Hadithi

Hakika dini ni nyepesi, na hatoifanyia mkazo dini yeyote ila itamshinda, basi shikamaneni na mfanye kadiri ya uwezo yanayoweza kukuwekeni karibu

Chanzo: HadeethEnc.com, Kiswahili v1.18.0

SahihiImepokelewa na Al-Bukhaariy

Matini ya Kiarabu

عَنْ أَبِي هُرَيْرَةَ رضي الله عنه عَنِ النَّبِيِّ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ قَالَ: «إِنَّ الدِّينَ يُسْرٌ، وَلَنْ يُشَادَّ الدِّينَ أَحَدٌ إِلَّا غَلَبَهُ، فَسَدِّدُوا وَقَارِبُوا، وَأَبْشِرُوا، وَاسْتَعِينُوا بِالْغَدْوَةِ وَالرَّوْحَةِ وَشَيْءٍ مِنَ الدُّلْجَةِ».

Tafsiri

Imepokelewa kutoka kwa Abuu Huraira -radhi za Allah ziwe juu yake- kutoka kwa Mtume -rehema na amani ziwe juu yake- amesema: "Hakika dini ni nyepesi, na hatoifanyia mkazo dini yeyote ila itamshinda, basi shikamaneni na mfanye kadiri ya uwezo yanayoweza kukuwekeni karibu, na toeni bishara, na takeni msaada nyakati za asubuhi au mchana au sehemu ya usiku"

Ufafanuzi

Alibainisha wazi Mtume rehema na amani ziwe juu yake kuwa Dini ya Uislamu imeegemezwa katika usahilishaji na wepesi katika mambo yake yote, na usahilishaji unathibitishwa pale panapotokea sababu ya kutokuwa na uwezo na haja, kwa sababu kuzama ndani sana katika matendo ya dini na kuacha upole matokeo yake ni kutoweza na kukoma kufanya amali zote au baadhi yake. Kisha akahimiza rehema na amani ziwe juu yake kuwa kati na kati pasina kupitiliza; Mja asifanye uzembe katika yale aliyoamrishwa, na wala asijibebeshe asiyoyaweza, akishindwa kuifanya amali nzima kamili; basi afanye inayokaribiana na hiyo. Alitoa habari njema Mtume rehema na amani ziwe juu yake ya malipo makubwa ya amali ya kudumu, hata ikiwa ni kidogo, kwa wale ambao hawawezi kufanya amali nzima kikamilifu, kwa sababu ikiwa kushindwa huko hakutokani na yeye mwenyewe, hakutopelekea kupunguzwa kwa malipo yake. Na kwa kuwa ulimwengu huu kwa hakika ni mahala pa kusafiri na mapito ya kuelekea Akhera, ameamrisha rehema na amani ziwe juu yake kutaka msaada katika kudumisha ibada kwa kuiweka nyakati tatu ambazo mtu anakuwa na hamasa: Wakati wa kwanza ni Asubuhi: Kwa kwenda mwanzo wa mchana; kati ya swala ya Alfajiri na kuchomoza jua. Wa pili: Mchana: Kwa kwenda wakati linapopinduka jua. Wa tatu: Giza: kwa mwendo wa usiku mzima au sehemu yake, na kwa sababu amali ya usiku ni ngumu zaidi kuliko amali ya mchana, akaamrisha kufanya baadhi yake, kwa kauli yake: Na baadhi ya usiku.

