Mjumbe wa Mwenyezi Mungu, wanawake na wanaume wote pamoja kila mmoja akimtazama mwenzake?! Mtume rehema na amani ziwe juu yake akambainishia: Kwa jambo la kisimamo na kukusanywa baada ya kufufuliwa kutoka katika kifo lina misukosuko kiasi kwamba watu macho yao hayatojali kutazama utupu.

Mafunzo

  • Kumebainishwa vitisho vya siku ya Kiyama, na kwamba mtu hakuna kitakachomshughulisha zaidi ya kuwaza hesabu yake na matendo yake.
  • Msisitizo wa kuwa mwanadamu hatumbukii katika maasi isipokuwa katika hali ya kughafilika; kwani lau akikumbuka ukubwa wa anayemuasi au adhabu zake basi asingeghafilika kumkumbuka na kumshukuru na kufanya vizuri ibada zake hata sekunde moja, na ndio maana utawaona watu siku ya Kiyama wameshughulishwa na nafsi zao, hawatazamani.
  • Haya kubwa ya wanawake waliokuwa katika zama za Mtume rehema na amani ziwe juu yake, kwa mfano huyu hapa Aisha radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake, anauliza kwa sababu ya aibu, pale anaposikia kwamba viumbe watakusanywa wakiwa uchi wanaume na wanawake.
  • Amesema Assanadi: Kila mmoja atashughulishwa na jambo lake na wala hatojua hali ya mwenzake, amesema Mwenyezi Mungu Mtukufu: "Kila mtu miongoni mwao siku hiyo atakuwa na lake la kumtosha" [Abasa: 37] Hakuna yeyote atakayegeuka kutazama uchi wa mwenzake.
  • Kutahiriwa: Kwa wanaume: Ni kukata ngozi inayositiri kichwa cha uume, na kwa wanawake: Ni kukata kingozi kilichoko juu mahali pa tundu, kinachofanana na kinyama cha jogoo.
Ufafanuzi: العربية

وصفَ النبيُّ صلى الله عليه وسلم بعضَ ما في يوم القيامة، وأن الناس يُجمعون بعد بعثهم من قبورهم للحساب، وحالهم أنهم حفاة الأقدام بلا نعال، وعراة الأجساد بلا ثياب ولا سِتْر، غُرلًا غير مختونين كيوم ولدتهم أمهاتهم، فلما سمعت أم المؤمنين عائشة رضي الله عنها ذلك قالت متعجبة: يا رسول الله، النساء والرجال جميعًا ينظر بعضهم إلى بعض؟! فبيّن لها النبي صلى الله عليه وسلم: أن شأن الموقف والحشر بعد البعث من الموت فيه من الأهوال ما يأخذ اهتمام الناس وأبصارهم عن النظر إلى العورات.

  • بيان لأهوال يوم القيامة، وأن الإنسان يومئذ لا يشغله شيء عن حسابه وأعماله.
  • تأكيد أن الإنسان لا يقع في المعصية إلا في حالة الغفلة؛ إذ لو تذكر عظمة من عصاه أو عقابه لما غفل عن ذكره وشكره وحسن عبادته طرفة عين، ولذلك ترى أهل المحشر مشغولين بأنفسهم لا ينظر بعضهم إلى بعض.
  • شدة حياء النساء في عهد رسول الله صلى الله عليه وسلم، فهذه عائشة رضي الله عنها تستفسر بحياء عندما تسمع أن الخلق يحشرون عراة رجالًا ونساء.
  • قال السندي: كل مشغول بأمره ولا يدري عن حال أخيه، قال الله تعالى {لِكُلِّ ‌امْرِئٍ ‌مِنْهُمْ ‌يَوْمَئِذٍ ‌شَأْنٌ ‌يُغْنِيهِ} [عبس: 37] فلا أحد يلتفت إلى عورة آخر.
  • الختان: هو للذكر: قطع الجلدة الساترة للحشفة، وللأنثى: قطع جلدة فوق محل الإيلاج تشبه عَرْفَ الدِّيْك.

Mada

Ripoti kosa

Zaidi