Hadithi

Pokea habari njema ya kupewa Nuru mbili hakupewa Nabii yeyote kabla yako: Ufunguzi wa kitabu (Alfatiha) na Aya za mwisho katika Suratul-baqarah, hautasoma herufi miongoni mwa Sura hizo mbili isipokuwa utapewa (unacho hitaji)

Chanzo: HadeethEnc.com, Kiswahili v1.18.0

SahihiImepokelewa Imamu Muslim

Matini ya Kiarabu

عَنِ ابْنِ عَبَّاسٍ رضي الله عنهما قَالَ: «بَيْنَمَا جِبْرِيلُ قَاعِدٌ عِنْدَ النَّبِيِّ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ سَمِعَ نَقِيضًا مِنْ فَوْقِهِ، فَرَفَعَ رَأْسَهُ، فَقَالَ: هَذَا بَابٌ مِنَ السَّمَاءِ فُتِحَ الْيَوْمَ لَمْ يُفْتَحْ قَطُّ إِلَّا الْيَوْمَ، فَنَزَلَ مِنْهُ مَلَكٌ، فَقَالَ: هَذَا مَلَكٌ نَزَلَ إِلَى الْأَرْضِ لَمْ يَنْزِلْ قَطُّ إِلَّا الْيَوْمَ، فَسَلَّمَ، وَقَالَ: أَبْشِرْ بِنُورَيْنِ أُوتِيتَهُمَا لَمْ يُؤْتَهُمَا نَبِيٌّ قَبْلَكَ: فَاتِحَةُ الْكِتَابِ، وَخَوَاتِيمُ سُورَةِ الْبَقَرَةِ، لَنْ تَقْرَأَ بِحَرْفٍ مِنْهُمَا إِلَّا أُعْطِيتَهُ».

Tafsiri

Imepokelewa kutoka kwa bin Abbas -radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yao- amesema: "Pindi Jibrili alipokuwa amekaa kwa Mtume rehema na amani ziwe juu yake alisikia kishindo kutoka juu yake, akanyanyua kichwa chake, akasema: "Huu ni mlango kutoka Mbinguni umefunguliwa leo haukuwahi kufunguliwa kabisa isipokuwa leo, kisha akateremka kutoka kwenye mlango ule Malaika, akasema: "Huyu ni Malaika ameteremka Ardhini hakupata kuteremka kabisa isipokuwa leo, akawasalimia, kisha akasema: "Pokea habari njema ya kupewa Nuru mbili hakupewa Nabii yeyote kabla yako: Ufunguzi wa kitabu (Alfatiha) na Aya za mwisho katika Suratul-baqarah, hautasoma herufi miongoni mwa Sura hizo mbili isipokuwa utapewa (unacho hitaji)"

Ufafanuzi

Malaika Jibril amani iwe juu yake alikuwa amekaa kwa Mtume rehema na amani ziwe juu yake, akasikia sauti kutoka mbinguni kama sauti ya mlango unapofunguliwa, Jibril akanyanyua kichwa chake na macho yake mbinguni, kisha akaeleza Mtume rehema na amani ziwe juu yake ya kwamba mlango huu kutoka mbinguni umefunguliwa leo, na haukuwahi kufunguliwa katu isipokuwa leo, akateremka kutoka humo Malaika kuja Ardhini, hakuwahi kuteremka kabla isipokuwa leo, Malaika akamtolea salamu Mtume rehema na amani ziwe juu yake, na akasema kumwambia: Kuwa na habari njema ya kupata Nuru mbili ulizopewa, ambazo hakuwahi kupewa Nabii yeyote kabla yako; nazo ni: Suratul-Fatiha, na Aya mbili za mwisho wa suratul-Baqara. Kisha Malaika akasema: Hatosoma yeyote harufi moja katika hizo isipokuwa Mwenyezi Mungu atampa yale yaliyomo ndani yake miongoni mwa heri na dua na maombi.

Mafunzo

  • Fadhila za Suratul-Fatiha na mwisho wa Suratul-Baqara, na himizo la kuzisoma na kuyafanyia kazi mafundisho yake.
  • Mbingu zina milango ambayo huteremka amri za Mola kupitia hapo, na wala hazifunguliwi isipokuwa kwa amri ya Mwenyezi Mungu Mtukufu.
  • Kumebainishwa takrima za Mtume rehema na amani ziwe juu yake kwa Mola wake Mlezi, kiasi ambacho amemkirimu kwa mambo ambayo hakuwakirimu Manabii waliokuwa kabla yake, akampatia Nuru hizi mbili.
  • Miongoni mwa nyenzo za kuwalingania watu kwa Mwenyezi Mungu ni kuwapa habari njema.
Ufafanuzi: العربية

كان المَلك جبريل عليه السلام قاعدًا عند النبي صلى الله عليه وسلم، فسمع صوتًا من السماء كصوت الباب إذا فُتح، فرفع جبريل رأسه وبصره إلى السماء، ثم أخبر النبي صلى الله عليه وسلم أن هذا باب من السماء فُتح اليوم، ولم يَسبق أنْ فُتح قط إلا هذا اليوم، فنزل منه ملك من الملائكة إلى الأرض، لم ينزل من قبل إلا هذا اليوم، فسلّم الملك على النبي صلى الله عليه وسلم، وقال له: أبشر بنورين أعطيتهما لم يعطهما نبي قبلك؛ وهما: سورة الفاتحة، وآخر آيتين من سورة البقرة. ثم قال الملك: لن يقرأ أحد بحرف منهما إلا آتاه الله تعالى ما فيهما من الخير والدعاء والطلب.

  • فضل سورة الفاتحة وخواتيم سورة البقرة، والحث على قراءتهما والعمل بما فيهما.
  • السماء لها أبواب ينزل منها الأمر الإلهي، ولا تفتح إلا بأمر الله تعالى.
  • بيان كرامة النبي صلى الله عليه وسلم على ربه، حيث أكرمه بما لم يكرم الأنبياء الذين قبله، فأعطاه هذين النورين.
  • من أساليب الدعوة إلى الله البشارة بالخير.

Mada

Ripoti kosa

Zaidi