Hadithi

Fanyeni mambo kuwa mepesi na wala msiyafanye kuwa magumu, na wapeni watu bishara njema na wala msiwakimbize

Chanzo: HadeethEnc.com, Kiswahili v1.18.0

SahihiWamekubaliana Bukhari na Muslim juu ya usahihi wake

Matini ya Kiarabu

عن أنس بن مالك رضي الله عنه عن النبي صلى الله عليه وسلم قال: «يَسِّرُوا وَلَا تُعَسِّرُوا، وَبَشِّرُوا وَلَا تُنَفِّرُوا».

Tafsiri

Kutoka kwa Anasi bin Maliki -Radhi za Allah ziwe juu yake- kutoka kwa Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- amesema: "Fanyeni mambo kuwa mepesi na wala msiyafanye kuwa magumu, na wapeni watu bishara njema na wala msiwakimbize".

Ufafanuzi

Anaamrisha Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- kuwafanyia wepesi watu na kutowafanyia ugumu katika mambo yote ya Dunia na Akhera, na hili liwe katika mipaka aliyoihalalisha Mwenyezi Mungu na sheria. Na anahimiza kuwapa bishara kwa kheri, na kutowakimbiza.

Mafunzo

  • Wajibu wa muumini ni kuwavutia watu kwa Mwenyezi Mungu na kuwahamasisha katika kheri.
  • Ni wajibu kwa mwenye kuwaita watu kwa Mwenyezi Mungu atazame kwa hekima namna sahihi ya kufikisha ujumbe wa Uislamu kwa watu.
  • Kutoa habari njema huleta furaha na watu kuelekea na kutulizana kwa mlinganiaji na yale anayowafundisha watu.
  • Kuwatia ugumu watu husababisha kuwachukiza watu na kuwakimbiza, na kuyatia shaka maneno ya mfikishaji.
  • Upana wa rehema ya Mwenyezi Mungu kwa waja wake nakuwa Yeye ameridhia kwao dini ya upole na sheria nyepesi.
  • Wepesi ulioamrishwa ni ule uliokuja katika sheria.
Ufafanuzi: العربية

يَأمُرُ النبيُّ صلى الله عليه وسلم بالتخفيف والتيسير على الناس وعدم التَّعْسِيْر عليهم في جميع أمور الدين والدنيا، وذلك في حدود ما أباح الله وشرع. ويَحُثُّ على تَبْشِيرِهم بالخير، وعدم تَنْفِيرِهم منه.

  • واجب المؤمن أن يحبب الناس بالله ويُرغِّبهم في الخير.
  • ينبغي على الداعي إلى الله أن ينظر بحكمة إلى كيفية تبليغ دعوة الإسلام إلى الناس.
  • التبشير يُولِّدُ السرورَ والإقبالَ والاطمئنانَ للداعي ولِمَا يَعرِضه على الناس.
  • التعسير يولِّدُ النفورَ والإدبارَ والتشكيكَ في كلام الداعي.
  • سعة رحمة الله بعباده وأنه رضي لهم دينًا سمحًا وشريعة ميسرة.
  • التيسير المأمور به هو ما جاءت به الشريعة.

Mada

Ripoti kosa

Zaidi