Chanzo: HadeethEnc.com, Kiswahili v1.18.0
Matini ya Kiarabu
عَنِ ابْنِ عَبَّاسٍ رضي الله عنهما قَالَ: قَالَ رَسُولُ اللهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ: «لَا يَنْظُرُ اللهُ إِلَى رَجُلٍ أَتَى رَجُلًا أَوِ امْرَأَةً فِي دُبُرٍ».
Tafsiri
Imepokelewa kutoka kwa Bin Abbas -radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake- amesema: Amesema Mtume wa Mwenyezi Mungu -rehema na amani ziwe juu yake-: "Hamtazami Mwenyezi Mungu mtu ambaye kamuingilia mwanaume au mwanamke katika tupu yake ya nyuma".
Ufafanuzi
Amebainisha Mtume rehema na amani ziwe juu yake ahadi kali ya adhabu kuwa Mwenyezi Mungu hatomtazama mtazamo wa huruma mwanaume aliyemuingilia mwanaume mwenzake katika utupu wake wa nyuma, au mwanamke katika utupu wake wa nyuma, nakuwa hilo ni dhambi kubwa katika madhambi makubwa.
Mafunzo
- Mwanaume kumwendea mwanaume mwenzake (Ulawiti) ni katika madhambi makubwa.
- Kumwendea mwanamke katika tupu yake ya nyuma ni katika madhambi makubwa.
- "Hamtazami Mwenyezi Mungu" Yaani: Mtazamo wa huruma au upole, na si makusudio yake: Kutazama kwa ujumla; kwa sababu Mwenyezi Mungu Aliyetakasika na kutukuka hakuna chochote kinachofichikana kwake na hakitoweki machoni mwake chochote.
- Matendo haya ni katika machafu makubwa na ni hatari sana kwa binadamu; kwakuwa ndani yake kuna kwenda kinyume na maumbile salama ya kibinadamu, na kupungua kwa kizazi, na kuharibu maisha ya ndoa, na kupandikiza uadui na chuki, na kuingia katika maeneo machafu yenye kutia kinyaa.
Ufafanuzi: العربية
بَيَّنَ النبيُّ صلى الله عليه وسلم الوعيدَ الشديدَ بأنَّ الله لا ينظر نظرةَ رحمةٍ إلى رجلٍ أتى رجلًا في دُبُرِهِ أو امرأة في دُبُرها، وأنه كبيرة من كبائر الذنوب.
- إتيان الرجلِ الرجلَ -وهو اللواط- من كبائر الذنوب.
- إتيان المرأة في دبرها من كبائر الذنوب.
- (لا ينظر الله) أي نظر رحمة ورأفة، وليس المراد به: النظر العام؛ لأن الله سبحانه وتعالى لا يخفى عليه شيء ولا يغيب عن بصره شيء.
- هذه الأعمال من أعظم الفواحش وأخطرها على البشرية؛ لما فيها من مخالفة الفطرة البشرية السليمة، وقلة النسل، وإفساد الحياة الزوجية، وغرس العداوة والبغضاء، والوقوع في الأماكن المستقذرة.