Hadithi

Ewe Aisha, hakika Mwenyezi Mungu ni Mpole anapenda upole, na hutoa malipo katika upole ambayo hayatoi katika ususuwavu (ukali), na wala hatoi kwa mengineyo

Chanzo: HadeethEnc.com, Kiswahili v1.18.0

SahihiImepokelewa Imamu Muslim

Matini ya Kiarabu

عَنْ عَائِشَةَ أُمِّ المُؤْمِنين رضي الله عنها زَوْجِ النَّبِيِّ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ أَنَّ رَسُولَ اللهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ قَالَ: «يَا عَائِشَةُ إِنَّ اللهَ رَفِيقٌ يُحِبُّ الرِّفْقَ، وَيُعْطِي عَلَى الرِّفْقِ مَا لَا يُعْطِي عَلَى الْعُنْفِ، وَمَا لَا يُعْطِي عَلَى مَا سِوَاهُ».

Tafsiri

Kutoka kwa Aisha Mama wa Waumini radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake, mke wa Mtume rehema na amani ziwe juu yake, ya kwamba Mtume rehema na amani ziwe juu yake alisema: "Ewe Aisha, hakika Mwenyezi Mungu ni Mpole anapenda upole, na hutoa malipo katika upole ambayo hayatoi katika ususuwavu (ukali), na wala hatoi kwa mengineyo".

Ufafanuzi

Alimuhimiza Mtume rehema na amani ziwe juu yake mama wa Waumini Aisha radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake juu ya upole, na kwamba Mwenyezi Mungu ni Mpole kwa waja wake anawatakia wepesi na wala hawatakii ugumu, wala hawalazimishi juu ya uwezo wao, ni wajibu kwa mja wake ajipambe kwa ulaini na kuchukua kilicho rahisi; asiwe mkorofi wala mkali, na kwamba Mwenyezi Mungu Mtukufu hutoa malipo kwa sababu ya upole na ulaini katika dunia kama kusifia vizuri, na kutoa mahitaji ya watu na kurahisisha malengo, na Akhera kutoa thawabu nyingi zaidi kuliko jinsi anavyotoa katika ususuwavu na ukali na ukorofi, upole huja na mambo ambayo hayaji katika mambo mengine.

Mafunzo

  • Himizo juu ya upole na katazo la ukali.
  • Thamani ya nafasi ya upole katika tabia njema zote.
  • Mtu mpole anastahiki sifa nzuri na malipo makubwa kutoka kwa Mwenyezi Mungu Mtukufu.
  • Amesema Assi-ndi: Ukali ni kinyume cha upole, yaani mwenye kuwaita watu kuja katika uongofu kwa upole na kwa huruma ni bora kuliko yule anayewaita kwa ugumu na ukali ikiwa mahali hapo panakubali mambo yote mawili, lau kama si hivyo basi achague kinachoendana na mahala, na Mwenyezi Mungu ndiye Mjuzi zaidi wa uhalisia wa hali.
Ufafanuzi: العربية

حَثَّ النبي صلى الله عليه وسلم أم المؤمنين عائشة رضي الله عنها على الرفق، وأن الله رفيق لطيف بعباده يريد بهم اليسر ولا يريد بهم العسر، فلا يكلفهم فوق طاقتهم، ويحب أن يتصف عبده بلين الجانب والأخذ بالسهل؛ فلا يكون فظًّا ولا غليظًا، وأن الله تعالى يعطي على الرفق واللين في الدنيا من الثناء الجميل ونيل المطالب وتسهيل المقاصد، وفي الآخرة من الثواب الجزيل، أكثر مما يعطيه على العنف والشدة والغلظة، فالرفق يأتي معه ما لا يأتي مع غيره.

  • الحث على الرفق والنهي عن العنف.
  • علو منزلة الرفق بين مكارم الأخلاق.
  • الرفيق يستحق الثناء الجميل والأجر الجزيل من الله تعالى.
  • قال السندي: العنف ضد الرفق أي من يدعو الناس إلى الهدى برفق وتلطف خير من الذي يدعو بعنف وشدة إذا كان المحل يقبل الأمرين، وإلا فيتعين ما يقبله المحل، والله أعلم بحقيقة الحال.

Mada

Ripoti kosa

Zaidi