Mafunzo

  • Wepesi na urahisi wa sheria ya Uislamu, na kuwa kwake ya kati na kati, kati ya uzembe na mkazo.
  • Mja analazimika kufanya matendo kwa kadiri ya uwezo wake, pasina kupuuza au kutia mkazo.
  • Ni lazima mja achague nyakati za kuwa na uchangamfu katika ibada, na nyakati hizi tatu ndizo nyakati bora ambazo mwili unakuwa na uchangamfu katika ibada.
  • Amesema bin Hajar Al-Asqalani: Ni kana kwamba rehema na amani ziwe juu yake amemuelekeza msafiri mahali pa kupelekwa, na nyakati hizi tatu ndizo nyakati bora kwa msafiri, hivyo akamzindua nyakati za uchangamfu wake; Kwa sababu ikiwa msafiri atasafiri mchana na usiku mzima, atakuwa hana uwezo na akakatikiwa, na ikiwa atajitahidi kutembea katika nyakati hizi za uchangamfu basi ataweza kudumu bila tabu.
  • Amesema bin Hajar: Hadithi hii inaashiria kuchukua ruhusa ya kisharia, kwa sababu kufanya ulazima mahali pa ruhusa ni ukiukaji, sawa na mtu anayeacha tayammam wakati hana uwezo wa kutumia maji na kuyatumia kwake kukapelekea kuleta madhara.
  • Amesema bin Munir: Hadithi hii ni miongoni mwa alama za unabii, kwa hakika tuliona na watu waliotangulia pia waliona kuwa kila mwenye kupita kiasi katika dini huishia njiani, na makusudio yake si kuzuia kutaka ukamilifu katika ibada, kwani ni katika mambo ya kusifiwa, bali ni kuzuia uzembe unaopelekea katika uvivu, au kupita mipaka katika jambo la sunna kunakopelekea kuacha kilicho bora, au kuitoa faradhi nje ya wakati wake, kama vile mtu aliyekesha usiku kucha kisha akalala na akapitwa na Swala ya Alfajiri kwa jamaa, au mpaka jua likachomoza na muda wa kuswali ukatoka.
Ufafanuzi: العربية

بَيَّنَ النبيُّ صلى الله عليه وسلم أنَّ دينَ الإسلامِ مبنيٌّ على التيسير والسهولة في كل شؤونه، ويتأكد التيسير عند وجود سبب العجز والحاجة، ولأنَّ التعمُّقَ في الأعمال الدينية وترك الرفق عاقبتُه العجز والانقطاع عن العمل كله أو بعضه، ثم حث صلى الله عليه وسلم على التوسط من غير مبالغة؛ فلا يُقصِّر العبد فيما أُمر به، ولا يتحمل ما لا يطيقه، فإن عجز عن العمل بالأكمل؛ فالعمل على ما يَقْرُبُ منه. وبشَّر صلى الله عليه وسلم بالثواب الجزيل على العمل الدائم وإن قلَّ لمَن عجز عن العمل بالأكمل؛ لأن العجز إذا لم يكن من صنيعه فلا يستلزم نقص أجره. وحيث أن الدنيا في الحقيقة دار سفر ونُقْلة إلى الآخرة أمر صلى الله عليه وسلم بالاستعانة على مداومة العبادة بإيقاعها في الأوقات الثلاثية المنشطة: الأول: الغَدوة: بسير أول النهار؛ ما بين صلاة الفجر وطلوع الشمس. الثاني: الرَّوحة: بالسير بعد الزوال. الثالث: الدُّلْجة: بسير الليل كله أو بعضه، ولأن عمل الليل أشق من عمل النهار أمر ببعضه بقوله: وشيءٍ من الدلجة.

  • يُسر وسماحة الشريعة الإسلامية وتوسُّطها بين الإفراط والتفريط.
  • على العبد أن يأتي بالأمر بقدر استطاعته، من دون تساهل أو تشديد.
  • على العبد أن يختار أوقات النشاط في العبادة، وهذه الأوقات الثلاثة بخصوصها هي أروح ما يكون فيها البدن للعبادة.
  • قال ابن حجر العسقلاني: كأنه صلى الله عليه وسلم خاطب مسافرًا إلى مقصدٍ، وهذه الأوقات الثلاثة أطيب أوقات المسافر، فنبهه على أوقات نشاطه؛ لأن المسافر إذا سافر الليل والنهار جميعًا عجز وانقطع، وإذا تحرَّى السير في هذه الأوقات المنشطة أمكنته المداومة من غير مشقة.
  • قال ابن حجر: الإشارة في هذا الحديث إلى الأخذ بالرخصة الشرعية، فإنّ الأخذ بالعزيمة في موضع الرخصة تَنَطُّعٌ، كمن يترك التيمم عند العجز عن استعمال الماء فيفضي به استعماله إلى حصول الضرر.
  • قال ابن المنير: في هذا الحديث عَلَمٌ من أعلام النبوة، فقد رأينا ورأى الناس قبلنا أن كل متنطع في الدين ينقطع، وليس المراد مَنْعِ طلب الأكمل في العبادة فإنه من الأمور المحمودة، بل منع الإفراط المؤدّي إلى الملال، أو المبالغة في التطوع المفضي إلى ترك الأفضل، أو إخراج الفرض عن وقته كمَن بات يصلي الليل كلَّه فنام عن صلاة الصبح في الجماعة، أو إلى أن طلعت الشمس فخرج وقت الفريضة.

Mada

Ripoti kosa

Zaidi