Hadithi

Hakika Mwenyezi Mungu amewafutia umma wangu yale yanayozungumzwa na nafsi zao, madamu hayajafanyiwa kazi au kuzungumzwa

Chanzo: HadeethEnc.com, Kiswahili v1.18.0

SahihiWamekubaliana Bukhari na Muslim juu ya usahihi wake

Matini ya Kiarabu

عَنْ أَبِي هُرَيْرَةَ رَضِيَ اللَّهُ عَنْهُ عَنِ النَّبِيِّ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ قَالَ: «إِنَّ اللَّهَ تَجَاوَزَ عَنْ أُمَّتِي مَا حَدَّثَتْ بِهِ أَنْفُسَهَا، مَا لَمْ تَعْمَلْ أَوْ تَتَكَلَّمْ».

Tafsiri

Imepokelewa kutoka kwa Abuu Huraira -radhi za Allah ziwe juu yake- kutoka kwa Mtume -rehema na amani ziwe juu yake- amesema: "Hakika Mwenyezi Mungu amewafutia umma wangu yale yanayozungumzwa na nafsi zao, madamu hayajafanyiwa kazi au kuzungumzwa".

Ufafanuzi

Anaeleza Mtume rehema na amani ziwe juu yake kuwa Muislamu haadhibiwi kwa mazungumzo ya shari ya nafsi yake kabla ya kuyafanyia kazi au kuyazungumza, kiasi kwamba Mwenyezi Mungu ameondolea uzito na kusamehe, na hakuuandikia makosa umma wa Muhammad rehema na amani ziwe juu yake kwa yale yanayopatikana akilini na yakazunguka katika nafsi bila ya kutulizana nafsi katika hiyo; yakitulizana katika moyo wake, mfano kama kiburi na kujiona au unafiki, au akafanya kwa viungo vyake au akasema kwa ulimi wake basi hapa atahesabiwa.

Mafunzo

  • Mwenyezi Mungu Aliyetakasika na Kutukuka, ameyaacha na kuyasamehe mawazo na fikira zinazojitokeza katika nafsi, mtu huzungumza mwenyewe ndani ya moyo wake na kupita katika mawazo yake.
  • Mtu atakapofikiria talaka, na ikapita akilini mwake, lakini akawa hajaitamka na wala hajaiandika, basi hiyo haizingatiwi kuwa ni talaka.
  • Mazungumzo ya nafsi mtu hahesabiwi vyovyote vile yatakavyokuwa makubwa madam hayajakita ndani ya nafsi yake na akayafanyia kazi au kuyazungumza.
  • Ukubwa wa cheo cha umma wa Muhammad rehema na amani ziwe juu yake kwa kufanywa maalum kwa kutokuadhibiwa kwa mazungumzo ya nafsi, kinyume na umma zilizokuwa kabla yetu.
Ufafanuzi: العربية

يُخْبِرُ النبيُّ صلى الله عليه وسلم أنَّ المسلم لا يُؤاخَذُ بحديث النَّفْس من الشر قبل العمل به أو التكلُّم به، حيث رفع الله الحرج وعفا، ولم يؤاخذ أمة محمد صلى الله عليه وسلم بما وُجِدَ في الذهن وتردد في النفس من غير أن يطمئن إليه ويستقر عنده؛ فإن استقرَّ في قلبه كالكبر أو الخيلاء أو النفاق أو عمل بجوارحه أو قال بلسانه فإنه يؤاخذ بذلك.

  • الله تبارك وتعالى تجاوز وعفا عن الأفكار والهواجس التي تطرأ على النفس، فيحدّث الإنسان بها نفسه، وتمر على خاطره.
  • الطلاق إذا فكَّر فيه الإنسان، وعرض في خاطره، ولكنه لم يتكلم به ولم يكتبه، فإنه لا يعتبر طلاقًا.
  • حديث النفس لا يؤاخذ به الإنسان مهما عظم ما لم يستقر في نفسه ويعمل به أو يتكلم به.
  • عظيم قدر أمة محمد صلى الله عليه وسلم باختصاصها بعدم المؤاخذة بحديث النفس بخلاف الأمم قبلنا.

Mada

Ripoti kosa

Zaidi